Mama mkwe hataki niolewe na mwanaye kisa mimi ni Mchaga

Unajua kwanini nashindwa kufanya maamuzi ni kwamba mchumba angu ananipenda sana haijawahi tokea mtu akanipenda kama huyu nawaza naweza muacha naye ataumia alafu hajanikosea chochote pia naweza pata mwanaume mwingine nikaolewa akajakunitesa nitajuta sana nitamkumbuka huyu japo naweza pia kupata Bora zaidi ya huyu Ila sasa ndo Kuna mawili hapo nahofia kuja kujuta badae huyu Kaka naye ananipenda naona kumuacha naye yupo ktk kipindi kigumu itakuwa nmemfanyia ukatili
 
Mimi mama yangu alisema hataki Kuona Mnyakyusa wala Mchaga wa machame...[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] So huwaga nikidate na mtu wa hivyo akianza story za future naonaga bora nimpotezee yani.. Sema kwa kesi yenu mama yake jamaa hakumwambia mapema yani so liwalo na liwe.

Sent from my SM-G611K using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli kipenzi changamoto huwa nyingi hiki kipindi
 
Hapo wa kumsikitikia ni huyo kijana anaejitutumia ukishaonywa na wazazi/mzazi wao wameshaona mbali sema akishupaza shingo mbeleni sijui atakua mgeni wa nani..
 
Hayupo serious yani natamani nikuoe mimi inaonesha mwaminifu sana.
 
Ngoja kwaresma iishe, turudi kutrend.
 
Mh [emoji45] aisee this is bad kwa watoa comments please tuangalie maneno ya kuweka hapa, this situation is bad
Situation is bad???
Ama unamaanisha the situation is Real!!
Wanawake wa kichaga sio kabisa. Kwetu tunawaogopa kama ukoma.
Hawakawii kukung'atisha udongo
 
Pole dada, hiyo jamii hawajawa tayari kuonana na makabila yote..Nina wasiwasi ameanzia kwa mchaga , lakini likipelekwa kabila jingine itakuwa hivyo hivyo.. Halafu huyo mama ameshaanza kuingilia ndoa mapema kabla ya kufungwa.. Inamaanisha ikifungwa tu ataingilia mahusiano ya mwanae na pengine ndivyo alivyo, si rahisi kumbadilisha ... Ila wewe mwenyewe unaweza kudalika kabla na kuangalia maeneo mengine. Heri nusu shari kuliko shari kamili.... Ninavyojua wamama kama hao , nongwa yao haiishi kwake tu, ataisambaza kwa ndugu wote na atakuwa mwiba kwenye ndoa yenu miaka yote...Nani atapenda kuingia kwenye mahusiano na ndoa ya nongwa hivyo, bora umehabarishwa mapema.... Tafuta kwingine atakuja ambaye Mungu amepanga kwa ajili yako.
Nakuelewa sana.... Wawili mnapendana ... Hata hivyo inabidi kuishi kwenye familia kubwa ambayo , mama mkwe ni sehemu yake.. utaona swala lako, hata kama sio kwa ulinganifu kiasi hicho , linafanana na la Merghan na Harry - wana wafalme..Harry amempenda mkewe, familia ya kifalme wana ubaguzi.. Mwisho wa siku wameamua kuishi peke yao.. Kwa jamii ya kizungu inawezekana kwa jamii zetu za kiafrika ni mtihani sana... Bado familia zinahusika na familia zetu asilimia 100%, labda muishi nje ya nchi.. Huko mnaweza kuanza familia yenu na marafiki bila kujali sana haya ya familia.

Kwa swali jingine, je mtarajiwa wako ana msimamo gani? Kwa penzi atasimama na wewe , lakini mbele ya safari, ukimkorofisha au ikitokea chochote atakumbuka sauti ya mama yake na atakuona kama wewe sehemu ya majuto .. Ongea naye mpate msimamo....Na kama baba Mkwe yupo anaweza kumhandle mama mkwe, kama hayupo basi ni dunia yake ndogo...
 
Janamke la kichaga hayati na nusu! Hachelewi kukuua abaki na mali zote.
Hii tabia inajulikana Tanzania nzima.
 
Wazazi wangu waliniambia siyo vizuri kwenda ukweni kabla hujaolewa siyo heshima na ukiangalia ni kweli pia mchumba angu nilimuuliza akanambia ni kweli inabidi Mimi mwenyewe nitafute siku special nikupeleke kukutambulisha rasmi Ila siyo Mimi kujipeleka mwenyewe inakuwa siyo heshima
Hujui jinsi ya kuwin mama Mkwe maana miaka 7 hata hujafika umakuwani. Hapo ulijikwaa
 
Na hiyo ndiyo heshima. Sio mnadate tu unajipeleka kwa wakwe, wakishakujua?
 
Nimekuelewa dada angu kwa uliyoeleza aisee hapo kuna upendo wa ndani kabisa,fuata ushauri mzuri humu,lazima utapata uliobora na utakusaidia,usisahau kutuambia harusi wapi wana jf tuje tucheze kwaito.
 
Dah pole sana, ila mimi ni mtu wa maono naona kabisa mtaoana na maisha yatakuwa fresh tu na furaha kwaiyo acha mawazo pika chakula kizur mle na mumeo .LAZIMA MUOANE LABDA JAMAA NDIO AWE HATAKI LAKINI SIO HUYO MAMA.
KISHA MSAMEHE HUYO MAMA KAMA HAKIJATOKEA KITU
 
Inaweza ikawa vita vya kiroho..
Tushirikiane kwenye kuomba.
 
We ukiolewa prove them wrong! Kuwa hata ukiwa mchaga bado unaweza kuwa mke mwema mwenye heshima na adabu kwa wakubwa na wadogo! Pia uchoyo usiwe fungu lako ova!
Vinginevyo, tegemea taraka na tilalia lukuki!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…