Miss Chuga mdogo angu;
1. Ni wanaume wachache sana ambao wanaweza wakaamua kwenda kinyume na wazazi wao, especially mama zao. Wanawake tukipenda huwa tunaforce kivyovyote huko nyumbani hadi mchumba atakubaliwa, wakibisha sana tunabeba mimba au tunahamia kwa mwanaume bila ndoa, maisha yanasonga. Ila hawa wenzetu, atakaloliamua mama mkwe mara nyingi ndiyo linakuwa final say. Usijiaminishe sana kwamba mchumba wako ana msimamo sana na hautobadilika. Nina rafiki angu Mmachame yalimkuta kama yako, mwisho wa siku mchumba akamwambia mimi siwezi kuendelea na mipango ya ndoa bila wazazi wangu. Ila Mungu sio wakwe, alikuja akaolewa zake na mtu mwingine na yupo anadunda na ndoa yake. (Hopefully wa kwako atapambana hadi mwisho)
2. Kamwe usije ukaungana na mtoto wa mama mkwe kwenda kinyume na mama mkwe; huo utakuwa ni ugomvi wa maisha, na ikiwezekana ugomvi utaendelea hadi kwa watoto wako (ya Hamissa na Mama Diamond). Yes kuna muda wazazi wanazingua, but still tunahitaji baraka zao, hata kama watazitoa kinafki na kuja kujumuika nanyi kwenye sherehe yenu. Usikubali kufunga ndoa na huyo mchumba wako kama wazazi wake hawajaridhia. Yeye anachotakiwa kufanya ni kuwalainisha na kuwaelewesha huko nyumbani kwao hadi waje wakubali. Usishindane na mama mkwe; kesho watapatana na kijana wake ila wewe ndiyo utabaki kuwa adui yake.
Naweza kukuelewa unajisikiaje, aibu unayoiwazia, kuchekwa na kuchambwa na wananzengo, bado muda wako na upendo ulioinvest kwenye hayo mahusiano, labda unaona na umri umeshaenda aisee inaumiza sana. Lakini pamoja na yote hayo, ikitokea imeshindikana kufunga hiyo ndoa; lia mshukuru Mungu kwa yote. Na usije ukakaa unajilaumu sijui ukaharibu maisha yako kisa umeachwa; hujafanya kosa lolote la kukufanya uachike: wewe kuzaliwa mchaga sio kosa wala sio dhambi na huwezi kubadili kabila lako ili kuwaridhisha wakwe. Kuvunjika kwa uchumba sio mwisho wa maisha
Imagine ukiforce hiyo ndoa, utaishi maisha ya aina gani na wakwe zako? Usije ukajidanganya kwamba labda mtaishi mbali na wakwe zako so ni sawa tu; mdogo angu hao ndugu mtawahitaji tu, na watoto wako watawahitaji hao ndugu wa baba zao pia.
Na usijidanganye kubeba mimba, kwa sababu unaweza kubaki single mom, ndoa isifungwe na hata huyo mtoto wako wasiwe na habari naye. Acha mambo yaende naturally, muache mchumba wako apambane hadi kieleweke. Ikishindikana basi mama, wewe sio wa kwanza wala wa mwisho kuvunja uchumba, na wakati mwingine ni bora kuvunja uchumba kuliko kuvunja ndoa. Familia nyingine unaenda kujipa mateso tu.
Muombe Mungu, mapenzi yake yatimizwe kwenye huo uchumba wenu. Litakalotokea lolote, kubaliana nalo then mshukuru Mungu. Yeye anakuwazia mema siku zote, na anaijua kesho yako.
Na nyie wanaume muulizage mapema kwa mama zenu, wawaambie hawataki muoe kabila gani: sio unakaa na mtoto wa mtu miaka 5 afu ndiyo mama mkwe anakuja "sitaki mchaga sijui mnani". Afu alivyokosa huruma eti aliruhusu kabisa utolewe mahari. Mungu amsamehe, hiyo mbegu isije ikamea kwa mabinti zake.
Ukiona linakuchanganya sana, washirikishe ndugu zako. Usije ukadondoka kwa presha bure. Mungu na akutetee