Dear we km na huyo shemela mnapendana na mmeweka malengo ya dhati juu ya maisha yenu kwa pamoja endelea kuwa nae, achana na mbambamba za mama, kikubwa wee ni mtu mzima na unajua nn unafanyaa.
Mama mpe heshima yake km mzazi, mambo yako binafsi uamuzi uko kwako na ni haki yakoo. Kumbuka kuwa huyo jamaa unampenda wee na sio yeye, na hata kuishi utaishi nae wee sio yeye, na hata ya ndani zaidi utayajua wee sio yeye.
Kuwa huru na moyo wako kufuata hitaji lako lilipo, usiishi kwa kutaka kumridhisha huyo mama yako utapata tabu sanaaa, mambo mengine usikubali yeye atie mkono wake atakuharibia mipango yako.
Pambania furaha yako wee mwenyewee, sio kupambania furahaa ya mama yako, hilo ni yake yeye.
Nakusisitiza, fuata moyo wako, maisha ni vile wee unaamua, maisha yako binafsi ni juu yako ni hakii yakoo, hupaswi kuingiliwa.