"Mama anatosha" Ni ukosefu Mkubwa wa Maadili wa Vijana wa sasa

"Mama anatosha" Ni ukosefu Mkubwa wa Maadili wa Vijana wa sasa

Minjingu Jingu

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2023
Posts
1,072
Reaction score
2,384
Unapata wapi Ujasiri wa kumwambia Baba yako kuwa Mama yako anatosha asiongeze mwanamke mwingine?

Zamani ilikuwa ngumu sana kuona au kusikia jambo kama hilo. Jamii nzima itakushangaa. Kwa Wamila au Waislamu wanaruhusiwa wake mpaka wa 4. Wewe unaanzaje kumwambia babayo kuwa mama yako anatosha?

Je akikuuliza unajuaje kuwa anatosha? Utajibu nini? Miaka hii unakuta watoto mpaka huingilia ugomvi wa wazazi wao. Ni ukosefu wa maadili kabisa.

Sasa juzi hapa kwa mbali namwona mwanaume kabisa kavaa tshirt imeandikwa nyuma MAMA ANATOSHA 2025. Nikaona huyu kilaza sana. Mambo ya familia yao anautangazia umma. Na je yeye anajuaje kama baba yake anatosheka na mama yake? Angetosha je angekuwa na mwanamke mwingine? Wala kusingekuwa na hiyo haja.

Mama yake hatoshi ndo maana baba yake anataka mwanamke mwingine. Angetosha asingetaka na mwandishi asingeandika kitu hicho.

Tuheshimu maamuzi ya watu.
 
Back
Top Bottom