Mama mkwe hataki niolewe na mwanaye kisa mimi ni Mchaga

Best hili la kukiuka matakwa ya Wazazi nani wa kumuoa au kuolewa naye wakati mwingine halileti dosari yoyote ile wanapoamua kufunga pingu za maisha kinyume na matakwa ya mzazi/wazazi.



 
Usiishi kuogopa macho ya watu watakuonaje eti hujaolewa, nakushauri kama haifai achana nayo, utajuta zaidi ukilazimisha maisha ya ndoa yatakutesa sana huku ulifanya kwa kujilazimisha
 
Nitarudi


Ili suala lako gumu

Kwanza Jamaa kakuambia, hapo tayari wee ushamchukia mkweo.


Pili, wewe ukiwambia Wazazi wako, tayari nao watamchukia mama mkwe wako


Tatu, uwaambie au usiwambie, jaama akimsikiliza mama yake ni aibu kwenu.


Daahh, embu ngoja nilale, nitoe mawazo ya kulana kimasihara, kesho nitakuja kukushauri kwa uzuri.
 
Mimi sina tatizo lolote na kinachotuchanganya mtoto wake wa kwanza kaoa mtu wa kabila lake tena majirani Ila bado mama mkwe na mawifi wanamfanyia vituko huyo dada sasa nahisi itakuwa ni tabia zao tu kuchukia wakwe na mawifi bila sababu Ila kwangu watakuwa wamechukulia kabila langu tu Kama kivuli Cha kuficha chuki zao
 
Wanaua waume zao
Jambo ambalo nimewahi kulishuhudia ni mama mmoja wa kichaga aliolewa na Dr mkuu wa hospital moja ya mission, ilikuja kugundulika anajenga nyumba Arusha bila mmewe kujua, akakodi gari ili kusafirisha furniture za ndani.....mchana kabisa ndiyo akaenda Police kureport eti kaibiwa bahati nzuri gari ilikamatwa ndiyo ukweli ukajulikana.......ni reference kubwa sana nyanda za juu
 
Isijekuwa mchumba ako kapata mchumba mwingine anayekuzidi kila eneo, kamtuma mama aweke kizuizi ili akuache nayeye aendelee na mchumba mpya...!!!
Hawa wadada wa siku hizi hata kupika hawajui.
Yaani unajikuta utaishi na mzigo maisha yako yote.
Shida zote za Nini?
 
Hapana mama ndoana tatizo na Mimi niliwaza mwanzo mama wewe Ila Kuna wakati waligombana sana kisa hili swala na Mimi nilimsikia mama mwenyewe simu ilikuwa na sauti na sahivi mtoto wake naye kachanganyikiwa haelewi afanyaje Mimi ndo inanibidi tena nimtie moyo
Isijekuwa mchumba ako kapata mchumba mwingine anayekuzidi kila eneo, kamtuma mama aweke kizuizi ili akuache nayeye aendelee na mchumba mpya...!!!
 
Ndio maana nimeomba msaada kwenu mnisaidie ili nisifanye maamuzi ya kijinga coz nmechanganyikiwa siko sawa
Umeona sasa sababu mama mkwe hataki mchaga
Ona eti unawaza ummbebee mimba kabla ya ndoa
Yaan hofu ya Mungu hauna kabisa
 
Kusema kweli mikoa ya Mbeya na iringa kwenu ukisema unaoa uchagani hakuna anayekuelewa.....sijui wachaga waliwafanya nini wazee wetu, nimeishi mikoa yote ,wazee wengi wamewasusia watoto wao Proposal za kuoa uchagani
Huwa wanatuteka tunakuwa watu wa uchagani.
Yaani unakuta wajukuu wanakujua Moshi kuliko bulongwa huko.
Haya Mambo wazazi wa mikoa hii yanawauma Sana.
Hili liko wazi na linafahamika
 
Acha tu ni aibu najiuliza kwanini aliacha mahari ipelekwe ingekuwa haijapelekwa pengne ningepata ujasiri wa kumuacha Ila wazazi wangu ni watu wa heshima sana hili swala litawachanganya sana pia itakuwa aibu ambayo haijawahi tokea kwetu ndomana nachanganyikiwa
 
Wamama mkwe sielewagi wana matatizo gani na wakwe zao Yani Karibu wote wanafanana tabia..

Chamsingi Mkifanikiwa kuoana Ni vema mkaishi mazingira tofauti na nyumbani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…