Mama hamtaki Mpenzi wangu

Mama hamtaki Mpenzi wangu

nitalifanyia kazi mkuu

Pole sana Miss Ariana, kumbuka kila mtu anapitia changamoto zake lakini wakati mwingine hili unalopitia usiruhusu liuteke sana ufahamu wako. Wengi humu wamekupa ushauri kwa utashi wao lakini hawana uzoefu na hawajapitia hali ngumu za kihisia kama unazopitia wewe kipindi hiki. Endelea kusonga mbele na maisha yako lakini huyo Mshikaji wako endelea nae usimuache kwa sababu ya maneno ya Mama yako .
 
Nlichogundua hapa nkikweli umerogwa,nipe namba ya mama yako PM nimpe mganga mzuri
 
Pole sana Miss Ariana, kumbuka kila mtu anapitia changamoto zake lakini wakati mwingine hili unalopitia usiruhusu liuteke sana ufahamu wako. Wengi humu wamekupa ushauri kwa utashi wao lakini hawana uzoefu na hawajapitia hali ngumu za kihisia kama unazopitia wewe kipindi hiki. Endelea kusonga mbele na maisha yako lakini huyo Mshikaji wako endelea nae usimuache kwa sababu ya maneno ya Mama yako .
asante nashukuru kwa ushauri mzuri umejitahidi kuhisi nnavyojiskia
 
Hapo ndiyo walipotufikisha mama zetu wa zama hizi,
KUWA MAKINI USHAFIKISHA MIAKA 28 HAPO JUA LISHAANZA KUZAMA UKICHEZA ZAIDI YA HAPO JIANDAE KUWA SINGO MAMA,,,

KAMA ANATAKA MWENYE PESA YEYE BABA YAKO ALIMKUTA ANAZO?

TUNAISHI ZAMA NGUMU SANA
Yani zama ngumu mnoo
yani mpaka nashangaa ni nini hiki mama zetu hebu wajue wakati mwingine hizi ndo ridhiki zetu
 
Wewe hapo umedata na mapigo ya kitandani mie ninamkasa na watu kama hao ushauri kimbia hama na mkoa kabisa kakuendea Kwa mganga na anatumia nyota Yako kachukua nyaya Yako napia , anatumia Kwa biashara zake mkimbie ipo siku utalia halafu , usipende kumwambia mama Yako ndio hapendi huo usiano wenu oho shauri yako
Wabongo bana..mnawaza uchawi uchawi tu
 
Mwanamme mlevi na mwenye kutumia sigara huwa sina mazoea nao kabisa, sasa mwezetu huyo wa kutumia bangi umewezaje? Ama mapenzi yamekuchanganya maana muda mwingine tukikunwa vizuri akili huama.

Embu msikilize mzazi wako, huwenda ukaangukia sehemu salama zaidi tofouti na sasa kwa huyo mlevi na mhuni.
 
Aisee mbona bangi na Pombe kila mtu anatumia Sasa sioni hiyo Kama sababu yenye mashiko .

Hapa TZ watu wengi wanavuta bangi na kinywa pombe na ugoro na hao ndo waoaji waliobaki Zama hizi na mileji zinasoma parefu.
 
Unaandika vzuri kwa mtu alieishia kidato cha nne. Pia una positive mindset which is good.

Ushauri wangu kwa sasa Acha kumwambia mama kila kitu kuhusu mahusiano yako, ikibidi kubali kua umemuacha. Then jipe muda hata wa mwaka mzima kumsoma huyo mtu.
 
Mtu akija kwenu kuoa, mkiridhia DINI na TABIA yake, basi muozesheni. Kwa upande wa TABIA (huenda na DINI pia), mama yako yuko sahihi kuhusu huyo jamaa, changamoto inayoonekana ni kwamba mama yako amechanganya vitu vingi sana; muonekano, uwezo wa kifedha, uvaaji, tabia nk nk. Wakati mwingine hisia zinakuja labda ni "kaka" yako au "baba" yako. In short mambo ni mengi.
 
ni kweli angesema sababu mbili ama3 sio mbaya ila amechanganya mambo mengi kuashiria chuki binafsi
 
Unaandika vzuri kwa mtu alieishia kidato cha nne. Pia una positive mindset which is good.

Ushauri wangu kwa sasa Acha kumwambia mama kila kitu kuhusu mahusiano yako, ikibidi kubali kua umemuacha. Then jipe muda hata wa mwaka mzima kumsoma huyo mtu.
Asante
nashukuru sana kwa hilo na ushauri wako nitaufanyia kazi mkuu
 
Unapendaje mlevi?Unajua ugumu wa kuacha ulevi?Kweli umerogwa
 
Aisee mbona bangi na Pombe kila mtu anatumia Sasa sioni hiyo Kama sababu yenye mashiko .

Hapa TZ watu wengi wanavuta bangi na kinywa pombe na ugoro na hao ndo waoaji waliobaki Zama hizi na mileji zinasoma parefu.
Sisifii ila nmeona vijana wengi sana wanavuta kwanzia huku Uswekeni kwetu mpaka Huko Mbezi beach/Masaki Vijana ambao hudhanii Wanavuta Bangi/sigara/Shisha pombe ndo wanachanganya Spirit/Gin/Whiskey nk Pombe na bangi sio nzuri ila Sio kitu cha ajabu kama mama angu anavyodhani kwenye jamii ya sasa
pia haitafaa kwenye maisha marefu ya ndoa ndio mana hata mimi naliangalia hilo kwasasa ila yeye ni hataki tu anaona hafai kabisa
 
Back
Top Bottom