Nashukuru kwa maoni yako lakini this time around there is an EXTREMELY DIFFERENT SITUATION HENCE DEFINING MOMENT IN THE HISTORY OF OUR COUNTRY AND MAYBE THE WORLD!
Kuna mwamko wa tofauti miongoni mwa wananchi mchungaji fanya uchunguzi utajua hilo!
Huu mwamko wa tofauti uko wapi? Umejiuliza ilikuwaje Chenge na Lowassa wakapokelewa kwa Shangwe kama Wafalme katika majimbo yao? Hivi unafikiri na hoja zote za kuwatuhumu Chenge, Lowassa, Mkulo, Karamagi, Msabaha leo kukifanyika uchaguzi mkuu wakakosa kura za kuwarudisha Bungeni?
Umeulizwa swali zuri sana, kuwa kama nyakati hizi ni za mwamko na mageuzi, ilikuwaje Upinzani ukapigwa ngwala Kiteto?
Be realistic my friend. Hizi kelele za kufoka "kamata mafisadi" zinanikumbusha wakati Lyatonga alipokaribia kuondoka CCM na hata alipoondoka.
Kama ulikuwa mdogo miaka 16 iliyopita, nitakupa kilichotokea na huyo Lyatonga ambacho kilifikia mahali kuanguka vibaya katika siasa za Tanzania.
Mrema alipojitoa CCM baada ya kuvuliwa Uwaziri, alianza kuhangaika kama malaya akitaka ukuu kwa kuwa alijiona kuwa ule umaarufu wake ndio ngao pekee.
Mind you this is typical political behaviour ya Wanasiasa Tanzania ambao wana umashuhuri kujiamini kuwa wao ni Alpha na Omega.
Alikwenda Chadema akamwambia Mtei ampishe Uenyekiti kama sharti la yeye Mrema kujiunga Upinzani. Mtei akamwambia, kwanza inabidi uwe mwanachama, pili itabidi upitie kila ngazi zinazotakiwa ukisubiri wakati Chadema ifanye mkutano mkuu ugombee uenyekiti, na kama ni kutaka kuwa mgombea wa Uraisi kwa Chadema, basi ni shurti upitie mchakato kama wengine. Mrema akalikataa hili, akaenda NCCR ambako wale wanausalama wenzake Mabere Marando, Lamwai na wengine ambao walikuwa ni viongozi, wakampa Uenyekiti harakaharaka ili NCCR kipate umaarufu.
Kilichofuata ni mtiririko wa vurugu ndani ya NCCR mpaka akafukuzwa akaenda TLP ambako nako bado hakujawa na salama.
Una lengo zuri kutaka mabadiliko yafanyike, lakini jifunze kuwa Historia inatuambia nini?
Kama unafikiri kujitoa CCM na kukimbilia Upinzani ni kazi rahisi, waulize wazee makini kama Cleopa Msuya, Salim Ahmed Salim, John Malecela na hata Edward Lowasa wa 1995, kwa nini walibakia CCM na hawakukimbilia huko unakosema ndiko kwenye njia pekee.
Unaposema CCM ni mafisadi, je una maana CCM nzima au sehemu ya CCM ina mafisadi? Maana kumbukumbu zangu zinaniambia kuwa CCM ni chama pekee chenye wanachama wengi kuliko vyama vyote vya upinzani vikijiunga. CCM imejijenga mijini na vijijini kiasi kuwa kila mtu anavuta pumzi inaitwa CCM.
Je unafikiri kuhama CCM ndio suluhisho pekee? Mwanasiasa makini wa CCM kamwe hawezi kufanya kosa la kujidhuru na kujitia kitanzi kama alivyofanya Mrema au Tambwe Hiza!