Mama mkwe hataki niolewe na mwanaye kisa mimi ni Mchaga

Halafu utakuta watu weusi wanamlalamikia malkia wa uingereza kwamba ana ubaguzi dhidi ya Meghan wakati sisi huku ndo taabu
 
Ngoja kwaresma iishe, turudi kutrend.
Ni hivyo tyu sipendi kutrend huko miandaoni[emoji28][emoji28] ningemchukua gara b piaaa... kwanini uutese moyo wako kisa kabilaaa...


Halafu tunajuaga kuwaka balaa. Kama si mchagga basi nyaki beibe[emoji28][emoji28][emoji91][emoji91]

Kwaresma malizika tuunganishe familia.
 
Usibebe mimba kwani hicho siyo kigezo, huyo jamaa ana nia njema kwa dalili za awali shida yangu ni kwamba mama mkwe asipokupenda huwa ni ngumu Sana kukukubali hata umlambe mwisho ninyi wachaga huwa hamjui African chemistry sasa take care ukiolewa na huyu jamaa unaweza pigwa fenesi siyo kipapai ukajikuta kwenye shida.
Yaweza kuwa Mungu kakuonesha uhalisia wa upande wa pili kwamba they don't want you ingekuwa Mimi ningechunguza hatma ya kuolewa na huyo jamaa na ningetoka na jibu tena nikiwa confident.
 
Sisi wengine tuna bahati unapata mchumba unawajulisha nyumbani baba & mama wanakwambia tunakuombea mwanangu hadi mnazaa mtoto ndo wanauliza kabila gani vile mkwe wetu? Pole sana piga moyo konde
 
Kunywa soda hapo kwa mangi nitalipa kaka
 
HIYO IKO WAZI .....SIKU MOJA NILIKUWA NA MJOKE MAZA ........KWAMBA MAZA EEEEH""""NTAOA MCHAGA [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. Ile sijamalizia kauli yangu aiseeeeeh ......nilikwepa mwiko wa kusongea ugali ...[emoji28][emoji28][emoji28] ....Ata sijui kwan huku nyanda za juu kusin wachaga wanaogopwa sana
 
Maono Tena?[emoji119]
 
Kwako kimeumana ulazimishe ndoa au auchane nayo?

kwa mwanaume wako kimeumana, huku mchumba huku mwanamke?

Mama mkwe kimeumana, amekuonyesha anakupenda ila anashindwa kukubali kumtoa mtoto wake kuja kwa mchaga

Pasua kichwa[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
 
Hapo ndipo ulijimaliza! Ujanja ni kuwawin mfano kujua lugha ya kwao. Naamini hujui hata kusalimia kimakua. Angalia una bahati maana kimakua mtoto ni wa mjomba. Ukiolewa mume wako anahamia kwenu. Jiongeze ili wakupokee, ukikaa na uchaga wa kuamini wazazi wako umekwisha.
 
Mie mbona girlfriend wangu huwa naenda nae kwetu, anamsaidia na maza kuangua machungwa... Nyie washamba wa wapi aisee?? Amkeni
kujipeleka peleka kwa wazazi wa a mere boyfriend ndiyo ujanja wa wapi? Mkarudie kufundishwa heshima,
 
Jamani eeh you are asking for too much. Mtu akiwa interested kujifunza lugha ya mwenzi wake ni sawa, na sio kufanya kila kitu ili tu kuwaimpress wakwe. Anatakiwa awapende tu na sio kuwa-impress. Asije akaishia kuspend maisha yake yote kuwaimpress watu ambao wanaweza wakagoma vilevile kumpenda. Awapende tu na kuwatreat vizuri, hiyo inatosha kabisa.
 
Ila watu jamani[emoji119][emoji119]yaani akajipe na kazi ya kujifunza lugha za watu kisa ndoa?
Sindo maana mtaendelea kusema tuna ego?[emoji28][emoji23][emoji23]

Acha tuonekane viburi. Hiyo ndoa ama utopolo? Ajifunze akitaka mwenyewe. English yenyewe inatushinda. Hapo ukute hata kichagga chake hakijui ndo akahangaike na lugha za watu?

Hivi haya yotemumejoweka katika nafasi kama kala zake? Mungejisikiaje?

@miss_chagga... ndoa si utumwa. Ukishaona mambo yanakuzidia kama ub quit haraka sana. Ndoa si kupelekeshana. Khaaa..... kila mtu abaki na asili yake
 
Yaani mimi nisivyojua kuvungaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Naanza kujifunza kimakua wkati kichagga sikiwezi vizuri kisa kumfurahisha mama mkwe. Kwanza naenda kuishi nao? Mimi napenda mapenzi bana siyo lugha. Nideekeeeee... akijua kimakua ndo atakua approved ama[emoji23]
 
Mtazamie kwanza uache kumpa hiyo Nyapu yako uone msimamo wake maana ukiendelea kumwacha akanyage nyapu daily mwana anaweza kujisahau
 
Em wasituchoshe jamani. Wakwe ndiyo tuwageuze Mungu wetu sasa khaaa
 
Dah miss chuga umeongea kwa hisia sana mamie yaani mpaka umenigusa ndani ndani kabisa ya moyo,i can feel you my dear,ninaumia pamoja na wewe,kwa kweli una wakati mgumu sana mpenzi,ushauri humu ni mwing sana umetolewa,la msingi mwombe Mungu akuongoze ufanye maamuzi sahihi ambayo hayatakuwa na madhara kwenu nyote lakini pia take your time usiharakishe kuchukua maamuzi nina amini muda unaweza kutoa majibu mujarabu,time tells mamie,kila la kheri my dear na upone upesi hayo maumivu yako ya kihisia .
 
Mkuu pole sana kwa hayo yote unayopitia kwa sasa kwani ni kipindi kigumu sana kimaisha na ni Mungu tu anaweza kukuvusha salama katika kipindi hiki hivyo nakushauri pamoja na ushauri mwingi ambao watu wameutoa humu Piga Magoti mlilie Mwenyezi Mungu hakika yeye hufanya njia pasipo na njia.

Pili nakushauri usijaribu kubeba mimba kama ulivyoeleza hapo kwenye uzi ili kushinikiza ndoa hii ni hatari sana kwa muskabali mzima wa maisha yako ya kesho, pia muombe Mungu akuondolee wazo la kutaka kujiua hii ni roho chafu naomba isipate nafasi.

Tatu ongea na huyo mume mtarajiwa umjue mtu mwenye maamuzi katika familia yao kwa sasa ni nani kutokana na kwamba baba yake hayupo, ukimpata huyo mwambie mtarajiwa amfuate aongee nae na pale inapowezekana wahusishwe viongozi wa dini ili huyo mtu aende akaongee na mama na kumueleza madhara atakayoyasababisha kwa uamuzi wake wa kutokutaka ndoa ifungwe na aelezwe haya yote yanayokuumiza ikiwa ni pamoja na yeye kukubali kuja kutoa mahari na kuvalishwa pete ili hali akijua kuwa hataki mwanae akuoe.

Ikiwa namba tatu hapo juu itafanikiwa basi nakutakia kila la kheri kwenye maisha mapya utakayoanza,ikiwa haitafanikiwa mim kwa nafasi yangu nakushauri usifunge ndoa bila wazazi wa mume kuwepo nina kesi nyingi za hivi maisha yenu yatakuwa magumu sana na hutayafurahia; kumbuka huyo ndio mtu ambaye mtaishi wote kwa kipindi chote cha maisha yako kilicho baki.

Mwisho kabisa ushauri wangu kwa wakuu wote hapa wachaga kama yalivyo makabila mengine wana mazuri yao na mapungufu yao ila kwenye kutoa maoni tuwe makini na kauli zetu tunaweza kulaani vizazi vyetu bila kujua. Mama na baba wakwe mliopo hapa na wale watarajiwa tujifunze jambo hapa sio vizuri kuumiza mtoto wa mwenzio kiasi hiki "what goes around comes around".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…