Mama mkwe na mwana wote wanapiga mbonji kwangu

Mama mkwe na mwana wote wanapiga mbonji kwangu

Ninapofanya mambo ya faraga na mke wangu kaka mtu anasikia, ni uungwana??
 
Shida za kuoa Kilimanjaro halafu wewe uaishi pale moshi mjini,nauli mtu haizidi hata 5000

Mtu anaoa Dar halafu anaenda kuishi mbezi beach oooh hooo kila sku ndugu hawakauki tena

watakuja kila week end kukusalimieni tu,Dawa ya Ndoa Unaoa Dar unaenda ishi Kigoma huko

Unaoa Bukoba unaleta kambi Dar,yani mtu akifikiria kuja kwanza lazima apige simu kutoa taarifa

sio mambo ya kuoa Sakina halfu unaenda kuishi ngaramtoni huo ndo uzwazwa maji...
 
mr.London, Pole sana brother.
Hii ni moja ya changamoto za ndani ya ndoa.

Wavumilie tu. Usije ukafanya maamuzi yatakayotowesha amani ndani ya familia zenu.
 
Chukua likizo ya ghafla uondoke ww mke na watoto wako 2. Wataondoka wenyewe
 
Tulifundishwa kuhusu siasa za Ujamaa na Kujitegemea. Ila sisi waswahili tulichoweka kichwani mwetu ni ujamaa tu, habari za kujitegemea hatupendi kuzisikia, na hili ni tatizo kubwa sana kwenye jamii yetu. Unakuta jitu zima miaka 30+ bado anaishi kwa kaka, shemeji , shangazi nk. Nawapa pongezi wachanga wote, ujinga huu hauna nafasi, nami nimewaiga, ndugu 18+ years kama si mwanafunzi au mgonjwa, kwangu hana nafasi. Huo ni misimamo wangu hata kwa watoto wangu wa kuzaa nao wanaijua hilo. Wasinimalizie hali ya kujikimu kwangu na wote kipindi cha uzeeni. Mwenye mawazo tofauti sawa, ila mimi huo ndiyo msimamo wangu na sitanii
 
mr.London,
Huyo ma’mkwe na mwae lao 1 tu. Jitie unafiki wa kutomwambia ukweli huku unaumia mwambie achague yeye/binti’ye yupi abaki!
 
Kama Una shamba wakurupushe kila weekend alfajiri shambani.Hakikisha kila siku kuna sala usiku kabla ya kulala tena ndefu.Weka Sheria kurudi mwisho saa 12 jioni.Mtu akila lazima aoshe vyombo vyake.Wataondoka wenyewe.
Ahahahahaha umetisha mzee baba, hizi vinaitwa vikwazo vya mabeberu
 
Tulifundishwa kuhusu siasa za Ujamaa na Kujitegemea. Ila sisi waswahili tulichoweka kichwani mwetu ni ujamaa tu, habari za kujitegemea hatupendi kuzisikia, na hili ni tatizo kubwa sana kwenye jamii yetu. Unakuta jitu zima miaka 30+ bado anaishi kwa kaka, shemeji , shangazi nk. Nawapa pongezi wachanga wote, ujinga huu hauna nafasi, nami nimewaiga, ndugu 18+ years kama si mwanafunzi au mgonjwa, kwangu hana nafasi. Huo ni misimamo wangu hata kwa watoto wangu wa kuzaa nao wanaijua hilo. Wasinimalizie hali ya kujikimu kwangu na wote kipindi cha uzeeni. Mwenye mawazo tofauti sawa, ila mimi huo ndiyo msimamo wangu na sitanii
Umekosha sana ubarikiwe.ubaya ubaya tu(mambo ya extended family haya hovyosan
 
Watu wa ukumbi huu, habari zenu.

Nimeoa na sasa nina watoto 2 alhamdullah, nampenda sana mke wangu lakini kuna jambo hili linaendelea kila uchao nahisi moyoni nimeanza kulichukia chukia.

Kuna muda mamamkwe amekuja kumsaidia ulezi wife wakati wa kujifungua lakini akapitiliza ule muda nilioambiwa na wife kama angekaa, sasa akawa anakaa kama ndio mahali pa kuishi. Yeye ni age kidogo, mama mtu mzima, hana mume.

Kuna kipindi huyu mama anaumwaumwa, mara ikaja ni kuhusu haya mambo yaliyoingia; sijui kapewa jini, mara shetani tafrani nyumbani mpaka sasa amesafirishwa mji wa pili kwa matibabu zaidi lakini nahisi akimaliza matibabu kama aturidi hapa kwangu.

Suala lingine naona shemeji yangu mtoto wa kiume shababi naye amekuja. Siku hiyo wife akaniambia leo shemeji yako, yaani mdogo wake, atalala hapa nikasema safi nikamtolea kitanda na godoro ili achape usingizi kwa siku ile, lakini naona siku ya pili kaendelea mpaka imefika kama wiki akasafiri kidogo kaenda kukaa kama siku 4 karudi yupo tunaendelea naye anachapa usingizi kama kawaida.

Nilijaribu kumuuliza wife ananimbia anafuatilia kitambulisho cha Taifa. Sasa mimi najiuliza, ivi unaweza kuacha shughuli zako siku zote kwa kitambulisho tu? Kuna siku akasema ile namba tayari ashapewa lakini mzee yupo ameganda tu na sasa pale home majukukumu yanaongezeka.

Naomba fatwa watu wa hapa, vipi niendelee kuvumilia maana hata uhuru pale nyumbani naona umebanwa kidogo.
Ukienda boga penda na ua lake mzeee hii dunia tu kwani wanakula kilo ngapi
 
Kama Una shamba wakurupushe kila weekend alfajiri shambani.Hakikisha kila siku kuna sala usiku kabla ya kulala tena ndefu.Weka Sheria kurudi mwisho saa 12 jioni.Mtu akila lazima aoshe vyombo vyake.Wataondoka wenyewe.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Nimekuja gundua jamii forum kuna watu wana zile tabia za uswahili ambazo siwezi hata kidogo. Yaani kuna raia wanakomaa kukwambia eti ukae na hao wageni, mimi hata kwa aunt zangu naenda tu madogo wakirudi likizo wakiniitaji na kuniita. Nikienda ni masaa machache tu. Hizi tabia za kutegeshea dada zenu waolewe ndo mkavae bukta za shemeji zenu ni ujinga mtupu. Pambana
 
Back
Top Bottom