Mama mkwe hataki niolewe na mwanaye kisa mimi ni Mchaga

U wife material material mama mkwe hauoni jamani Ila Mimi na Imani kuwa ni sehemu ya maisha siku zote shetani hapendi mambo mazuri ndomana tunapata majaribu Ila namini Mungu yupo mambo yatakuwa sawa tu
Miss chagga ni mwnamke wa ajabu kweli. Ni wife material hakuna mfano nakuhakikishia. Kiuhalisia alivyo ni tofauti na anavyojionesha hapa JF. Kwa bahati namfahamu tangu akiwa kinda
 
U wife material material mama mkwe hauoni jamani Ila Mimi na Imani kuwa ni sehemu ya maisha siku zote shetani hapendi mambo mazuri ndomana tunapata majaribu Ila namini Mungu yupo mambo yatakuwa sawa tu
Nikweleze ulipoteleza?
 
Asante sana ushauri wako ntaufanyia kazi
 
Asante sana
 
Pole dada, hiyo jamii hawajawa tayari kuoana na makabila mengine tofauti na kabila lake..Nina wasiwasi ameanzia kwa mchaga , lakini likipelekwa kabila jingine itakuwa hivyo hivyo.. Halafu huyo mama ameshaanza kuingilia ndoa mapema kabla ya kufungwa.. Inamaanisha ikifungwa tu ataingilia mahusiano ya mwanae na pengine ndivyo alivyo, si rahisi kumbadilisha ... Ila wewe mwenyewe unaweza kubadilika kabla na kuangalia maeneo mengine. Heri nusu shari kuliko shari kamili.... Ninavyojua wamama kama hao , nongwa yao haiishi kwake tu, ataisambaza kwa ndugu wote na atakuwa mwiba kwenye ndoa yenu miaka yote...Nani atapenda kuingia kwenye mahusiano na ndoa ya nongwa hivyo, bora umehabarishwa mapema.... Tafuta kwingine atakuja ambaye Mungu amepanga kwa ajili yako.
 
Nazidi kuchanganyikiwa sijui hata nisimamie upande gani yani ubongo umechoka Kuna kitu kinanisukuma nipige tu mayowe sijui kwanini nahisi ni dalili za kuchanganyikiwa hivi mnajua haya mambo ni magumu sana jamani uwiiiiiiiii!!!! Jana Kuna mtu alishauri huku kuwa ukikubali mfunge ndoa bila ndugu zake watasema umemloga nikaona kweli nikamshauri mchumba angu amuombe mchungaji akaongee na mama yake ili akubali nikamwambia Mimi nataka amani sitaki vita akanijibu nimechoka kuwabembeleza tena usiwaze hilo nmeshasema tunafunga ndoa kuhusu kwetu achana napo uko nshamaliza hakutaka hata niendelee kuongelea hili swala hivi ningefanyaje jamani haya mambo ni mazito jamani acheni usiombe yakukute peke yangu bila Mungu sitoweza yani Kama Jana usiku sijalala hapa naskia tu Kuna sauti inanisukuma nipige mayowe na ninahisi siku ya leo haitopita bila kupiga mayowe ubongo ushastack natamani hata atokee mtu aniteke kupoteza ushahidi maana ujasiri wa kuwaambia kwetu sina kabisa wazazi wangu watakufa na presha wakisikia Jana tu nmemgusia dada yangu juu juu naye presha ikampanda ikabidi tu nimwambie nilikuwa nakutania mambo yako sawa maana alianza hadi kulia sembuse wazazi Ee Mungu naomba nitetee
 
Dada nakuelewa sana yani unaweza ugua KICHAAA so just take care.


Ushauri wangu wa mwisho ambao kimsingi ndio unachotakiwa kufanya. huyo Mchumba wako hana mali kwa sasa so sio kwamba umefata mali hapana. Hao ndugu zake hawakuchukii sababu eti ni mchaga ila bhasi tu hawajakupenda wao binafsi na Kimsingi wewe Hata ndugu wa mwanaume wakikupenda mpaka Kufa na jamaa akawa hakupendi hapo Kweli utapata tabu sana na kimsingi hakuna ndoa lakini ndugu WAKIKUCHUKIA AKIWEPO MAMA MKWE BILA SABABU bhasi jitahidi usiwape sababu huko mbele ya Kumwambia mtoto wao unaona tulikwambia huyu sio mwanamke.



Pole sana lakini KAMA JAMAA KAAMUA AKUOE BILA KUJALI NDUGU ZAKE WEWE HAO NDUGU ZAKE HUJAZALIWA NAO NA UNAENDA KUISHI NA MUMEO.

Sent from my SM-G611K using JamiiForums mobile app
 
Ila jamani tuzungumze generally.. tutoe ukabila.

Kwanini huwa wapenzi wakitangaza ndoa changamoto kama hizi huibuka? Yaan mitihani inakuja ambayo hujawahi hata kuisikia wala kuona

Yupo kijana ametaka kuoa. Kulikuwepo na housegirl kwao. Kale kabinti kalikua kana mambo mengi sana. Kijana wala haishi same place. Anakuja nadra sana anaishi mkoa tofauti...
Binti akaondoka kwa jeuri.. imepita miezi minne binti anatafuta namba ya kijana kwa udi na uvimba hasemi sababu. Kumbe ana mimba kubwa. Mimba ina miezi 6 ila yeye akadanganya lile gap la miez minne aloondoka. Mamake akampigia mama w kijana kumpa taarifa. Binti akapelekwa na mamake walmtoe mimba. Kimchekanes walmtukana mama na mtoto wakamwambia mbona mimba si ya miezi minne ni 6 hii? Mama akapata aibu. Basi binti akakazia kwa bqana harusi mtarajiwa apate namba. Watu wanahoji iweje awe mpenz wako kisha akupe mimba na usiwe na maqasiliano naye?

Binti alikuja kubanwa sana ndo akasema ukweli kwamba alidanganya hajawahi kuwa hata na mahusiano na kijana ila aliangalia wapi kuna nafuu ya misha muangushie mzigo apatenafuu ya maisha yeye na mwanae...

Ndugu, jamaa na marafikiwakashauri kijana ajikaze mitihani ni mingi na mikubwa itazidi kuja muhimu awe makini.

Nimekusimulia hiki kisa chagga ili ujue changamoto kipindi kama hiki huja sana aisee. Yaan usiogope.nakushauri uwe mvumilivu sana kwa sasa. Usifanye maamuzi kuridhisha nafsi yako halaf uje kujuta baadae. Usiogope hata. Kama ni wako atakua wako tu. Ukute hata pia si yeye mumeo munaachana tu unashangaa posa ingine hii hapa muda mfupi na ukaoleewa. Miaka 6 ya mahusiano isikuumize hata kidogo.
 
Umemaliza. Yaan awaprove wrong
 
Umemaliza. Yaan awaprove wrong
Kabisa asibadilike maana wadada wa kichaga na kipare nao jamani kweli sio wote ila asilimia kubwa hujisahau.. Akiolewa anataka amtawale mwanaume yeye ndo awe kichwa cha familia..majibu ya ovyoo hapo mwanaume lazima amwambie mama yake na atakumbuka maneno ya mama yake.

Sent from my SM-G611K using JamiiForums mobile app
 
Kama tu mabinti wa kichaga, harusi kila siku zinafungwa. Watuwacheeeeee
Sisi ni mti wenye matunda...
Halafu sasa mbona huku tunaongoza kutoa mabinti wanaooleka[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Ila wanavyotuandama sasa[emoji1787][emoji1787]
 
Yaani ukisema tu ni "ni mchaga" sura inambadilika hapo hapo
 
Yaani [emoji23][emoji23][emoji23]
Ila chagga and nyaki girls shine banaa. Wapambanaji mnoo[emoji28]
Usikute ndo wanachokiogopa watu.
Maana mwanamke akishaweza jisimamia anaonekana mjeuri...
And yes.. nimejifunza tumelelewa kwa upendo sana makwetu. Na wao wajifunze kulelea watoto wao wa kike kwa upendo wasisahau makwao.

Mtoto wa kike hasahau kwao asilani.
Hapa wanaume wanalalamika tu lakini wanasahau kama sisi ndo watendaji wakuu. Wakishaoaga waanajisahau na ndoa zao sisi ndo tunabaki kuwadekeza wazazi wetu[emoji847]
 
Isijekuwa mchumba wako kapata mchumba mwingine anayekuzidi kila eneo, kamtuma mama aweke kizuizi ili akuache na yeye aendelee na mchumba mpya...!!!
Kama vile uko karibu na ukweli!!
 
Bado mko page na mume wako mtarajiwa na anakwambia mtaoana sasa kwanini unachanganyikiwa? Utajiumiza bure kisha uzue balaa lingine la ugonjwa. Sasa hivi ni kuhakikisha tu kwamba mnaendelea kuwa page moja na hili swala la kutaka upate mimba kabla ya kukuoa achana nalo usije kuishia kuwa singo maza.
Mipango ya harusi yenu July 2020 ni lazima iendelee kwa upande wako mengine mwachie Mwenyezi Mungu.
Pigania hili penzi lenu kadri uwezavyo ila si kwa urozi. Kupoteza mtu uliyekuwa naye miaka 7 mkapendana muda wote huu hadi wote mkaona mnastahili kuwa mke na mume si mchezo.
 
Hii kauli ya kusema sijui mabinti wa kichagga hivi na vile mbona tunaona makabila mengi tuu hawana adabu[emoji28][emoji28]
Hizi mimba za chuki mnazozibeba acheni. Ndo maana tunaamuaga kuwakera humu. Sisi tunawapenda sana tu ila mnazingua sana pia. Mmeshjaiwekea inferiority complex kwamba mabinti wa kichagga tuko hivi basi ndo kila sa mtu unakaa kwa kujihami kulinda title yako ya ubaba. Haifai[emoji28][emoji28] yes.. pesa tunatafuta.
Nawaangalia tu watu wanavyojisifia kuuliwana mabinti wa kichagga as if matajiri kweelii na helaa kibaao kila mtu[emoji23]
 
Sitaki tu kuwa mnafiki nimechukia kweli leo nina siku ya 5 silali nimemeza hadi dawa za usingizi Ila zimegoma nimepungua ndani ya siku 5 kila mtu ananiuliza tatizo nini, mchumba angu nae kapungua yeye ndokabisa hali Bora hata Mimi najikaza nakula kidogo mchumba angu tunapendana sana tumetoka mbali nimemvumilia mengi sana niseme tu kwa kifupi yeye ndo furaha yangu iliyobaki hivi wewe ungeweza kumpenda mtu anayekupitisha kwenye yote haya na hapa mchumba angu Bado yupo upande wangu lakini Bado Nina hali mbaya hivi sipati picha na yeye akinigeuka nahisi sitoweza kuishi tena utakuwa ni mwisho wa maisha yangu alafu unaanzaje kumpenda mtu ananinyima furaha natamani hadi nife kwajili yake hapa naandika hivi huku nalia na maumivu ambayo hayaelezeki wewe usiombe yakukute labda Kama hujawahi kupenda Bora mpendane alafu muachane wenyewe au mwanaume mwenyewe akuache unaweza vumilia badae ukasahau kuliko bado mnapendana Ila mtu anawaachanisha bila sababu ungeijua kidogo historia ya mahusiano yetu nahisi na ww ungenionea huruma tulitoka chuo uzuri nilimaliza nae hatuna hata mia tumeishi maisha magumu sana mpaka inafika hatua tunalalia andazi 1 wakati mwingne hatuli kabisa nimemvumilia ilifika hadi hatua Mimi natafuta ela nasingizia kwetu naumwa Nampa afate kuku vijijini aje auze nampenda sana kutoka moyoni mpaka sahivi tumefanikiwa alafu ndugu zake wananiona sifai alinambia hakuwahi kuwazaga swala la kuoa Ila Mimi ananioa kutokana na wema niliomuonesha ndomana naye anataka tufunge ndoa hata kama ndugu hawataki coz yeye siyo mjinga anajua tulipotoka na tuliyopitia imefika hatua natamani hata itokee shoti ya umeme tuungue tufe watukose wote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…