Mama kapata mafao, afanye biashara gani?

Mama kapata mafao, afanye biashara gani?

Mivi

Member
Joined
Oct 5, 2018
Posts
73
Reaction score
53
Habari za leo wakuu,

Naomben mawazo yenu mama yangu amepata mafao ya kustaafu, ameniomba nmshauri afanyaje. Yupo maeneo ya Iringa, nimesema sehemu ili hata unapotoa ushauri uangalie na mazingira.

Japo nilikua nimeanza kubainisha baadhi ya vitu kama anunue pikipiki tuweke vijana, pia ana nyumba zake wamepanga wanafunzi nimemshauri aikarabati iwe na hadhi ya kukaa familia.

Naomben mniongezee mawazo mengine
 
Pamoaja na hayo niomba kujua kasubiri kwa muda gani tangu kustaafu?
 
Ajenge nyumbani zingine apangishe aachane na biashara ya pikipiki, hiyo ni biashara kichaa vijana ni wahuni sana.
Ushauri mzuri watu saivi wanaekeza kwenye majumba biashara itakufa bure kwa kipindi hiki ila nyumba haitakufa abadan utapata pesa na nyumba yako pia utakuwa nayo
 
Kwasasa achukue pesa robo tatu ya pesa yote aliyo nayo aweke fixed account kwa muda hata wa miaka miwili,

Then hiyo pesa inayobaki ndo afikirie biashara ya kufanya( pia anaweza chukua nusu tunya iliyobaki)

Kama biashara itakuwa inalipa na kuzalisha baada ya muda anaongeza pesa nyingine na maisha yanaendelea

Hizo boda boda ataangukia pua mpaka atashangaa
 
ajenge nyumba za kupanga tu.. akinunua hizo boda boda atajuta kuzaliwa.. seke seke za vijana madereva na wezi wa piki piki
 
Habari za leo wakuu , samahan, naomben mawazo yenu mama yangu amepata mafao ya kustaafu , ameniomba nmshauri afanyaje, yupo maeneo ya iringa , nimesema sehemu ili hata unapotoa ushauri uangalie na mazingira, japo nilikua nimeanza kubainisha baadhi ya vitu ,kama anunue pikipiki tuweke vijana,, pia ana nyumba zake wamepanga wanafunzi , nimemshauri aikarabati iwe na hadhi ya kukaa familia, naomben mniongezee mawazo mengine
Yaani hii inaonyesha jinsi ngozi nyeusi tulivyo mbumbumbu ktk kupanga mipango ya maendeleo baada ya kustaafu!
Huyo mama yetu alijua siku moja atastaafu (ktk ideal condition kwamba kifo baadaye) na yawezekana kadunda miaka zaidi ya 30 kazini, inashangazi kwamba baada ya kupata 'mpunga' wake, amechanganyikiwa na hajui nini afanye! All in all, Kwani hana ndugu wa karibu wenye busara na hekima wampatie ushauri mzuri nini afanye? Hapa jukwaani utapigiwa 'miluzi' mingi hadi utachanganyikiwa.
Have a good luck!
 
Habari za leo wakuu , samahan, naomben mawazo yenu mama yangu amepata mafao ya kustaafu , ameniomba nmshauri afanyaje, yupo maeneo ya iringa , nimesema sehemu ili hata unapotoa ushauri uangalie na mazingira, japo nilikua nimeanza kubainisha baadhi ya vitu ,kama anunue pikipiki tuweke vijana,, pia ana nyumba zake wamepanga wanafunzi , nimemshauri aikarabati iwe na hadhi ya kukaa familia, naomben mniongezee mawazo mengine
aanze kuuza donati
 
Back
Top Bottom