Wanawake wajasiriamali kutoka Mkoani Arusha wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa uwezeshaji wake wa Mitungi ya gesi takribani 1,000 iliyogaiwa bure kwa wajasiriamali wa chakula Mkoani Arusha, wakisema matumizi ya nishati safi hiyo yamekuwa na manufaa makubwa kwao.
Machi 14, 2025 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda akiwa nje ya Viunga vya Ofisi yake, aligawa mitungi 1,000 kwa Mama lishe na Baba lishe wa Mkoa wa Arusha, akiahidi kuwa awamu nyingine ya pili itafuata, wakigawa majiko 1,000 kwa kila awamu katika jitihada za kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa tija ya afya na utunzaji wa mazingira yanayoharibiwa kutokana na ukataji wa miti kwaajili ya mkaa na kuni.