SI KWELI Mama anayenyonyesha akifanya mapenzi anaweza kumdhoofisha (kumbemenda) mtoto

SI KWELI Mama anayenyonyesha akifanya mapenzi anaweza kumdhoofisha (kumbemenda) mtoto

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Zipo imani na madai ya mbalimbali ya kijamii yanayobainisha namna ambavyo mama anaweza kumdhoofisha (kumbemenda) mtoto wake baadhi ya madai hayo ni:

1. Baba na Mama hawapaswi kujamiiana wakati kipindi cha unyonyeshaji kwa sababu kufanya hivyo hupelekea mtoto wao kudhoofika (kumbemendwa).

2. Lazima mama aoge ajioshe na sabuni kwanza baada ya kujamiiana ndipo amnyonyeshe mtoto wake ili asimbemende.

3. Mama akipata ujauzito wakati bado ananyonyesha anaweza kumbemenda mtoto wake.

4. Mzazi akijamiiana nje ya ndoa akishiriki tena tendo na mwanamke wake anayenyonyesha anambemenda mtoto.


1667450883849.png
 
Tunachokijua
Kubemenda ni nadharia inayohusishwa na udumavu wa mtoto. Ni kitendo kinacho maanisha kushindwa kukua vizuri kwa mtoto kuendana na umri wake.

Udumavu huu huhusisha maeneno muhimu ya ukuaji wa ubongo, kimo, ongezeko la uzito wa mwili na uwezo wa mwili katika kupambana na magonjwa.

Watoto wenye udumavu wa aina hii hupitia changamoto nyingi za kiafya katika makuzi yao na madhara ya changamoto hii huendelea pindi wawapo shuleni na nyakati zingine za maisha yao ya kila siku.

Ukweli upoje?
JamiiCheck imepitia baadhi ya vyanzo mtandaoni ambavyo vinaeleza hoja hiyo ni imani tu za kijamii ambazo hazina ushahidi wa kisayansi.

Vyanzo hivyo vinaeleza kuwa Kitaalamu Baba na Mama wanaruhusiwa kujamiiana (kufanya mapenzi) mara tu baada ya SIKU 42 kupita tangu kujifungua.

Hii ni baada ya kukoma kwa majimaji na uchafu wa uzazi unaoitwa lochia.

Aidha, wataalamu hawa wanaeleza kuwa sababu ya mtoto kudhoofu na kutokua zinaweza kuchangiwa na mambo yafuatayo;
  • Mtoto kutokupata maziwa ya kutosha (mama hanyonyeshi, au hana maziwa ya kutosha au mtoto hanyonyi)
  • Uwepo wa maambukizi ya Magonjwa kama UKIMWI, magonjwa ya kuzaliwa nayo, pneumonia.
  • Mtoto kukosa lishe inayofaa, yaani utapiamlo pia huwa unadhoofisha mtoto na kuleta shida kwenye Ukuaji.
Ili kuboresha ukuaji wa mtoto wataalamu wa afya wanashauri Mama anyonyeshe Mtoto wake ipasavyo mara kwa mara (asipozingatia italeta shida kwenye ukuaji wa mtoto). Aidha, Mtoto anyonye miezi 6 pasipo kumpa kitu kingine chochote, akifika Miezi 6 hakikisha unampa lishe Bora (lishe yenye makundi yote ya vyakula) ili asipate utapiamlo.

Chanzo cha Nadharia hii
JamiiCheck imezungumza na baadhi ya wazee kujua sababu ya kuweka katazo la kufanya mapenzi kwa Mama anayenyonyesha.

Wanaeleza kuwa sababu zilizopelekea kusisitizwa kwa jambo hili ilikuwa ni kuepusha ujauzito wa mapema kabla mtoto hajakua vizuri na kuwafanya wanawake/ wasichana wawe waaminifu katika ndoa zao.

Zaidi ya hayo, JamiiCheck imezengumza na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, Dkt. Godfrey Chale anayepatikana Jijini Dar es Salaam anafafanua:

Mama anayenyonyesha anaweza kuendelea kushiriki tendo na mwenza wake kama kawaida kwa muda wote wa ujauzito kadiri atakavyojisikia na kuona inafaa kwake.

Dhana ya kuwa anaweza kumbemenda mtoto akishiriki kujamiiana sio kweli, kisayansi na kitaalam hakuna ukweli juu ya suala hilo.


Aidha, Dkt. Chale anaeleza kuwa Mama anayenyonyesha akipata ujauzito anatakiwa kuendelea kunyonyesha kama kawaida.

Anatakiwa kufanya hivyo hadi miezi mitatu ya mwisho kabla ya kujifungua, ili maziwa yakate kisha yaanze kujitengeneza mengine kwa ajili ya mtoto atakayezaliwa.

Ikitokea mjamzito ameendelea kunyonyesha hadi anapojifungua, anaweza maziwa yatakosa ubora kiasi, hivyo mtoto atakayezaliwa atakosa maziwa mazuri na hivyo anaweza kukosa afya njema.

HITIMISHO
Hivyo, kutokana na vyanzo hivyo na ufafanuzi Wataalamu wa Afya hoja inayodai Mama anayenyonyesha akifanya mapenzi anaweza kumdhoofisha (kumbemenda) mtoto, haina ukweli.
Siyo kweli. Anayekuambia hiyo ni kweli muulize kama ana watoto, muulize kama alikua ana uwezo wa kuafford lishe (siyo unga wa lishe, namaanisha chakula bora) kwa mtoto na matibabu na kama alikua anaweza afford lishe, mtoto tangu anazaliwa alikua hagomi kula?

Stori za kubemenda zipo uswahilini tu. Hilo neno ukienda kulitamka baadhi ya maeneo wanaomba uwafafanulie.
 
Siyo kweli. Anayekuambia hiyo ni kweli muulize kama ana watoto, muulize kama alikua ana uwezo wa kuafford lishe (siyo unga wa lishe, namaanisha chakula bora) kwa mtoto na matibabu na kama alikua anaweza afford lishe, mtoto tangu anazaliwa alikua hagomi kula?

Stori za kubemenda zipo uswahilini tu. Hilo neno ukienda kulitamka baadhi ya maeneo wanaomba uwafafanulie.
Huko geti kali watoto wanafungiwa ndio maana huwezi kuzisikia lakini jaribu kufika hospital kubwakubwa kuna watoto wanapelekwa kule unaona kabisa huyu keshabemendwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari Wana jamvi,

Nimekua nikisikia Kwamba, Kama ni mwanaume upo kwenye ndoa ama unaish na mwanamke na umebahatika kupata mtoto. Ukianza kutembea na wanawake wengine nje Mtoto wako Afya itaanza kunyong'onyea.

Je, Kuna Ukweli Wowote Kuhusu hili.

Naomba Ufafanuzi

Mshana Jr
GENTAMYCIME
Robert Heriel Mtibeli

Hakuna Kitu kama hicho.

Ishu hapo ni uchafu ambao Watoto wadogo hawatakiwi kuwa contaminated nao.

Mavazi, nguo za kulalia, ngozi ya yeyote atakayembeba mtoto ikiwa na uchafu basi Mtoto anaweza kuumwa.

Ndio maana inashauriwa Baba ukitoka kazini upitie bafuni uoge vizuri ndipo ukambebe mtoto kutokana na Mchana mzima umekutana na kugusana na vitu vingi ambavyo vinaweza kuwa na uchafu uliobeba bacteria, virus n.k
 
Huko geti kali watoto wanafungiwa ndio maana huwezi kuzisikia lakini jaribu kufika hospital kubwakubwa kuna watoto wanapelekwa kule unaona kabisa huyu keshabemendwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Nina watoto mkuu

Hata hospitali hiyo nadharia ya kubemendwa walicheka nilipouliza kisha nikaambiwa ok tuonyeshe connection ya afya ya mtoto kuzorota na babs au mama kutoka nje au wao kujamiiana.

Nikajibu mi ndiyo nawauliza nyinyi mnionyeshe connection wakajibu sisi hatujui ndiyo tunaomba wewe utuonyeshe
 
Nina watoto mkuu

Hata hospitali hiyo nadharia ya kubemendwa walicheka nilipouliza kisha nikaambiwa ok tuonyeshe connection ya afya ya mtoto kuzorota na babs au mama kutoka nje au wao kujamiiana.

Nikajibu mi ndiyo nawauliza nyinyi mnionyeshe connection wakajibu sisi hatujui ndiyo tunaomba wewe utuonyeshe
Sidhani kama hospital wanajua kila kitu.. Maana wana limitations kubwa sana kwenye ufahamu wa haya mambo ndio maana huwezi kutibiwa bila vipimo..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna ukweli mwingi kwenye hili.. Mtoto ni zao la baba na mama na Hicho huwa tegemezi kwa asilimia 100 toka kwa wawili hawa kimwili na kiroho pia
Viwango vya utegemezi hupungua kadiri anavyokua mpaka kuja kujitegemea mwenyewe kwa mambo mengi

Kwahiyo katika umri huo wa utegemezi mkubwa hasa akiwa hajaanza kutembea ni muhimu sana kumlinda kimwili na kiroho
Kiroho ukiachana na haya mengine ya kiimani kuna hili la mtoto kuathirika kama mzazi akichepuka kwakuwa mtu anapochepuka hutengeneza bond na huyo anayechepuka naye na kubeba joto/nishati yake anbapo mzazi asipojitakasa kabla ya kumbeba mtoto lazima aathirike kutokana na joto jipya mwilini mwa mzazi wake

Kina mama waliofunzwa haya mambo huwa hawaruhusu baba ambebe mtoto akitoka alikotoka bila kwanza kumwandalia maji ya kuoga na kubadili nguo.. Lakini pia kina mama hufanya hivyo kama wakichepuka wakati wanalea ana wakifanya na waume zao, japo hili athari zake ni ndogo

Waswahili huita kubemenda mtoto, yaani mtoto anashindwa kusimama na kutembea, afya inadorora na kuumwa mara kwa mara.. Hii hutokea sana kama mzazi asipozingatia usafi na halafu joto la anakochepukia likawa lina nguvu zaidi kuliko la mwenzake home

Kingine ni wasaidizi wa nyumbani nao wakifanya ngono na kuwabeba watoto bila kuoga watoto wanadhurika japo si wazazi wao kwakuwa tayari wanakuwa pia wameshatengeneza bond

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa itakuwaje kwa wale watoto wanaobebwabebwa na watu tofautitofauti?
 
Kumbuka Kila mwanamke unayetembea naye Kuna mawili.
Wengine Wana mapepo Yao yanaweza kuingilia familia yako.
Wengine wanaweza kukufunga na familia yako Ili umuone Bora hata kumchezea mtoto wako
 
Risk zipo ila wanaweza kufanya kama kawaida kwa kuzingatia mama anatakiwa awe ameshapumzika vya kutosha baada ya kujifungua. Maana kujifungua ni sawa na ugonjwa mwanamke anakuwa hahitaji purukushani za siku zote.

Mwanamke mwenye mtoto anae nyonyesha anaweza kufanya mapenzi kama kawaida na mwanaume wake. Ila ni vema yeye na mume wake azingatie mambo kadhaaa kama ifiatavyo:

1. Mwanaume na mwanamke wasiwe watu wa ufuska. Inawezekana mwanaume katoka huko ameshikana na mwanamke sehemu za siri na pengine huyo mwanamke ana maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Yale maji maji na vimelea hubaki kwenye mikono na mwili wa mwanaume sehemu alizoshikana na mwanamke.

So akifika akamgusa mkewe au mtoto ni likely anaweza gusisha vimelea kwa mtoto na mkewe na mkumletea madhara ambayo yanaweza hata kupelekea kubemenda.

2. Katika kufanya mapenzi, mama anayenyonyesha anaweza shika ujauzito tena huku akiwa ananyonyesha. Sasa hii ni mbaya kwasababu maziwa ya mama yataanza kushuka virutubisho kama matokeo ya mwili kuadjust flow ya virutubisho kutoka kutengeneza maziwa na sasa kuuandaa mwili kukuza kichanga kipya tumboni kwa mama.

Mtoto akinyonya haya maziwa atakuwa ananyonya maji tu yasiyokuwa na lishe sawa sawa na mfuga kuku wa kisasa kuwapa vifanga wa wiki moja mapumba badala ya starter,je watakuwa au watadumaa na hata kufa?! Hii itaathiri ubongo, uti wa mgongo na mifupa eventually mtoto anaweza kubemendwa.

Mwanamke anayenyonyesha, ukigundua una ujauzito kimbia clinic haraka utapewa ushauri wa lishe ya mtoto ili umbadilishie na kujiandaa kulea ujauzito mpya haraka sana. Kichanga aliyezaliwa anaweza ishi na kukuzwa kwa maziwa ya kopo na atakuwa vema tu. Wapo watoto mama zao hufariki siku wanazaliwa, unadhani hawa wanalishwaga nini hadi wanakuwa wakubwa?!

3. Sasa kunaeneo jingine ambalo watu hawajui unaweza bemenda mtoto na halihusiani na ngono. Ni eneo la lishe. Mwanamke ni vema sana kuulinda mwili wako kwa kula 80% ya vyakula vyako vya siku vyenye ubora na sio haya ma junk food. Mwili wako muda wowote utakaposhika ujauzito unaanza kufyonza virutubisho mwilini mwako na kuanza kuunda mtoto.

Sasa wewe kama unapenda kula chipsi mayai, soda, beer, na vyakula vingine ambavyo si imara, then jua una alter na kubadilisha DNA signature uliyopewa na ancestors wetu wa Africa. Si unaona wazungu kansa zinavyowasumbua na ni kama zipo embedded kwenye DNA kwa sasa. Mtoto anazaliwa miezi michache tu tayari ana kansa.

Sasa wapo wanawake wanakunywa sana soda wakati wa ujauzito, components za soda zina madhara kwenye ubongo wa mtoto aliyetumboni, unaweza mbemenda hata kabla hajazaliwa anatoka anashida ya uti wa mgongo hawezi kukaa au kutembea. Au unakula mboga za majani zilizofanyiwa fumigation muda mfupi kabla ya kuchumwa, ikipikwa, sumu zinapita kwa mtoto na kuharibu ubongo wake.

Yapo mengi ya kuandika ila nitaishia hapa. Kwa ufupi ni kwamba kubemenda mtoto ni matokeo ya tendo lolote ambalo litasababisha mtoto kutopata ulinzi wa mama yake kiafya na kusababisha damage especially ubongo na uti wa mgongo simply hivyo tu.

So chochote utafanya kuanzia ulaji wako, ngono zembe, na hata watu wanaokuja kumshika mtoto aliyezaliwa ndio maana mila zetu zinashauri siku 40 za kwanza mtoto asitoke nje ili kulinda afya yake awe at least strong.

Yule shost yako anaweza kuja busu mtoto wako mwenye wiki mbili shavuni, mkononi, kwenye paji la uso au mdomoni kumbe ametoka kuFrench Kiss Fiancee wake aliyetoka kulamba chumvini ya side chick ambaye anatoka na mwarabu ambaye anamla tigo na kuchomeka mbele na nyuma na kumpa maradhi yasiyotibika. Mtoto anaweza pata homa kali na kudhurika ubongo pengine hata kufa.

Hata mama anaweza dhuru mtoto wake asipokuwa msafi kwa kuoga vizuri na kunawa mikono yake na kuweka nguo, mazingira ya mtoto na vyombo vya mtoto safi masaa yote.

Ndio maana ni vema na muhimu sana kwa mwanaume unapoamua kujenga familia yako ulinzi unaanza na wewe kujali afya yako, mkeo na mtoto.

Pia ndio maana tunasisitiza sana watoto wa kike kujiandaa kuwa na mke wa mwanaume m'moja ili kuepusha matatizo kama haya. Inaweza tokea mwanaume ni mstaarabu ila mwanamke ni changamoto hajitambui.

Anaingiza wanaume ndani au anaruka na wanaume huku ananyonyesha mtoto. Huku ndipo vimelea vya ngono hutokea. Imagine mwanamke anacheat katoroka kamuacha mtoto na house girl, mume anarudi ghafla, mwanamke anarudi kutoka katika uhuni wake anakuta mume ameshika mtoto anaelia sana sababu hajanyonya.

Panic inamsahaulisha alipotoka anafikia kumshika mtoto na kubeba na kuanza kumnyonyesha titi ambalo alipokuwa anakunjwa jamaa walikuwa wananyonyana sehemu za siri na kunyonyana midomo na jamaa analamba chuchu za mtoto. Mtoto anyonya na kumeza vimelea na vinakwenda kumuathiri.

Au baba katoka nje kupigana mashine na mchepuko wamenyonyana papuchi na dushe na kunyonyana lipsi, jamaa anafika home anaanza kumshika mkewe kwa mahaba, mala wamekiss au pengine na yeye kunyonya chuchu za mtoto ( i hope mshasikia malalamiko ya akina mama kuwa kuna wanaume wananyonya maziwa ya watoto) mtoto anakuja pewa hii chuchu yenye vimelea tayari anaanza kupata changamoto.

Ila pia kuna changamoto ya kisasa ambayo ni ndogo ila inakuwa. Watoto wanapata changamoto kupitia watu tunaowaacha nao majumbani. Kuna case za watoto kufanyiwa matendo ya uchafu na yasiyoelezeka kama kijana kumnyonyesha mtoto wa ndugu yake dushe na shahawa mtoto akazimeza, au house girl kumpeleka uvinza mtoto hadi akafika kileleni. Haya matukio na mengine yasiyoelezeka ni rahisi sana kubemenda mtoto.

Mambo ni mengi tuchukue tahadhari
Nimekuelew saan jamaa kwa ufafanuzi mzuri na makini 👊
 
Zipo imani na madai ya mbalimbali ya kijamii yanayobainisha namna ambavyo mama anaweza kumdhoofisha (kumbemenda) mtoto wake baadhi ya madai hayo ni:

1. Baba na Mama hawapaswi kujamiiana wakati kipindi cha unyonyeshaji kwa sababu kufanya hivyo hupelekea mtoto wao kudhoofika (kumbemendwa).

2. Lazima mama aoge ajioshe na sabuni kwanza baada ya kujamiiana ndipo amnyonyeshe mtoto wake ili asimbemende.

3. Mama akipata ujauzito wakati bado ananyonyesha anaweza kumbemenda mtoto wake.

4. Mzazi akijamiiana nje ya ndoa akishiriki tena tendo na mwanamke wake anayenyonyesha anambemenda mtoto.


Huu upumbavu sijui waliambbiwa na nani sijui
 
Wasalam mabibi na mababu...

Kwanza yote kwa yote nashukuru Mungu wife kanizalia Katoto, mana miongoni mwa factor za kuonyesha urijali ni kupata katoto.

Sasa mara baada ya 40 kuisha nkasema nifate familia niirejeshe Nyumbani lkn wazee, vijana, marafiki wa kila Rika Wamekuwa wakisema usije ukambemenda mtoto, usije ukamuaribu, ingawaj najua hlo kwa Muda tu kuwa ata mkifanya mapenz bas msimshike mtt mpk muoge.

Sasa kichwa changu kinawaza sana yaani kuna uhusiano gani wa kustareheka na mkeo na kumbemenda mtoto?

Iweje kumshika mtoto kulete madhara ya ukuaji wa mtoto?? Yani kuna uhusiano gani wa kimwili na kiroho starehe imdhuru mtoto!!

Nataman kupata faida kwa kiundani sana.
 
Sasa mara baada ya 40 kuisha nkasema nifate familia niirejeshe Nyumbani lkn wazee, vijana, marafiki wa kila Rika Wamekuwa wakisema usije ukambemenda mtoto, usije ukamuaribu, ingawaj najua hlo kwa Muda tu kuwa ata mkifanya mapenz bas msimshike mtt mpk muoge.

Sas kichwa changu kinawaza sn yan kuna uhusiano gn wa kustareheka na mkeo na kumbemenda mtoto? Iweje kumshika mtoto kulete madhara ya ukuaji wa mtoto?? Yan kun uhusiano gn wa kimwil na kiroho starehe imdhuru mtoto!!
Wahenga wazingatiwe,, wanaonaga vitu ambavyo havina majibu kisayansi. Lakini unakuta vina ukweli
 
Hili swala bana sijui huwa lina ukweli au uongo yaani hata halieleweki huko mtaani ila ukija kitaalamu kiafya ni kama halina ukweli ni pale tu mama akiwa busy na mchepuko au vijana afu hazingatii kunyonyesha mtoto basi atadhoofu kiafya sabu hapewi lishe yake kwa usahihi na hajaliwi na mamake hapo lazima wahega waseme mtoto kabemendwa...!!

Ila ukija ki maadili haijakaa sawa mwanamke wako awe na mtoto wako afu eti aende kua anapigwa mpini huko na wajuba afu anakuja kushika mtoto wako bila kuoga huku ana janaba au amnyonyeshe mtoto manyonyo yametoka kushikwa shikwa huko na wahuni, hapo lazima azingue kwa mtoto...
 
Ni kulinda afya ya mtoto, yaani mgegedane na lile jasho + shahawa na mtoto nae aje alale hapo na kumbebabeba na mikono yenu iliyogusanishiana mpaka nnya.

Jiongeze.
 
Back
Top Bottom