Mama hamtaki Mpenzi wangu

Mama hamtaki Mpenzi wangu

Olewa nae ila jiandae kuwa mfuasi wa Kuhani Musa au Mwamposa kwa misukosuko ya huko mbeleni kwa stress zitakazokupata..
 
Wazazi wetu maisha waliyoishi wao katika ujana wao ni tofauti na maisha ya sasa hivyo hata ushauri wao hauna msaada wowote kwa maisha ya sasa!
Kama umempenda huyo kijana endeleeni na mipango yenu hela zinatafutwa mnaweza kuja kuwa billionaire mpaka watu washangae, maisha ya ndoa hayana formula,
 
Habari za saa hii wana Jf

Naomba msaada wenu wa mawazo juu ya swala hili, kama kichwa cha habari kinavyojieleza;
kwa miezi mi3 hii nmekua na mahusiano ya kimapenzi na kijana karibu na maeneo ninayoishi,
  • Mimi binti wa 28 yrs Mpenzi ana 38 aliwahi kuishi na mwanamke kwa miaka kadhaa zamani akaachana na mwanamke wake baada ya kuachishwa kazi ( kampuni ilifilisika)
  • Kwasasa ana biashara zake
-Wote tumeishia 0- level kielimu
-Anataka kunioa pale nikiridhia

Sasa tatizo linaanza baada ya mama kuhisi uhusiano baina yetu, anasema kijana hafai kwanza
-Ana vuta bangi/pombe
-Hajui kuvaa sio mtanashati
- Aliwahi kuishi na mwanamke
-Anatoka familia ya kawaida kama yetu kwahiyo hafai hatanisaidia chochote
- Hana mvuto mbele za watu
-Hana Cv nzuri hata nikimtambulisha
- Anahisi kaniroga ndo mana nmekua nae kimahusiano
-Kwanza anakaa maeneo ya karibu na nyumbani
-Hana hadhi ya kuwa na mimi

Sababu ni nyingi!!

Kwa kuliona hilo tukaamua basi ahame makazi tayari kashahama, mazingira yote tumeyafanya yawe mapya,kwa kila kitu cha hadhu anayoitaka mama,nmeshambadilisha huo muonekano kwa kiasi chake ili afanane na anavyotaka mama ila naona pamoja na kutaka aridhike ila kila siku anaanzisha sababu mpya ya kumkataa anasema anajitutumua tu ili anipate na pombe ameacha anipate akishanioa ntapata shida mana atarudi kwenye mambo yake yote!! Pia namdhalilisha kwa wamama wenzie kwa kuwa na mahusiano na jamaa

- Mama anasema yuko tayari kwenda kwa mganga yoyote akavunje mahusiano mana kwanza jamaa atakua kaniroga sio kawaida.

Sasa hapo nifanyaje wakuu? Maana naona nachanganyikiwa kila siku anaanzisha jambo jipya! ilihali nmemwambia mimi mwenyewe sijasoma! Kazi sina wala bishara yoyote na kijana wa watu ameridhia ana fanya kila jukumu lake bila kinyongo ila mama anasema anafanya mana hana hadhi ya kuwa na ww ndo mana inabidi afanye tu...

Kinachoniumiza ni hakuna siku amewahi niuliza changamoto za maisha yangu ya mahusiano. nmejaribu kumwambia wachumba wakija wakijua sijasoma/sina kazi wanagairi haelewi.. anasema umerogwa wewe
nikiomba space nitulize kichwa sipewi naambiwa mpaka utanielewa...

Nimepata feeling mama yangu ni Toxic /narcissistic mom ila nikieleza hisia zangu yeye ana cheka ndo ananiona kama mpuuzi..

Maana mimi nmemwambia kwanini tusimwachie Mungu tu kama Mungu hajapanga tutaachana tu ila kwa ridhaa yetu mengine tutarekebishana sitaki uwe kama unanipangia maisha ila haelewi kabisa , niko njia panda maana maisha nayaona machungu kabisa ni mimi ndo tatizo au mama? Nishaurini wakubwa kabla sijashuka presha nikazimika mana bi mkubwa kasema kama ntakufa nife mana ndo ilivyopangw
Ulieishia o level unajua mambo ya Toxic/ narcissistic mom wewe utakuwa unatuchora tu
 
Na hivyo vitu sio kivile, pombe ameacha tangu nimwambie mi pia staki hivyo vitu akishindwa kuacha tutakua tu casual amenielewa anayafanyia kazi hayo

ukimuuliza anasema umemtukana
Nani alikudanganya kuwa mlevi na mvuta bangi huacha ulevi.
Kinachokusumbua wewe ni umri kwenda muda mfupi ujao utajuta
 
Back
Top Bottom