miss chuga
JF-Expert Member
- Dec 25, 2019
- 303
- 660
- Thread starter
- #301
Unajua kwanini nashindwa kufanya maamuzi ni kwamba mchumba angu ananipenda sana haijawahi tokea mtu akanipenda kama huyu nawaza naweza muacha naye ataumia alafu hajanikosea chochote pia naweza pata mwanaume mwingine nikaolewa akajakunitesa nitajuta sana nitamkumbuka huyu japo naweza pia kupata Bora zaidi ya huyu Ila sasa ndo Kuna mawili hapo nahofia kuja kujuta badae huyu Kaka naye ananipenda naona kumuacha naye yupo ktk kipindi kigumu itakuwa nmemfanyia ukatili
Pole dada, hiyo jamii hawajawa tayari kuoana na makabila mengine tofauti na kabila lake..Nina wasiwasi ameanzia kwa mchaga , lakini likipelekwa kabila jingine itakuwa hivyo hivyo.. Halafu huyo mama ameshaanza kuingilia ndoa mapema kabla ya kufungwa.. Inamaanisha ikifungwa tu ataingilia mahusiano ya mwanae na pengine ndivyo alivyo, si rahisi kumbadilisha ... Ila wewe mwenyewe unaweza kubadilika kabla na kuangalia maeneo mengine. Heri nusu shari kuliko shari kamili.... Ninavyojua wamama kama hao , nongwa yao haiishi kwake tu, ataisambaza kwa ndugu wote na atakuwa mwiba kwenye ndoa yenu miaka yote...Nani atapenda kuingia kwenye mahusiano na ndoa ya nongwa hivyo, bora umehabarishwa mapema.... Tafuta kwingine atakuja ambaye Mungu amepanga kwa ajili yako.