Mama mkwe na mwana wote wanapiga mbonji kwangu

Tatizo ni nyumba ndogo?au uchoyo umekujaa hujui mama wa mkeo ni kama mama yako mzazi
 
Aliyetakiwa kusaidia ulezi ni your mom na siyo mama mkwe....
 
Kuoa halafu ukae na ndugu its very challenging... regardless ni ndugu wa upande gani...
 
Mkuu umenichekesha sana, umewaza nini??? Eti wakuigize unavyotembea na kuongea, yaliwahi kukukuta?
 
ni kweli mkuu,maana hapo unaweza ukapshana kauli kidogo tu na mkeo tayari mama ake anaingilia!au hata mama yako mzazi asipoelewana na wife unakua na mtihani wa ku pick sides...

Na hapo mleta mada kagusia na imani za kishirikina huyo mama hashindwi kumpa dawa binti yake ili "kum- restrain " jamaa!!
Kuoa halafu ukae na ndugu its very challenging... regardless ni ndugu wa upande gani...
 
Back in days,tumemuigiza sana mshua anavoongea na kutembea,tena na bibi na mama wakiwepo....i fel u bro[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hahah. Mbona kama umeongea kwa experiance?
 
Wewe jamaa [emoji1787]
Yaani kidogo nipaliwe na supu ya utumbo hapa. Eti kijeba
 
Kuna watu wanasema vip angeku ndugu zake.
Mimi umri utakapo kuwa mkubwa siwazi wala sitegemei kuishi kwa wanangu labda maradhi ya uzee na niwe sina wa kuniangalia...

Nina mdogo wangu alikuja (niko single ).Naona mtu haondoki.Nikamtaftia kazi chap.Naona mwezi wa tatu bado haondoki.Sitakagi ujinga nikatafta chumba nikalipa kodi nikanunua na kigodoro cha futi 3 na nusu,pazia mbili,ndoo moja ya maj na shuka.

Asubuh moja nikampeleka.Sasa hivi ana mafanikio kunizidi.Ndugu mwisho kukaa kwangu ni week
 
si utaulizwa unawaachaje achaje... dawa wanunulie unga kilo 10 dagaa kilo moja na maharage kilo 3 , Tokomea wiki 2-3 hivi
Nayeye mwanaume anatakiwa arudi kwao hakae kama wiki tatu tena aondoke na mtoto wake mdogo
 
Hivi unajua wengine hazimo, ndio kwanza watagonga mlango sabuni ya kuoga imeisha wanaomba hela wakanunue, [emoji3][emoji3][emoji3] kama namuona vile anatoka na taulo kumpa shemeji hela ya sabuni
 
Safi sana, haya ya kusema namuogopa bikubwa yanaumiza Bora hukumkosea adabu, mkilelewa kwenye ukweli na uwazi haya mbona madogo tu
 

Mama mkwe wako katika umri huo uliousema, moja kwa moja anaqualify kuwa ni dependant wa wanawe, mkeo akiwa mmoja wa anaopaswa awategemee kwa asilimia 100. Na kama mama mkwe wako anamtegemea mkeo, automatically anakutegemea wewe. Issue ya kwamba yuko mahali anakaa sehemu na kujitegemea mwenyewe, mlitakiwa mumshukuru Mungu, anawapa ahueni ambayo ni priviledge kwenu wewe na mkeo, siyo right yenu. Kwa hiyo inapofikia wakati wa previledge kuisha, usifanye makosa hayo ya kuanza kuidai kama right. Swala la mama mkwe kuja kwako kwa minajili ya kumsaidia mwanawe kulea mtoto halafu baadaye akabadilisha mawazo na kuamua kukaa moja kwa moja, hakumuondolei haki yake ya msingi ya kuishi kwenu na kuendelea kuwa dependant wenu, kisa tu siku anakuja alisema kuwa angerudi kwake lakni ameamua kutokurudi. Kama itatokea kwa BAHAT MBAYA akarudi tena kwake, hiyo itakuwa previledge kwenu, lakini kama ataamua kubaki, basi anaamua kutumia haki yake ya msingi ambayo si yeye tu anaistahili, bali wazazi wote wenye sifa kama zake.

Kuhusu huyo sehemeji yako,mpe muda kidogo, najua hatimaye atarudi kwao. Tumia hekima zaidi namna ya kuishi naye, kwa sababu hajamaliza hata mwezi. Tuseme kwa mfano angekuja kwako na kukuambia kuwa anapenda akae nyumbani kwako mwezi mzima, ungemkatalia? Sasa nashauri uchukulie kama ni mgeni ambaye amekuja kwako na atakaa mwezi mzima au hata miwili.

Mwisho unanipa wasiwasi kidogo kwamba pengine wewe una kiwango fulani cha uchoyo ambacho binadamu walio wengi hawana, uchoto unaoweza ukapelekea hata ukafukuza mgeni nyumbani kwako bila kuwa amefanya kosa lolote la msingi ila kisa tu amekaa kwako sana kwa muda ambao wewe hukuutarajia. Usije hata siku moja KATIKA MAISHA YAKO YOTE, ukafanya hivyo, NI AMRI SIYO OMBI. Mwanaume tumia ubongo wwako umepewa bure na Mungu wala hujaulipia gharma yoyote!
 
Hivi unajua wengine hazimo, ndio kwanza watagonga mlango sabuni ya kuoga imeisha wanaomba hela wakanunue, [emoji3][emoji3][emoji3] kama namuona vile anatoka na taulo kumpa shemeji hela ya sabuni
Kadiri anavyogonga mlango na wewe unasukuma zaidi, mbeleni huko mtaelewana tu. Kwani unafikiri aibu lazima waone wao, hata wife akiona aibu atatafuta namna ya kuwaelimisha waache runway wazi
 
Nasubiri uzi wa siku nduguzo wakija na kupiga kambi...

Baada ya hapo ndio nitakomenti kuhusu uzi huu
 
Kiongozi naomba tufahamiane tunaweza kuwa mashemeji maana nimependa msivyoshobokea kujazana kwa mashemeji!
 
Safi sana, haya ya kusema namuogopa bikubwa yanaumiza Bora hukumkosea adabu, mkilelewa kwenye ukweli na uwazi haya mbona madogo tu
Kuna njia ya kuongea nae yaani kwa nidhamu. Sasa bro yeye sijui huwa anakwama wapi? Yaani atakaa nalo moyoni lakini hawezi kumwambia
 
Wasikufilisi hao. Ukitoka muachie mkeo pesa ndogo ya kutosha ugali na mboga za majani tu. Ndugu ukiwalisha vuzuri na kuwawekea kifurushi cha azam hawatoki hapo kwako wataona wamefika. Omba likizo shinda nyumbani useme umefukuzwa kazi. Anza kumuomba shemejio akutoe pesa kidogo mle hapo nyumbani uone kama hatoaga mwenyewe
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Wewe jamaa nimependa ushauri wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…