Mama hamtaki Mpenzi wangu

Mama hamtaki Mpenzi wangu

Kuna wengine humu ni wapuuzi tu na huwa wanatumia uhuru wao wa kutoa maoni vibaya. Maisha ni yako na Nyege ni zako achana na watoto ambao bado wanakula chakula cha Wazazi wao
Yani kanichosha sana mana hayo maswala sijayaongelea hata
 
Habari za saa hii wana Jf

Naomba msaada wenu wa mawazo juu ya swala hili, kama kichwa cha habari kinavyojieleza;
kwa miezi mi3 hii nmekua na mahusiano ya kimapenzi na kijana karibu na maeneo ninayoishi,
  • Mimi binti wa 28 yrs Mpenzi ana 38 aliwahi kuishi na mwanamke kwa miaka kadhaa zamani akaachana na mwanamke wake baada ya kuachishwa kazi ( kampuni ilifilisika)
  • Kwasasa ana biashara zake
-Wote tumeishia 0- level kielimu
-Anataka kunioa pale nikiridhia

Sasa tatizo linaanza baada ya mama kuhisi uhusiano baina yetu, anasema kijana hafai kwanza
-Ana vuta bangi/pombe
-Hajui kuvaa sio mtanashati
- Aliwahi kuishi na mwanamke
-Anatoka familia ya kawaida kama yetu kwahiyo hafai hatanisaidia chochote
- Hana mvuto mbele za watu
-Hana Cv nzuri hata nikimtambulisha
- Anahisi kaniroga ndo mana nmekua nae kimahusiano
-Kwanza anakaa maeneo ya karibu na nyumbani
-Hana hadhi ya kuwa na mimi

Sababu ni nyingi!!

Kwa kuliona hilo tukaamua basi ahame makazi tayari kashahama, mazingira yote tumeyafanya yawe mapya,kwa kila kitu cha hadhu anayoitaka mama,nmeshambadilisha huo muonekano kwa kiasi chake ili afanane na anavyotaka mama ila naona pamoja na kutaka aridhike ila kila siku anaanzisha sababu mpya ya kumkataa anasema anajitutumua tu ili anipate na pombe ameacha anipate akishanioa ntapata shida mana atarudi kwenye mambo yake yote!! Pia namdhalilisha kwa wamama wenzie kwa kuwa na mahusiano na jamaa

- Mama anasema yuko tayari kwenda kwa mganga yoyote akavunje mahusiano mana kwanza jamaa atakua kaniroga sio kawaida.

Sasa hapo nifanyaje wakuu? Maana naona nachanganyikiwa kila siku anaanzisha jambo jipya! ilihali nmemwambia mimi mwenyewe sijasoma! Kazi sina wala bishara yoyote na kijana wa watu ameridhia ana fanya kila jukumu lake bila kinyongo ila mama anasema anafanya mana hana hadhi ya kuwa na ww ndo mana inabidi afanye tu...

Kinachoniumiza ni hakuna siku amewahi niuliza changamoto za maisha yangu ya mahusiano. nmejaribu kumwambia wachumba wakija wakijua sijasoma/sina kazi wanagairi haelewi.. anasema umerogwa wewe
nikiomba space nitulize kichwa sipewi naambiwa mpaka utanielewa...

Nimepata feeling mama yangu ni Toxic /narcissistic mom ila nikieleza hisia zangu yeye ana cheka ndo ananiona kama mpuuzi..

Maana mimi nmemwambia kwanini tusimwachie Mungu tu kama Mungu hajapanga tutaachana tu ila kwa ridhaa yetu mengine tutarekebishana sitaki uwe kama unanipangia maisha ila haelewi kabisa , niko njia panda maana maisha nayaona machungu kabisa ni mimi ndo tatizo au mama? Nishaurini wakubwa kabla sijashuka presha nikazimika mana bi mkubwa kasema kama ntakufa nife mana ndo ilivyopangwa.
Baba yako wa kisirisiri huyo.
 
WhatsApp Image 2023-05-24 at 8.49.49 AM.jpeg
 
kwasasa ni kama ameacha tangu nimkataze hajanywa na wala hakua mlevi ivyo ni mnywaji tu
- mama hakuchaguliwa baba
-ninae kaka angu ila hamfikii wa lolote kwenye kujituma mpaka maendeleo huyu jamaa yuko mbele sana
jamaa yeye amesema tumpe muda ajithibitishe kuwa ni sahihi na anajitahidi ila mama hamtaki
mpaka biashara anataka kunifungulia ila mama hataki
Umeona tatizo lilipo? Hataki na biashara?Mamaako anataka udode

Mamaako sio mtu mzuri kwako

Piga chini olewa atajijua mwenyewe na mawivu yake[emoji57][emoji57]
 
Mamaako anakuonea wivu.... wanawake Wana shida sana

Baba yako yuko wapi?
yupo hapa
ila hajui hili swala mana ni mahusiano tu

ila tu kuna mda akiamua kuturopokea mambo na baba anatujumlisha wote kwamba tunaroho mbaya pale tunaposema haki kuhusu mwanae kipenzi wa kiume ambae hakosei kwenye macho ya mama ake.
anatuambia mimi na baba tunaroho mbaya sana kuingilia maisha ya mwanae
basi mzee wangu anaishia kusema "mama ako anazeeka vibaya"
mana mama akiamua jambo kaamua since day one na anajisifu kabisa kwamba yeye akiamua kaamua
ndo tunanyamazaga na mshua wangu hatuna jinsi
 
Usikute huyo ni kaka yako kwa namna moja au nyingine.
Anaweza kuwa baba wa kambo pia kama mama siyo mzee sana (hapa utanisamehe kwa mawazo haya).
Kingine kuna akina mama wanataka mambo makubwa na sifa kwa majirani.
Inawezekana kuna magonjwa au tabia mbaya za kurithi kwenye familia ya huyo kija, mama anaijua historia yao.
Mwisho fanya maamuzi sahihi kulingana na nafsi inavyo kuambia ila ukumbuke wazazi wanaleta mkosi kwenye ndoa ya watoto wao waliyo ikataa.
 
Back
Top Bottom