Mama Dangote kabla ya kuwa "star" alikuwa "bar maid"

Mama Dangote kabla ya kuwa "star" alikuwa "bar maid"

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Siku zote maisha ni kama gwaride, ukisikia nyuma geuka wa mwisho anakuwa wa kwanza.

Licha ya utajiri na ustaa alionao Bi. Sandra, enzi za ujana wake alishafanya sana kazi za ubaamedi na inavyosemekana hata Mzee Abdul alimkuta kwenye kazi hiyo hiyo ya ubaamedi.

Licha ya ubaamedi, Bi. Sandra aliwahi kuwa mnenguaji kiuno maarufu enzi hizo na alikuwa tishio balaa, bendi kibao zilikuwa zinahitaji huduma yake.

Lakini Mungu hamtupi mja wake, leo hii ukizungumzia wamama wenye mkwanja mrefu basi lazima kwenye hiyo listi Bi. Sandra awepo licha ya kudharaulika sana enzi za ujana wake. Mbaya zaidi kutimuliwa kama mbwa na aliyekuwa mwandani wake, Mzee Abdul.

Hili ni funzo tosha kwenye maisha tusidhalauliane humjui huyu unayemdharau leo kesho atakuwa nani.

Bi. Sandra alidharaulika sana kwa kufanya kazi ya ubaamedi na unenguaji lakini leo hii ndo mwanamama mwenye ushawishi zaidi hapa nchini na hata akitaka agombee ubunge ni rahisi sana kupita kutokana na kukubalika na kundi kubwa la watu.

mama_dangote_20200211_1.jpeg
mama_dangote_20200211_2.jpeg
 
Back
Top Bottom