Mama kapata mafao, afanye biashara gani?

Mama kapata mafao, afanye biashara gani?

Habari za leo wakuu , samahan, naomben mawazo yenu mama yangu amepata mafao ya kustaafu , ameniomba nmshauri afanyaje, yupo maeneo ya iringa , nimesema sehemu ili hata unapotoa ushauri uangalie na mazingira, japo nilikua nimeanza kubainisha baadhi ya vitu ,kama anunue pikipiki tuweke vijana,, pia ana nyumba zake wamepanga wanafunzi , nimemshauri aikarabati iwe na hadhi ya kukaa familia, naomben mniongezee mawazo mengine
Sinto shangaa vijana wenye adabu ndogo wakikuomba namba ya bimkubwa...teh[emoji28]
 
Akili ishachoka kuna mtu ametoa wazo zuri kama anaeneo na mafao mazuri bora ajenge tu mana akili yake ilishaisha ofisi akisema apambane na biashara stress atakufa mapema bure ujana wake alikuwa wp mshauri ale hela yake taratibu
 
biashara itakayo mfaa kwa umri wake afungue duka vyombo ikae kama part time tu uku akianza kujenga nyumba ili apangashine ila hizo biashara ya usafiri ni pasua kichwa iwe pikipiki au gari asisubutu
 
Atafute location nzuri ya watu afungue duka la makolokolo yaan mahitaji ya kila siku. Au kama hapo mtaani watu wanaonunua mtaani ni wengi aweke duka. Dukani aweke huduma za kifedha kama M-Pesa, TigoPesa n.k
 
Atafute sehemu nzuri penye watu na eneo lenye hatimiliki na vipimo vya ardhi vinavyotambulika, alafu anunue hilo eneo ajenge nyumba either ya kupangisha kwa mtu mmoja mmoja au ajenge guest house. Pesa itayobaki atulie tu atumie kwa matumizi yake binafsi, amshukuru mungu kumpa uhai mrefu. Msimshauri afanye biashara huu ni muda wake wa kupumzika.
 
Mkuu anasema anaona usumbufu wa kusimamia ujenzi
 
Yaani hii inaonyesha jinsi ngozi nyeusi tulivyo mbumbumbu ktk kupanga mipango ya maendeleo baada ya kustaafu!
Huyo mama yetu alijua siku moja atastaafu (ktk ideal condition kwamba kifo baadaye) na yawezekana kadunda miaka zaidi ya 30 kazini, inashangazi kwamba baada ya kupata 'mpunga' wake, amechanganyikiwa na hajui nini afanye! All in all, Kwani hana ndugu wa karibu wenye busara na hekima wampatie ushauri mzuri nini afanye? Hapa jukwaani utapigiwa 'miluzi' mingi hadi utachanganyikiwa.
Have a good luck!
ni nini maana ya kuita JF ni jukwaa la GREAT THINKERS mkuu? mtendee haki muomba ushauri, hayo mengine baki nayo mwenyewe.....
 
watoto wake hamuwezi kumsaidia kusimamia ujenzi?

kama ujenzi hataki aweke fixed deposit 90% ya mafao awe anakula riba tu
Anaweza pia kupata ushauri kwa wajuzi wa mambo ya dhamana za Serikali kwani nimeliona tangazo kwenye social media likinadi juu ya mambo ya dhamana za serikali Benki Kuu.
 
Mshauri Mama ajenge nyumba za kupanga Dodoma
dom sahvi nyumba zinshuka thaman watumish walishahamia wote wameenea
Nyumba sahv zinashushwa bei ili waliojenga mpya nao wawavutie wateja (ni bora kupata mpangaj wa lak1 kulko kukosa kabsa) we kama umejoanga kupga hela dom sahau nakushauri bora ujenge dar
 
Hakuna mstaafu aliyetajirika kwa kuwekeza pension. Hiyo hela mwambie ale pole pole asogeze miaka mingine mitano ya maisha yake. Asisahau kununua ka Vitz ili naye atembee akiwa amekaa.
 
Ajenge nyumbani zingine apangishe aachane na biashara ya pikipiki, hiyo ni biashara kichaa vijana ni wahuni sana.
Kiufupi mafao ya kustaafu sio ya kuanzisha biashara au hata kusomesha watoto /ujenzi Wa nyumba ya kuishi sasa kwa vile alishaanza kuwa na wanafunzi wapangaji ni bora kuimarisha na kujiwekea akiba apate matumizi na matibabu yake
 
Mkuu anasema anaona usumbufu wa kusimamia ujenzi
Duuuh anataka anunue pikipiki maana amna usumbufu wa kununua vile ana hela ni sawa pia boss maana mambo yasiwe mengi na mengi yasiwe mambo
 
Kiufupi mafao ya kustaafu sio ya kuanzisha biashara au hata kusomesha watoto /ujenzi Wa nyumba ya kuishi sasa kwa vile alishaanza kuwa na wanafunzi wapangaji ni bora kuimarisha na kujiwekea akiba apate matumizi na matibabu yake
Kwahiyo unataka aweke chini ya mto awe anajichukulia kidogo kidogo?
 
Back
Top Bottom