Mama kapata mafao, afanye biashara gani?

Mama kapata mafao, afanye biashara gani?

Yaani hii inaonyesha jinsi ngozi nyeusi tulivyo mbumbumbu ktk kupanga mipango ya maendeleo baada ya kustaafu!
Huyo mama yetu alijua siku moja atastaafu (ktk ideal condition kwamba kifo baadaye) na yawezekana kadunda miaka zaidi ya 30 kazini, inashangazi kwamba baada ya kupata 'mpunga' wake, amechanganyikiwa na hajui nini afanye! All in all, Kwani hana ndugu wa karibu wenye busara na hekima wampatie ushauri mzuri nini afanye? Hapa jukwaani utapigiwa 'miluzi' mingi hadi utachanganyikiwa.
Have a good luck!
Genta
 
Kweli kuanza biashara mpya uzeeni sio tombola la uhakika. Uwezekano wa kuua mtaji kabisa ni mkubwa sana.

Kuna wadau wametoa wazo la fixed deposit. Badala ya fixed deposit anaweza kuwekeza kwenye mojawapo ya mifuko ya UTT (hasa Jikimu, Ukwasi) ambapo atakula faida yake 9-10% polepole huku mtaji ukibaki.
 
Habari za leo wakuu , samahan, naomben mawazo yenu mama yangu amepata mafao ya kustaafu , ameniomba nmshauri afanyaje, yupo maeneo ya iringa , nimesema sehemu ili hata unapotoa ushauri uangalie na mazingira, japo nilikua nimeanza kubainisha baadhi ya vitu ,kama anunue pikipiki tuweke vijana,, pia ana nyumba zake wamepanga wanafunzi , nimemshauri aikarabati iwe na hadhi ya kukaa familia, naomben mniongezee mawazo mengine
Ndugu ngoja nikwambie ukweli bila kuficha.
Kwa umri wake biashara inayofaa ni kujenga nyumba za kupangisha tu labda na fremu mbele ya nyumba tu.
Sasa hapo inategemea na mtaji wake ni kiasi gani.
Kwa mfano Kama pesa yake ni Zaid ya milioni 50 ajenge apartments ndogo ndogo Kama nne hivi,yaani chumba sebule mara 4 na kila moja atapangisha kwa laki 1 kwa hyo kila mwezi anapokea laki 4 ita saidia sana.
Kuna biashara zingine hazimfai kwa umri wake bali zinawafaa vijana kwa sababu wakifilisika Wana nguvu za kutafuta pesa tena na kuanza upya.
 
Kwasasa achukue pesa robo tatu ya pesa yote aliyo nayo aweke fixed account kwa muda hata wa miaka miwili,

Then hiyo pesa inayobaki ndo afikirie biashara ya kufanya( pia anaweza chukua nusu tunya iliyobaki)

Kama biashara itakuwa inalipa na kuzalisha baada ya muda anaongeza pesa nyingine na maisha yanaendelea

Hizo boda boda ataangukia pua mpaka atashangaa
Ushauri huu utamsaidia hata mjukuu wake. B blessed bro.
 
Yaani hii inaonyesha jinsi ngozi nyeusi tulivyo mbumbumbu ktk kupanga mipango ya maendeleo baada ya kustaafu!
Huyo mama yetu alijua siku moja atastaafu (ktk ideal condition kwamba kifo baadaye) na yawezekana kadunda miaka zaidi ya 30 kazini, inashangazi kwamba baada ya kupata 'mpunga' wake, amechanganyikiwa na hajui nini afanye! All in all, Kwani hana ndugu wa karibu wenye busara na hekima wampatie ushauri mzuri nini afanye? Hapa jukwaani utapigiwa 'miluzi' mingi hadi utachanganyikiwa.
Have a good luck!
Mtu anaomba ushauri unatoa wosia. Mwaga ushauri mkuu
 
Kama mafao yanamtosha na anapata pension yake kila mwezi huu ni muda wa kupumzika sio kukimbizana na kupeana stress hususan na wapigaji wa kibongo...

Amefanya kazi miaka yake yote.., huu ni muda wa ku-retire, kama yupo bored afanye kitu alichokizoea ili tu asibweteke sio kuanza biashara ambayo hajawahi kuifanya maisha yake yote..., biashara nayo ina skills zake and as they say you can not teach an old dog new tricks....
 
Ajenge hostel nzr kwa ajili ya wanafunzi wa Chuo hapo iringa. I’m very sure hyo itamlipa
 
Pana nyumba Frelimo zinauzwa bei ya kawaida utaiboresha na uhakika wa wapangaji upo pia,na pia kuna nyumba zinauzwa zipo mbili kwenye uwanja mmoja m/40 zina wapangaji tayari wana lipa laki mbili kila mmoja
 
Back
Top Bottom