Uchaguzi 2020 Mama Maria Nyerere: Nimelazimishwa kuja kuongea, niliwaambia nimekuja kuongeza wingi wa watu, Mkutano wa CCM Musoma

Uchaguzi 2020 Mama Maria Nyerere: Nimelazimishwa kuja kuongea, niliwaambia nimekuja kuongeza wingi wa watu, Mkutano wa CCM Musoma

Joyce joyce

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2020
Posts
457
Reaction score
1,973
Wakuu mama Nyerere alipoamushwa kuja kuzungumza kwenye mkutano wa Ccm, katoa Kari ya Mwaka, kasema kuwa yeye hana LA kuongea Kwa sababu amelazimishwa kuja kwenye mkutano huu.



"Mimi kwa bahati nzuri pamoja na Wanamara wenzangu sisi ni kundi lile tulilokuja tuongeze idadi ya watu, vichwa viongozeke kwahiyo sikuja kuzungumza chochote wao walinilazimisha kwamba nizungumze nikasema sina lakuzungumza"- Mama Maria Nyerere

Baada ya ujumbe huu mgumu unaonyesha namna watu wanavyolazimishwa kufanya wasichopenda kufanya, naamini viongozi wamekereka kwa sababu polepole katamka maneno haya:

Mama tunajua una majukumu mengi, endapo ukijisikia kuondoka ondoka upo huru Mwenyekiti amekupa baraka zote.

Huyu mama nadhani ni mara ya kwanza anasimamishwa Kwenye jukwaa la kampeni. Tusiwafanyie hivi watu Hawa waliotumika kwa heshima, waacheni wabaki na heshima yao.
20200905_154643.jpg
20200905_154640.jpg
20200905_154637.jpg
20200905_154634.jpg

 
🙆🏽‍♀️🙆🏽‍♀️🙆🏽‍♀️🙆🏽‍♀️Habari hii haijakamilika bila ushahidi
 
Aibu

Ccm bado wanaamini kua ukoo wa nyerere wanaweza kuwashawishi watu wagumu wa Mara wapige kura kisa mke wa Nyerere? Yule mama wanamsumbua tu.

Mtu kama Makongoro alipata kura 5 kwenye kura za maoni, atamshawishi nani apige kura? Makongoro sijui Madaraka wote walipata kura 7 kwao Butiama, wakashindwa hata kutumia ile PR ya baba yao halafu wanaenda Musoma kupiga kampeni. Wale ni losers, hawana wa kumshawishi.
 
Hivi ni kwa nn ccm inaitenga sana familia ya Nyerere? Hadi kwenye uteuzi wamesusiwa...... Makongoro na madaraka waligombe kuteuliwa ubunge wote wakakatwa na wajumbe na magufuli nae kawakata.....

Ndio maana ccm ina kaana😏😏
 
Back
Top Bottom