Mama Kanumba Atoa siri za mwanae

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
MAMA wa aliyekuwa nguli wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amesema kama kuna msanii anataka kufikia ' levo ' za mwanaye basi asali sana.

Akifunguka mbele ya kinasa sauti cha Risasi Jumamosi, mama Kanumba alisema pengo la mwanaye katika sanaa linaonekana wazi hivyo ni vyema kwa anayetaka kuliziba kufuata nyayo zake .

"Miongoni mwa siri kubwa za mafanikio kwa mwanangu zilizomfanya awike kuliko wengine ni kupenda kuthubutu , kusali sana na kutokuwa na wivu wa maendeleo kwa kujiepusha na majungu.

"Tatizo wasanii wetu hawa hawapendi kuthubutu wamekalia tu kufanyiana majungu , hawapendi kuona mwenzao anafanikiwa wanaanza kumfitini, ni vizuri wangejifunza kitu kwa Kanumba ambaye alipenda kuthubutu , " alisema mama Kanumba .
 
Hana jipya akajipange tuu maana atatudanganya sana
 
Haya ndo maneno tunayotaka kusikia kutoka kwako mama wa super star asiyekuwa na mpinzani east Africa, the late kanumba, sio kutwa kuanza kuropoka sijui mambo ya serengeti, kama ukitulia unaweza kupiga pesa kibao kupitia mwanao, we tupe tu siri za mwanao ata kama za uwongo, maana kuna watu leo kesho wanatamani kufika level za mwanao ila hawajui watafikaje

Aya na nyie mnaojiita makanumha sijui , bi mdashi ndo kashatoa siri kuwa mnatakiwa msali sana sasa sijui wenzangu na mie mtaweza, maana tunawajua nyie kwa MGANGA ndo kuna mungu wenu ,kutwa usharobaro na jeuri halafu eti unataka kuwa kama kanumba. Mama tumekusikia
 
Alikua ana sali sana, kwenye dini ipi?

Si alikuwa mwimba kwaya marehemu, jamaa alitoka kwenye familia ya kidini, na kweli kanumba alikuwa yupo tofauti sana na vijana wengine, alikuwa na HEKIMA sana na heshima kwa kila mtu, na ndio maana alifika mbali, hayo mambo mengine ni ya kibinadamu, ila kanumba alikuwa anamjua sana Mungu
 

Hata Diamond akifa mtasema hivi hiviiii
 
Hata Diamond akifa mtasema hivi hiviiii

Nilikuwa namuona marehemu kwa jicho la kitofauti sana, alikuwa mstaarabu sana hilo linajulikana mbona, alikuwa sio mtu wa anasa kihivyo na mashauzi alikuwa hana na ndio maana Daima atakumbukwa, huyo ndomo atakumbukwa kwa ubunifu wake tu ila sio kijana mwenye maadili kama kanumba
 
kwahiyo mpaka sasa bongo movie hakuna aliyefikia level za kanumba?
 

Anaekufa husifiwa tu hata we ukifa utasikia wanakana kua warumi hakua mbea kabisaaaa
 
Anaekufa husifiwa tu hata we ukifa utasikia wanakana kua warumi hakua mbea kabisaaaa

Ahahahahahahahahaahahhhahajajaaajjahahahaaahahahahah

Binamu leo umeniweza, watasema warumi hakuwa mbea alikuwa anasema kweli kabisa, hahahaaha hahaah chezeya

Halafu binamu najiulizaga kweli, ivi mimi nikifa jamii forum itajua? Itajuaje? Naumizaga kichwa kweli, naona wengine member wakifa watu wanajua
 
Last edited by a moderator:
Adam kuambiana (R.I.P) alikuwa anamnyemelea lakini ndo ivo tena!

Hapana, marehemu kuambiana alikuwa ni zaidi ya kanumba, jamaa was super creative bhana nothing compare in Tz
 

Mimi pia nimewahi kuwaza hili jambo lakini nikawaza hivi....nitamtafuta ndugu yangu muaminifu nitamuambia user name yangu ya huku kwani hakuna ajuae kesho yake hata siku nikifa awaambie member wenzangu...unaonaje wewe?
 
Last edited by a moderator:
Alikuwa anasali sana,siku moja akiwa katika maombi na mwanamaombi mwenzie akatereza akajipiga kichwa ukutani,inasemekana alitumia maji mengi ya baraka mengine yalimwagika akatereza.....

Hahahaaaaa wewe mchokozi sana...sasa kama ndio hivyo lulu ana kesi ya nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…