mbere
JF-Expert Member
- Mar 5, 2015
- 6,967
- 6,465
Hilo halifuti utoto, ukianza fuatilia ni watoto wangapi wanaendesha magari na kwenda club mbona wengi tu...
Maneno hamwelewi hata pichaa
Siku moja baada ya Elizabeth Michael 'Lulu' kuhukumiwa kifungo cha kutumikia jela miaka miwili kwa kosa la kuua bila kukusudia, mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Frora Mutegoa amesema wanaombeza kwa kuishukuru mahakama wamuache kwa hakuna mwenye uchungu zaidi yake.![]()
Jana baada ya Mahakama Kuu kumtia hatiani mwigizaji huyo na kumpa adhabu ya kifungo cha miaka miwili jela, Mama Kanumba aliishukuru mahakama akisema imetenda haki jambo ambalo lilizusha gumzo wengi wakisema hakupaswa kufurahia adhabu hiyo.
Akihojiwa na waandishi wa habari nje ya mahakama kuu jijini Dar es salaam jana Jumatatu baada ya hukumu kutolewa alisema anashukuru kwa kuwa haki imetendeka na kwamba atakwenda kumzika rasmi mtoto wake.
Hata hivyo, Mwananchi leo Jumanne amesema asibezwe kwa kauli hiyo kuwa hakuna anayejua uchungu anaoupata kila siku.
"Mimi sijui kama ninafurahia kama wanavyodai, waulize kwamba, yeye Lulu alipokufa mwanangu Kanumba alifurahia? Mimi ni mkristo, sipendi kuona baya likimfika binadamu mwenzangu, lakini Lulu ameenda miaka miwili jela na atarudi, je mwanangu atarudi lini? nitamwona wapi tena"? Amehoji.