Ndugu zangu Waislamu na wale wasiokuwa Waislamu au na hata wale vingunge.
Kuna hili jambo linaloendelea katika mitandao kuhusiana na kijana aliejulikana kama Naseeb Abduli ai Diamond Platinum ,whatever ! Hili fukuto linanasibishwa na Uislamu na baadhi ya ndugu zetu wajiitao Mashehe wameingia au kuvutwa katika kutolea hoja jambo hilo.
Nilichokiona na kukusikia kutoka kwa mmoja wa wahusika ambae anasema yeye ndio Baba wa mtoto,ameelezea na katika kuelezea kwa kugusia ndo baada ya kuulizwa Je huyu mama yake Diamond uliwahi kufunga nae ndoa au kumuoa? Jawabu lake alijibu kwa kusema hakuwahi kufunga nae ndoa hata ya mkeka, waliishi pamoja kwa miaka mingi hawakuwahi kufunga ndoa. Kwa maana hiyo walikuwa wazinifu,fulustop.watoto waliowapata wamewapata kwa njia ya uzinifu,ifahamike mtoto hana kosa hata chembe.
Wanataka kuuochomekea Uislamu na vipimo vya DNA, Uislamu unasuala moja tu hapo Je waliowana kama inavyotaka dini ya Uislamu,Kama hilo halipo basi hayo yote ni yao na Uislamu hauna ruhusa ya kushiriki hapo na kama utaingizwa basi hukumu yao watu wawili hao ni kupigwa mawe mpaka wakate roho.
Mashehe mnaotaka kuupaka matope Uislamu kwa kubandikiza aya za kuunga kuunga japo haziungiki kaeni mbali na aibu hizo zinazooibuka ,hayo ni yao na wafuasi wao.