Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Erick Kabendera anasema mama yake alikuwa mwalimu wa enzi za ukoloni na ndiye aliyemfundisha yeye na kumpa ujuzi mwingi wa Kingereza, Historia na Uandishi. Anasema nyumbani kwao kulikuwa na maktaba kubwa ambapo walikuwa wanasoma vitabu vingi sana pamoja na mama yake.
Kabendera anasema hata wakati anakamatwa walikuwa wanajadili Historia ya mataifa ya maziwa makuu na mama yake mwenye miaka 80! Alimpomtembelea mahakamani alihuzunika sana jinsi watu walivyokuwa wananyang'anya haki zao na watu wengine wako kimya tu.
Anasema wakati wa vitu kuu ya pili ya dunia mama yake alitaka kwenda kusoma nje ya Kagera lakini kulikuwa na amri ya wakoloni kuwazuia wanawake wasitoke ndani ya Kagera kwasababu walikuwa wanatorokea Nairobi ambapo inadaiwa walikuwa wanaenda kujiuza na kurudi na magonjws, mama yake na mwanamke mwingine waliandamana kwa mkuu wa wilaya kupinga amri iliyowazuia wanawake wa Kagera kusafiri nje ya Kagera na wakaruhusiwa kusafiri.
Hakika Kabendera alipata mama bora, labda ndio maana inaonekana hana viashiria vya Utanzania. Wamama wengine wa kibongo kipaumbele kwa watoto wao ni kwa Mwamposa, Sunday School, mafundisho ya komunio au Madrasa na wa kike kuolewa. Sifa kubwa ya wamama wengi wa kibongo wakielezewa na watoto wao ni wacha mungu na waliowafundisha maadili. Mama yake Kabendera aliamua kumnoa mwanae katika elimu dunia.