Mama hamtaki Mpenzi wangu

Mama hamtaki Mpenzi wangu

Habari za saa hii wana Jf

Naomba msaada wenu wa mawazo juu ya swala hili, kama kichwa cha habari kinavyojieleza;
kwa miezi mi3 hii nmekua na mahusiano ya kimapenzi na kijana karibu na maeneo ninayoishi,
  • Mimi binti wa 28 yrs Mpenzi ana 38 aliwahi kuishi na mwanamke kwa miaka kadhaa zamani akaachana na mwanamke wake baada ya kuachishwa kazi ( kampuni ilifilisika)
  • Kwasasa ana biashara zake
-Wote tumeishia 0- level kielimu
-Anataka kunioa pale nikiridhia

Sasa tatizo linaanza baada ya mama kuhisi uhusiano baina yetu, anasema kijana hafai kwanza
-Ana vuta bangi/pombe
-Hajui kuvaa sio mtanashati
- Aliwahi kuishi na mwanamke
-Anatoka familia ya kawaida kama yetu kwahiyo hafai hatanisaidia chochote
- Hana mvuto mbele za watu
-Hana Cv nzuri hata nikimtambulisha
- Anahisi kaniroga ndo mana nmekua nae kimahusiano
-Kwanza anakaa maeneo ya karibu na nyumbani
-Hana hadhi ya kuwa na mimi

Sababu ni nyingi!!

Kwa kuliona hilo tukaamua basi ahame makazi tayari kashahama, mazingira yote tumeyafanya yawe mapya,kwa kila kitu cha hadhu anayoitaka mama,nmeshambadilisha huo muonekano kwa kiasi chake ili afanane na anavyotaka mama ila naona pamoja na kutaka aridhike ila kila siku anaanzisha sababu mpya ya kumkataa anasema anajitutumua tu ili anipate na pombe ameacha anipate akishanioa ntapata shida mana atarudi kwenye mambo yake yote!! Pia namdhalilisha kwa wamama wenzie kwa kuwa na mahusiano na jamaa

- Mama anasema yuko tayari kwenda kwa mganga yoyote akavunje mahusiano mana kwanza jamaa atakua kaniroga sio kawaida.

Sasa hapo nifanyaje wakuu? Maana naona nachanganyikiwa kila siku anaanzisha jambo jipya! ilihali nmemwambia mimi mwenyewe sijasoma! Kazi sina wala bishara yoyote na kijana wa watu ameridhia ana fanya kila jukumu lake bila kinyongo ila mama anasema anafanya mana hana hadhi ya kuwa na ww ndo mana inabidi afanye tu...

Kinachoniumiza ni hakuna siku amewahi niuliza changamoto za maisha yangu ya mahusiano. nmejaribu kumwambia wachumba wakija wakijua sijasoma/sina kazi wanagairi haelewi.. anasema umerogwa wewe
nikiomba space nitulize kichwa sipewi naambiwa mpaka utanielewa...

Nimepata feeling mama yangu ni Toxic /narcissistic mom ila nikieleza hisia zangu yeye ana cheka ndo ananiona kama mpuuzi..

Maana mimi nmemwambia kwanini tusimwachie Mungu tu kama Mungu hajapanga tutaachana tu ila kwa ridhaa yetu mengine tutarekebishana sitaki uwe kama unanipangia maisha ila haelewi kabisa , niko njia panda maana maisha nayaona machungu kabisa ni mimi ndo tatizo au mama? Nishaurini wakubwa kabla sijashuka presha nikazimika mana bi mkubwa kasema kama ntakufa nife mana ndo ilivyopangwa.
Nenda ukamseme kwa baba
 
Hata mimi nisingekuozesha yaani mwanaume an a kunywa pombe, bangi ,sigara mie hapana wanakuaga malaya mno

Afu pia wewe umeishia olevel na yeye olevel watoto wenu nani atawafundisha? Tafta hata mkaka mwenye diploma mtoto enu awe inspired kusoma kwa bidii

Usitangulize hisia mbelembele
Wrong
 
Sio mara zote wazazi wako sahihi,, inahitaji maamuzi magumu fuata sauti yako ya ndani kama jamaa amebadili vyote hadi kufikia kuhama mi nakushauri mpe nafasi
Na hapo yawezekana kijana keshalamba sukari ya mama so anakanya yai la kuku sema ndio hivyo mama anashindwa kumfungukia bint kwamba ni kiben teen chake kile kimeshamvua pichu
 
Mimi nafikiri sababu lukuki atowazo mamako ni vile hajamkubali mkwee anajaribu kukuvunja moyo ili uachane na jamaa na maana anajaza sababu nyingi,
Ila sababu ya msingi niliyoona hapo kwenye bangi best sio rahisi mzazi kukubali binti yake aolewe na mvuta bangi au hiyo ya uvaaji ukute suruali hadi makalioni harafu boxer nje hata mimi nakuainishia sababu nyingi ili uachane nae tu.
Na sio kwamba dogo keshaona nyuchi ya mama sasa anakanyaga na mtoto?
 
Yani anataka kunifungulia baishara nijipambanie hata kabla hajanioa
ila anamuogopa mama na mimi ndo mshika dau
ila watu hawajui, wanakazana kusema bangi ooh havutii
sasa leo mama anasema kwanza kwao kuna zezeta baba yao atakua mchawi yani sababu haziishi jamani [emoji119] asubuhi kaniumiza sana mana nilimwambia hao wanaosema hafai pamoja na wewe mnajua mpaka hapa nilipo nmekutana na mangapi??? mnajua ugumu nmepitia kihisia mnajua nmepambana kiasi gani kupata mtu mwenye spirit kama yake nyie mnachoona ni muonekano! mkaka wa watu kanifanya hata shida ndogo ndogo sina! anajitoa muhanga hasa
nmemwambia hao wanaonisema nikikaa home sijaolewa watasema pia ndo mana nmeona nichukue kilichobora kwangu ama ni enjoy wakati huu..
ila akacheka kwa dhihaka na kusema we mpumbavu sana wakati huo mimi naongea kwa machozi
nmeumia sana kuona hajali kabisa hata jinsi ananiumiza. hio picha haifutiki rohoni mwangu ndio ikanifanya nianzishe hii mada nmeumia sana
Eish...hebu endelea na huyo kijana achana na Maza ako[emoji848]

Mzazi ambae chozi la mwanae halimhangaishi ni mama gani huyo hana utu?

Yaan ningekuwa mimi ningepiga chini kumsikiliza, nakuwa busy na mahusiano yangu
 
Huyo Mother wako ana imani za kijinga sana kwenye dunia ya sasa hivi. Kuna Siri kubwa sana kati ya huyo Mama yako na huyo Mpenzi wako. Jaribu kufanya uchunguzi
Huyo maza eidha kaliwa na huyo jamaa au anamtaka jamaa kimapenzi!...

Huyo dada afanye uchunguzi

Kuna kitu nimegundua[emoji848]
 
Eish...hebu endelea na huyo kijana achana na Maza ako[emoji848]

Mzazi ambae chizi la nwanae halimhangaishi na mama gani huyo hana utu?

Yaan ningekuwa mimi ningepiga chini kumsikiliza, nakuwa busy na mahusiano yangu
yani nmeumia sana.
hiko kitendo hakitafutika moyoni
 
kwasasa ni kama ameacha tangu nimkataze hajanywa na wala hakua mlevi ivyo ni mnywaji tu
- mama hakuchaguliwa baba
-ninae kaka angu ila hamfikii wa lolote kwenye kujituma mpaka maendeleo huyu jamaa yuko mbele sana
jamaa yeye amesema tumpe muda ajithibitishe kuwa ni sahihi na anajitahidi ila mama hamtaki
mpaka biashara anataka kunifungulia ila mama hataki
Baba yako yuko hai? Kama yuko hai yeye ana msimamo gani?
 
Wewe hapo umedata na mapigo ya kitandani mie ninamkasa na watu kama hao ushauri kimbia hama na mkoa kabisa kakuendea Kwa mganga na anatumia nyota Yako kachukua nyaya Yako napia , anatumia Kwa biashara zake mkimbie ipo siku utalia halafu , usipende kumwambia mama Yako ndio hapendi huo usiano wenu oho shauri yako
 
kwasasa ni kama ameacha tangu nimkataze hajanywa na wala hakua mlevi ivyo ni mnywaji tu
- mama hakuchaguliwa baba
-ninae kaka angu ila hamfikii wa lolote kwenye kujituma mpaka maendeleo huyu jamaa yuko mbele sana
jamaa yeye amesema tumpe muda ajithibitishe kuwa ni sahihi na anajitahidi ila mama hamtaki
mpaka biashara anataka kunifungulia ila mama hataki
Uongoo
 
Back
Top Bottom