Mama jirani yangu anamfungia ndani mwanaye mwenye ulemavu

Mama jirani yangu anamfungia ndani mwanaye mwenye ulemavu

FK21

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2019
Posts
8,600
Reaction score
10,760
Ni katika nyumba ya kupanga moja hapa mjini Dar.

Kuna mama ana watoto wawili mmoja wa kike mzima mmoja ni uyo mlemavu nae ni wa kike anamfungia mwanae ndani kisa hawezi kutembea ni mwaka sasa mtoto hajaliona jua zaidi ya kusikika akilia tu.

Je, hii ni sahihi huwa naumia sana nikisikia sauti ya huyo mtoto akilia ndani.

Nawashilikisha wana Jamiforums wenzangu muweze kuona changamoto wanazopitia walemavu.
 
Hakuna kosa hapo anamfungia kwa usalama wake, kosa ni kutompeleka shule kama ana umri wa kwenda shule
 
Nenda ustawi wamfuate kimyakimya
Nadhani wanajamii forums wamekuelekeza vizuri sana, nenda ustawi wa jamii, waeleze uliyoyashuhudia, naamini watachukua hatua stahiki juu ya tukio hili kwani wao ni mamlaka iliyopewa na serikali kushughulikia masuala ya kijamii, kama hili. Tafadhali usisite, na uchukuwe hatua hii mapema kabla mambo hayajaharika zaidi ili umnusuru mtoto huyu.
 
Siwafahamu sasa nawapataje na je akinijua nmemchomesha?
Hata kuwasilisha hapa umefanya vizuri sana. Usikatishwe tamaa na majibu ya kebehi hapa ndivyo ilivyo. Hata ufanye jambo zuri namna gani siyo wote wataridhika. Ila mimi naona ungeeleza vizuri zaidi. Huyo mama anaishi wapi, mtaa gani, na kufika makazi yake unatumia njia gani. Hili litatoa urahisi kwa mtu, mwandishi wa habari au mamlaka kufuatilia. Jambo jingien unalowezakufanya ni kutafuta social media account ya eg Insta, Facebook nk. y hawa wanaharakati wanaofuatilia mambo ya jamii kama kina Joyce Kiria na kuwaandikia ujumbe huku ukiwaelekeza na sehemu. Kama hutaki kujulikana unaweza kutumia username ambazo siyo halisi kama hapa au uwaambie wahusika wasikutaje. Kujitoa kwako kwa dakika tano kunaweza kuokoa maisha ya kiumbe au kuondoa kiumbe kwenye matatizo makubwa.
 
Wanawake live, Mara wanawake jeshi kubwa plus malkia wa nguvu mi nadhani wanawake wangeanza kwanza kuelimishana kuhusiana na changamoto zao wenyewe maana ukiwaweka mahali wanawake wawili pamoja ni kama umemfungia Simba na swala pamoja. Sa wewe mwanao tu wa kumzaa unamtenda Hivyo je jamii itamtendaje harakati zenu zingeanzia kwanza kwenye upendo
 
Hata kuwasilisha hapa umefanya vizuri sana. Usikatishwe tamaa na majibu ya kebehi hapa ndivyo ilivyo. Hata ufanye jambo zuri namna gani siyo wote wataridhika. Ila mimi naona ungeeleza vizuri zaidi. Huyo mama anaishi wapi, mtaa gani, na kufika makazi yake unatumia njia gani. Hili litatoa urahisi kwa mtu, mwandishi wa habari au mamlaka kufuatilia. Jambo jingien unalowezakufanya ni kutafuta social media account ya eg Insta, Facebook nk. y hawa wanaharakati wanaofuatilia mambo ya jamii kama kina Joyce Kiria na kuwaandikia ujumbe huku ukiwaelekeza na sehemu. Kama hutaki kujulikana unaweza kutumia username ambazo siyo halisi kama hapa au uwaambie wahusika wasikutaje. Kujitoa kwako kwa dakika tano kunaweza kuokoa maisha ya kiumbe au kuondoa kiumbe kwenye matatizo makubwa.
Sawa mkuu nitafanya ivyo jambo ambalo sio zuri majirani wakimshauri mtoe acheze na wenzake hataki
 
Kweli hii tabia ni mbaya sana, je ni kweli watu wote hawajajua hilo.

Pengine uhame hapo kwanza ndo uongee na watu wa serikali ya mtaa ili wabebe hilo jukumu, huwezi jua ata react vipi atakapojua umemsemea.

Wapo baadhi wanaharibu watoto wao kisa pesa ila pia ulemavu mwingine ni MAPENZI YA MUNGU.
 
Sawa mkuu nitafanya ivyo jambo ambalo sio zuri majirani wakimshauri mtoe acheze na wenzake hataki
Fanya mkuu. Mungu atakulipa kwa njia nyingine. Hakuna binadamu anayepaswa kukaa ndani muda wote. Hata kama ni mlemavu ana haki ya kucheza na watoto wengine. Kuna cases nyingi zimeshatokea na watoto walipokuja kugundulika baadae walikuwa wamegeuka na kuwa kama misukule kwa kukaa ndani. Nakumbuka kuona kisa kama hiki. Mtoto alilkuwa anasikika kulia ndani na siku majirani walipovamia wakakuta mtoto amefungwa mnyororo kama mbwa na huwezi kujua tena kama ni binadamu.
 
Kweli hii tabia ni mbaya sana, je ni kweli watu wote hawajajua hilo.

Pengine uhame hapo kwanza ndo uongee na watu wa serikali ya mtaa ili wabebe hilo jukumu, huwezi jua ata react vipi atakapojua umemsemea.

Wapo baadhi wanaharibu watoto wao kisa pesa ila pia ulemavu mwingine ni MAPENZI YA MUNGU.
Anaweza kutoa taarifa bila kutoa utambulisho halisi.
 
Kweli hii tabia ni mbaya sana, je ni kweli watu wote hawajajua hilo.

Pengine uhame hapo kwanza ndo uongee na watu wa serikali ya mtaa ili wabebe hilo jukumu, huwezi jua ata react vipi atakapojua umemsemea.

Wapo baadhi wanaharibu watoto wao kisa pesa ila pia ulemavu mwingine ni MAPENZI YA MUNGU.
Hana pesa yeyote anaishi nae chumba kimoja na mmewe na mwanae mwingine wa darasa la 4 ila uyo mlemavu huwa amefungiwa ndani tu inafika kipinndi analia kwa nguvu sana
 
Umesoma ukaelewa? Amesema hamtoi nje! Kama muda wote yuko ndani na hatoki nje hili ni kosa kubwa.
Kosa liko wapi kama ana umri chini ya miaka mitano hakuna kosa mkuu.kosa ni kutompeleka shule kama ana unri wa kuanza shule
 
Back
Top Bottom