Mama kasema tukosoe na tushauri suluhu: "Bure Bure" ya NIDA inatuchelewesha

Mama kasema tukosoe na tushauri suluhu: "Bure Bure" ya NIDA inatuchelewesha

Kwa Tanzania yetu ninayoijua unaweza ukalipa na kitambulisho usipate. Mbona Tanesco unalipa na unakaa miezi sita kabla ya kufungiwa umeme.
Mimi huwa najiuliza mbona kitambulisho Cha mpiga kura vilitengenezwa ndani ya muda mfupi. Mkiendekeza kulipia kila kitu tumekwisha. Huduma gani tusiyolipia kwa mlango wa nyuma, huku tunalipa Kodi kibao. Kodi tunazolipa zinatosha kugharimia vitambulisho.
Kitambulisho cha kupigia kura hakina overlay hologram (holographic sign kwaajili ya security) hizi ni alama za kumeta meta ambazo ndio huongeza gharama na muda katika utengenezaji wa kitambulisho kwani huwekwa baada ya kuprint ile kadi (application yake ni kwa kutumia machine au manual) inategemea na uwezo wa hiyo machine.

Sema taratibu nzuri ni kuwa nida wao waweke hizi NIN kwenye database zao kisha kuprint wapewe watu binafsi wenye stationary wa print kisha waende nida wakawekewe zile overays.

Gharama ziwe hivi...
Kuaccess database ya nida kwa kila NIN iwe ni 500
Overlay(hologram) iwe ni 2000 kwasababu hizi ni gharama kutengeneza
Kuprint I'd stationery iwe 5000

Faida yake ni kuokoa muda zaidi, kuongeza mzunguko wa pesa.

Kwa kuwa NIDA Wana ofisi mikoa yote hivyo hologram hizi zipatikane huko kurahisisha utolewaji wa vitambulisho.

NB.
NIDA kuna NIN za watu zinafanana.
 
Back
Top Bottom