Mama hamtaki Mpenzi wangu

Mama hamtaki Mpenzi wangu

Habari za saa hii wana Jf

Naomba msaada wenu wa mawazo juu ya swala hili, kama kichwa cha habari kinavyojieleza;
kwa miezi mi3 hii nmekua na mahusiano ya kimapenzi na kijana karibu na maeneo ninayoishi,
  • Mimi binti wa 28 yrs Mpenzi ana 38 aliwahi kuishi na mwanamke kwa miaka kadhaa zamani akaachana na mwanamke wake baada ya kuachishwa kazi ( kampuni ilifilisika)
  • Kwasasa ana biashara zake
-Wote tumeishia 0- level kielimu
-Anataka kunioa pale nikiridhia

Sasa tatizo linaanza baada ya mama kuhisi uhusiano baina yetu, anasema kijana hafai kwanza
-Ana vuta bangi/pombe
-Hajui kuvaa sio mtanashati
- Aliwahi kuishi na mwanamke
-Anatoka familia ya kawaida kama yetu kwahiyo hafai hatanisaidia chochote
- Hana mvuto mbele za watu
-Hana Cv nzuri hata nikimtambulisha
- Anahisi kaniroga ndo mana nmekua nae kimahusiano
-Kwanza anakaa maeneo ya karibu na nyumbani
-Hana hadhi ya kuwa na mimi

Sababu ni nyingi!!

Kwa kuliona hilo tukaamua basi ahame makazi tayari kashahama, mazingira yote tumeyafanya yawe mapya,kwa kila kitu cha hadhu anayoitaka mama,nmeshambadilisha huo muonekano kwa kiasi chake ili afanane na anavyotaka mama ila naona pamoja na kutaka aridhike ila kila siku anaanzisha sababu mpya ya kumkataa anasema anajitutumua tu ili anipate na pombe ameacha anipate akishanioa ntapata shida mana atarudi kwenye mambo yake yote!! Pia namdhalilisha kwa wamama wenzie kwa kuwa na mahusiano na jamaa

- Mama anasema yuko tayari kwenda kwa mganga yoyote akavunje mahusiano mana kwanza jamaa atakua kaniroga sio kawaida.

Sasa hapo nifanyaje wakuu? Maana naona nachanganyikiwa kila siku anaanzisha jambo jipya! ilihali nmemwambia mimi mwenyewe sijasoma! Kazi sina wala bishara yoyote na kijana wa watu ameridhia ana fanya kila jukumu lake bila kinyongo ila mama anasema anafanya mana hana hadhi ya kuwa na ww ndo mana inabidi afanye tu...

Kinachoniumiza ni hakuna siku amewahi niuliza changamoto za maisha yangu ya mahusiano. nmejaribu kumwambia wachumba wakija wakijua sijasoma/sina kazi wanagairi haelewi.. anasema umerogwa wewe
nikiomba space nitulize kichwa sipewi naambiwa mpaka utanielewa...

Nimepata feeling mama yangu ni Toxic /narcissistic mom ila nikieleza hisia zangu yeye ana cheka ndo ananiona kama mpuuzi..

Maana mimi nmemwambia kwanini tusimwachie Mungu tu kama Mungu hajapanga tutaachana tu ila kwa ridhaa yetu mengine tutarekebishana sitaki uwe kama unanipangia maisha ila haelewi kabisa , niko njia panda maana maisha nayaona machungu kabisa ni mimi ndo tatizo au mama? Nishaurini wakubwa kabla sijashuka presha nikazimika mana bi mkubwa kasema kama ntakufa nife mana ndo ilivyopangwa.

Samahani we ni dini gani?
 
Wahuni sio watu wazuri ebu chunguza mwenyewe mpe mwaka
 
mi nmempa nafasi ajiprove ila mama kasema hataki tu hapo ndo nachoka na sababu zake ndo hizo
Mimi nafikiri sababu lukuki atowazo mamako ni vile hajamkubali mkwee anajaribu kukuvunja moyo ili uachane na jamaa na maana anajaza sababu nyingi,
Ila sababu ya msingi niliyoona hapo kwenye bangi best sio rahisi mzazi kukubali binti yake aolewe na mvuta bangi au hiyo ya uvaaji ukute suruali hadi makalioni harafu boxer nje hata mimi nakuainishia sababu nyingi ili uachane nae tu.
 
Mama anaona mbali sana kwavile mnaishi kwenye jamii moja atakuwa anamfahamu vizuri, mapenzi ni ukipofu hasa kwa vijana mihemuko hutawala tafakari chukua hatua jamii unayoishi nayo itakupa majinu mazuri kuliko sisi humu
 
Na hivyo vitu sio kivile, pombe ameacha tangu nimwambie mi pia staki hivyo vitu akishindwa kuacha tutakua tu casual amenielewa anayafanyia kazi hayo
Hamna kitu kigumu kama kuacha pombe kwa external influence. Walevi wengi huwa wanapumzika tuu kutumia kilevi.
Je Bangi nayo ameacha kuvuta?
 
Mimi nafikiri sababu lukuki atowazo mamako ni vile hajamkubali mkwee anajaribu kukuvunja moyo ili uachane na jamaa na maana anajaza sababu nyingi,
Ila sababu ya msingi niliyoona hapo kwenye bangi best sio rahisi mzazi kukubali binti yake aolewe na mvuta bangi au hiyo ya uvaaji ukute suruali hadi makalioni harafu boxer nje hata mimi nakuainishia sababu nyingi ili uachane nae tu.
Hivi unadhani wanaovuta bangi wote wanavaa mlegezo?? anavaa kawaida tu
wale wa mlegezo ni utoto... mana mimi mwenyewe nmekulia mazingira ya kuona wavutaji nawajua
mama angu basi tu yani
 
Kua makin sana na Mganga atakae mwendea mama ili kuhalibu mahusian yenu.mpe mala2 yaela atakayo toa mama hvo mkeka wamama utakua umechanika.
OVA.
 
Miezi mitatu michache sana...Kaa naye hata mwaka huweza utagundua dosari anazoeleza mama yako..
.halafu unataka kuolewa sababu nawe hujasoma na huna kazi? Hakuna kingine kinachowaunganisha zaidi ya hicho? Unamkubali sababu wapenzi wengine walikusumbua? Huna sababu nyingine? Nadhani mama ana point msikilize fanya uchunguzi.
Anaolewa kwasababu yeye ni mwanamke watu muna maswali ya kiwaki Sana, pia ukisema akae na mtu mwaka mzima kumbuka ana miaka 28 now inamaana huo mwaka mzima akimuona aio sahihi ampate mwengine akiwa na miaka 30 nae amchunguze miaka 3 bila guarantee kuwa sahihi au aio akiona sio sahihi tena si atafika miaka 40 akichunguza watu

Mtu sahihi unamjua ndani ya Week 1 tu ya dating na ndani ya miezi 3 inatosha ku-comfirm kilakitu tuache kuaminishana ujinga
 
Wazazi wetu maisha waliyoishi wao katika ujana wao ni tofauti na maisha ya sasa hivyo hata ushauri wao hauna msaada wowote kwa maisha ya sasa!
Kama umempenda huyo kijana endeleeni na mipango yenu hela zinatafutwa mnaweza kuja kuwa billionaire mpaka watu washangae, maisha ya ndoa hayana formula,
wanasema et bangi na pombe wameacha mengine nilioyasema wameshupalia hayo kama hao watu wa hivyo hawapo kwenye jamii, ntajitahidi kuzingatia ushauri wako mkuu
Halafu wahuni wanajuaga kupenda hao,yaani akiwa na demu wake anamuonjesha nyasi wanablaze pamoja burdan......wanajikuta zao wako Jamaica
hahahahaha ila jamani, mimi anajua sipendi nmekataa
wahuni hata kwa sita by sita shughuli wanakupeaaa haswaaa
ni kweli
Ulieishia o level unajua mambo ya Toxic/ narcissistic mom wewe utakuwa unatuchora tu
Ndio najua Mpaka psycho and the likes
ni kawaida tu mbona mkuu
Nani alikudanganya kuwa mlevi na mvuta bangi huacha ulevi.
Kinachokusumbua wewe ni umri kwenda muda mfupi ujao utajuta
wala na sijasema nataka anioe, nataka kuwa na amani ya mahusiano manake mama anayafatilia sana
😁😁😁 wahuni tuna vitu special, alafu huwa hatu cheat... PM ipo wazi
Kwenye kucheat nakubali
mana sijwahi kusikia wala kuona
Mimi nafikiri sababu lukuki atowazo mamako ni vile hajamkubali mkwee anajaribu kukuvunja moyo ili uachane na jamaa na maana anajaza sababu nyingi,
Ila sababu ya msingi niliyoona hapo kwenye bangi best sio rahisi mzazi kukubali binti yake aolewe na mvuta bangi au hiyo ya uvaaji ukute suruali hadi makalioni harafu boxer nje hata mimi nakuainishia sababu nyingi ili uachane nae tu.
 
kwasasa ni kama ameacha tangu nimkataze hajanywa na wala hakua mlevi ivyo ni mnywaji tu
- mama hakuchaguliwa baba
-ninae kaka angu ila hamfikii wa lolote kwenye kujituma mpaka maendeleo huyu jamaa yuko mbele sana
jamaa yeye amesema tumpe muda ajithibitishe kuwa ni sahihi na anajitahidi ila mama hamtaki
mpaka biashara anataka kunifungulia ila mama hataki
Fata moyo wako.
 
Case yako ni complicated,Maana wa mama nao huwaga na jicho la kuona mbele sana,Ila pia sometimes wanakosaga utu na kupenda tuolewe na wanaume wenye stutus na pesa hata Kama hatuwapendi,kupeana maumivu tu kuishi na mtu usompenda kisa mama
sasa nmempa nafasi anitafutie maana kwa nguvu zangu nmeshindwa
Mama yako anapaswa kukupa ushauri tu na siyo kukupangia uwe na nani katika maisha yako.
ndo nanipangia hapa
Msikilize mama..sawa wazazi wameona MENGI.... akat namaliza chuo kikuu nilipata mchumba ELIMU yake o_level
Nilifight mzee alikua na position ya kuni sapport lakini hakufanya hivyo.....
Akanambia kwanini nataka kuoa wakati Sina hata Masters degree 😊😊
Sikua na kazi by then miaka 15 iliyo pita
Nilisikiliza wazazi now nipo na nimesha kua na mtu mwingine maishani Tupo na good life & happy life ☺️☺️

Sikiliza mzazi wako sawaaa ten years later Rudi hapa kukoment 🤣🤣🤣😂😂😂😂
mimi hizi prediction za yajayo huwa sizipi nafasi mana hata nilikotoka yashanikuta mengi tu maisha ni kumove on, huwezi kuacha kujaribu kisa utafeli
 
Back
Top Bottom