Mama kesha Pasua Mbarika Tumuunge Mkono kwa nguvu zote

Mama kesha Pasua Mbarika Tumuunge Mkono kwa nguvu zote

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,775
Reaction score
46,063
Mama bila kumung'unya maneno leo akiongea na Baraza la Maaskofu (TEC), ametamka:

"Corona ipo tuchukue hadhari zote kama tunavyoelekezwa na wataalamu."

Kauli hii ni ya kijasiri kabisa. Heko mama Samia rais wetu kipenzi wa JMT.

Mama ni wa kuungwa mkono kwa nguvu zote na waungwana wote.

"Waungwana kwa maana halisi ya wapenda haki, usawa, demokrasia na maendeleo."

Ni wazi kuwa wapo baina yetu ambao hurukwa na akili kila wasikiapo agenda mbili hizi zikiongelewa popote:

1. Tahadhari dhidi ya Corona
2. Uwepo wa katiba mpya.

Hawa tunawamudu, kwani hawana hoja.

Mama kesha pasua mbarika na yeye ndiye amiri jeshi mkuu!

IMG_20210625_121904_739.jpg


Aungurumapo Simba mcheza nani?
 
Barakoa lazima kwa maneno na si vitendo. COVID-19 inaweza ondoa populality ya chama cha siasa na uongozi....chezea COVID-19. Handle with care!

Labda kwa nia ya mabishano tu ambayo si nia yetu sisi waungwana hata kidogo.

Agenda zetu ni mbili (wazi kabisa):

1. Corona ishughulikiwe kitalaamu
2. Katiba mpya ni jambo la msingi

Wanaorukwa na akili wakiyasikia hayo ituhusu sisi vipi?
 
Njoo mbezi mwisho huku, hakuna tahadhari Wala twahadhari. Corona haipo
 
Mbona tulisha waambia kitambo kuwa Covid itaendelea kuwepo mpaka kwenye August 2022? Au hamkusikia?
 
Njoo mbezi mwisho huku, hakuna tahadhari Wala twahadhari. Corona haipo

Tunawapongeza nyote kwa upole mnaoudumisha sasa.

Matusi haijawahi kuwa maungwana. Si nia yetu kujitangazia ushindi. Hii si leo wala kesho. Kwa kauli hii ya Mama, Tanzania imeshinda!

IMG_20210625_121904_739.jpg


Panapo tatizo la tafsiri jinasibu kusema na kamanda Sirro, msimamizi mkuu wa sheria na matakwa ya serikali kwa ufafanuzi zaidi.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Mama bila kumung'unya maneno leo akiongea na Baraza la Maaskofu, ametamka:

"Corona ipo tuchukue hadhari zote kama tunavyoelekezwa na wataalamu...
Mama anaupiga mwingi sana

Kuna siku chadema watasema mama amekua too nice abadilike

Halafu wataita maandamano ili wapigwe virungu

Acha tusubiri
 
Mama anaupiga mwingi Sana

Kuna siku chadema watasema mama amekua too nice abadilike

Halafu wataita maandamano ili wapigwe virungu

Acha tusubiri

Mama yuko vizuri sana. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Mengine ni ya utabiri kama ya nabii Tito tu. Ya utabiri na ramli kama hizo yanatuhusu nini sisi?

Mama tunamwombea yote ya kheri aendelee kuwaumbua mmoja mmoja, wote wasiomtakia mema.
 
Mnafiki tu naye, kipindi cha dikteta mbona alikuwa hasemi au hapakuwa na corona?

"Kutotambua aina ya uongozi wa juu uliokuwapo na kuwalaumu watendaji kwa uporaji, hujuma, maonevu na ukiukwaji mkubwa wa haki uliokuwapo awamu ile, itakuwa si kututendea haki." Alisikika mbunge mmoja ambaye alikuwa RC kipenzi wa mkoa fulani kipenzi cha aliyekwenda akisisitiza.

Au nasema uongo ndugu zangu.

Haiyumkiniki Mama alikuwa mmoja wa wahanga hao.
 
Mbona tulisha waambia kitambo kuwa Covid itaendelea kuwepo mpaka kwenye August 2022? Au hamkusikia?

Tutakuwa tulikuwa hatujasikia mkuu.

Ila usisahau kuwakumbusha na wenzako hawa kina Countrywide wao bado hawajasikia. Bila shaka hapa watakuwa wanakushangaa kuwa vipi, mbona ghafla na kimya kimya umewahama kambi!

Ila nisiache kukwambia tulijua mtahama kambi na hata kujimilikisha sauti za juu kuliko sisi.

Hiiiiii bagosha!
 
Back
Top Bottom