Wapendwa tumeongea mengi sana humu na kiukweli ni wazi kuwa mwenzetu anahitaji msaada na yuko njia panda na anapitia wakati mgumu sana kwa sasa
ila naomba tu nikumbushe kitu kimoja muhimu sana hapa duniani,kwani nimeona kuna wengine wanaongea katika namna ya wazazi nini banah as long as we umependa basi kazi imeisha
wapendwa naomba tukumbushane kuwa hata sisi ambao leo ndo tuko kwenye process ya kufunga ndoa ni wazazi watarajiwa ambao baadae tutakuwa na mabinti na vijana wetu ambao tungependa watusikilize na watuchukulie sisi kama part ya Maisha yao na watilie maanani maoni na maadili tuliyowapatia,jiulize wewe leo ni mzazi unamuonya mwanao kuhusu kuoa au kuolewa na mtu Fulani kwa sababu umeona wazi kuwa anaweza kumletea shida huko mbeleni,ungependa mwanao aitikieje? ungependa kumwacha mwanao ajiingize kwenye ndoa ambayo itamletea matatizo hapo baadae? au afanye chochote ambacho kitamsababishia shida hapo baadae?
actually sio kila sababu ambayo mzazi anaimpose ina maana au inaweza kutuletea shida kama tutaamua kwenda nayo kinyume,mf mzazi anamkataa mwanamke kwa sababu mbaya hana mvuto mtazaa watoto vituko,au labda hamtaki mwanaume kwa sababu ni masikini hana pesa,what the heck ?????????? Lakin kuna mambo ambayo wazai wetu wameona kwa sababu ya kuishi kwingi hivyo wanapojaribu kutupa opinion zao zenye mashiko na ambazo ni fact tujaribu kupima uzito wa yale wanayotuambia,kwa sababu mara nyingi maonyo ya wazazi huwa hayaanguki hivi hivi,esp kama ni facts.
My take kwako
miss chuga kamwe usipuuze hisia za mama ya mume wako kwa sababu hata wewe kuna siku utakuja kuwa mama mwenye uchungu na upendo sana kwa kijana au binti yako,sidhani kama ungefurahia kuona kijana wako anacut ties na wewe au kupuuza vile unavyohisi kwa ajili ya mwanamke au mwanamume mwingine esp kama utakuwa na sababu za msingi za kutenda au kusema kwa namna moja ama nyingine.
kama unaamini unaweza kumproove wrong mama mkwe na kumfanya ajutie maamuzi ya kukutatalia kuolewa na kijana yake,basi jairibu kutumia hata watu wazima wamshawishi ili akubaliane na ndoa yenu hata kama ni kwa shingo upande ili baada ya hapo umuoneshe kuwa kijana wake hakukosea kukuchagua wewe kama mke
last option kama unaamini umedhamiria kujenga mji na huyo mume wako na unaamini una uwezo wa kurudisha uhusiano mzuri uliopo baina ya mama na mwanaye na kumprove wrong mama mkwe na kama umejaribu mbinu za kutumia watu wazima ikashindikana,basi kafungeni ndoa bomani na mashahidi wenu wawili tu bila kuhusisha upande wowote wa ndugu au wazazi kisha baada ya hapo uanze kazi ya kumrudisha mume wako na mama yake warudi kwenye good terms na kumuonesha kijana wao hakuksea kukuchagua wewe,na kamwe usiache kwani ukifanikiwa utakuwa the best mkwe ambaye wamewahi kuwa naye,na pengine wanaweza kuwa upande wako kuliko unavyotarajia kiasi hata wewe ukikosea wanaamini kijana wao ndo ana shida,mara nyingi ndoa ni kujisacrifice kwa ajili ya furaha ya mtu mwingine
tofauti na hapo usijjingize kwenye hiyo ndoa my dear,ni kweli ndoa ni ya watu wawili,lakini ndoa haipo kwa ajili ya kuwatenganisha na wazazi na ndugu au mahali tulipokulia,na kuna wakati tu katika maisha yetu mtawahitaji wazazi au ndugu au watu wowote zaidi ya ninyi wanandoa wenyewe,thats the fact of life,unaweza ukashangaa mkilazimisha bila bidi yoyote ya kushawishi wazzai hata huyo mumeo ikitokea ishu yoyote serious kati yenu anaweza akaongea maneno yakakuvunja moyo kabisa,utasikia anasema ndo maana mama yangu alikataa ndo mambo kama haya sasa najutia bora ningemsikilizaga mama yangu,
haya mapenzi ni ya mwanzoni tu my dear,ndoa zina mengi marriage is not a bed of roses, inaweza ikafika point mkachokana jamaa anaweza amua hata kuoa mke mwingine kwa kisingizo tu mama yangu aliwahi kunikatalia ila nililazimisha tu ,na wakati huo ukose backup yoyote ile
usilazimishe kuna watu waliachwa siku ya ndoa yenyewe wanasubiria mume/mke kanisani haonekani hiyo aibu yake na maumivu yake hayawezi kufananishwa na hatua uliyofikia wewe,na bado baada ya muda mfupi tu wakapata wenzi wazuri na bora kuliko hao waliowaacha,
so please my dear usifanye maamuzi kwa kurupuka,omba sana mwongozo wa Mungu,tafakari na uchukue hatua,utakuja kuwa mama siku moja na labda ndipo utakapoweza kuzielewa vizuri Zaidi hisia za mama mkwe wako kwa sasa(esp kama ana sababu za msingi kuamua uamuzi wa namna hiyo na hajaamua kuweka wazi)