Mama Mongella - Aghushi na Kutafuna Mamillioni Ya Pesa!

Alishayazoea ya CCM, Viongozi wengi wa CCM ni wachafu sio watakatifu hata kidogo hivyo kuwa hivi wala tusishangae kabisa maana ufisadi kila sehemu labda wa kijibu ni Spika na, Mafisadi wapo watu wengi wa kila namna, Kuanzia Tanzania mpaka Bunge la Africa
 

........yaani kusurvive kwa huyu mama........miye nilikuwa napigia mstari tu ule usemi wa Nyani Ngabu............this thing came too late......and clearly its a bad image to our nation............
 
Kumbe acha Karamage amfaidi mke wa Mongella. Mongela na Karamage ni Dugu moja. Wanabebana Kifisadi na wanasaidiana kifisadi.

Hivi huyu mama si ndiyo inasemekana alipotoka Beijing yeye na kundi lake walikuwa wamejaza kwenye vijaluba semCondoms??!!!
 
Ila ni aibu kubwa sana kwa Tanzania jamani kama hayo yaliyosemwa ni ukweli.
 
MMh kama hizo tuhuma ni kweli atakuwa ametuangusha sana,na nchi yetu kwa ujumla kweli fedha fedheha
haya mambo ni ya kweli kabisa na nilikuwa south africa wakati yanatokea na it was higherly covered negatively in her regard. nimemwona anajitetea kwenye vyombo vya habari watu wanamchafulia jina....hana pa kutokea
 

Hii ishu kama ulivyosema mkuu ni ya siku nyingi sana hadi ilishasahaulika hadi ilivyoibuka tena juzi juzi na wabunge wa Bunge la Afrika kuishikia bango hadi kieleweke.
Ninachojiuliza:
1. Hivi Tanzania kuamua kulipa/kufidia upotevu huo inatafsirika vipi? Does it mean kuwa serikali inawajibika kwa makosa ya huyu mama?

2. The fact kwamba kalazimika kuwajibika, uwajibikaji huo wa kuachia ngazi tu hautoshi. Hata kama alipata nafasi hiyo kwa jitihada binafsi bado alikuwa na dhamana na hivyo anapaswa kuwajibishwa zaidi baada ya kuliingizia serikali hasara.

Sitaki kuamini hiki ndicho kilichotokea maana I have lot of respect for this Lady.
GOD FORBID!
 
........yaani kusurvive kwa huyu mama........miye nilikuwa napigia mstari tu ule usemi wa Nyani Ngabu............this thing came too late......and clearly its a bad image to our nation............

Heheheheheheheee....

Limama hili lina sura mbaya inayoendana na tabia yake ya ufisadi.
 
naona wengine hamna uhakika kama hili ni kweli...kwa taarifa ni kweli na huyu mama amejizalilisha sana na pia kuiletea aibu nchi yake, wakati wa bunge la PAP habari zake ziliandikwa sana kwenye magazeti ya south na kuna watu walishangaa sana kule kama kweli huyu mama anaweza kufanya vile...ni aibu na sijui kwa nini anakuwa mbishi maana alikuwa hataki hata kuwajibika..

lakini pia serikali kuingilia kati na kutaka kulipa hasara aliyosababisha ni unacceptable..why?? je serikali imeridhia kama aliyoyafanya si sahihi?
kama serikali imeona si sahihi, anachukuliwa hatua gani???
na je mpaka sasa serikali ya TZ imefanya uchunguzi gani, na taarifa imetolewa wapi??? intakuwa inafanya kosa kubwa sana....
 
Kama Slaa anavyo taka kulivalia hili suala serikali inabidi kumkata kwenye mafao yake na ikibidi kuuza Mali zake , na adhabu zingine zinazo stahili.
 


WoS na mimi naungana na wewe hapa.

Kuhusu TZ kulipa hizi pesa haiwajibiki. LAKINI nadhani Membe na JK waliamua kufanya hivi kama damage control dhidi ya taifa letu. Maana report ya auditors ilikuwa so scathing against matumizi mabaya ya pesa na madaraka ya huyu mama. Na ukichukulia hizi ni nafasi za ku-lobby..kama issue inge escalate mama akafukuzwa at the level kama Accra na wakuu wa nchi za Africa..Tanzania ingekuwa in the hole..next time tukitaka kupendekeza wagombea kwenye nafasi kubwa kama hizi. So basically it was a diplomatic game kulipa hizi pesa.

Labda cha kujiuliza..will this issue be swept under the carpet? huyu mama atawajibishwa kwa namna yoyote ile? Kwa kuijua nchi yangu ilivyo..hii imetoka..na hata kama juzi uliangalia Press conference ya huyu mama wakati anakuja..alisema"she has done proud all Africa women"..well you can see..matapeli tunawapokea kwa ushujaa.

What Iam sure of, huyu mama kazi hii ameondolewa kwa nguvu. Na South Africa na nchi nyingine hii issue ilikuwa well covered-only in Bongo!
 
Kumbe acha Karamage amfaidi mke wa Mongella. Mongela na Karamage ni Dugu moja. Wanabebana Kifisadi na wanasaidiana kifisadi.

Hivi huyu mama si ndiyo inasemekana alipotoka Beijing yeye na kundi lake walikuwa wamejaza kwenye vijaluba semCondoms??!!!
Mkulu naomba ufafanue kidogo.
 
hiyo yote haisaiidii labda hao PAP wamchukulie shelia wenyewe lakini sisi kama watanzania hatuwezi kufanya chochote juu yake, tutabaki kuumia tu.

nadhani itakuwa ngumu hawa PAP kuchukua hatua nyingine zaidi ya kumfukuza[kumlazimisha ajiuzulu]wao wanauhakika chao kitarudi,si serikali yetu italipa kwa mapene yetu walipa kodi?kazi kwetu sisi wavuja jasho wa nchi hii
KWELI NCHI HII INAJENGWA NA WENYE MOYO NA KULIWA NA WENYE CHOYO
 
mimi ningependa kujua kama hizo hela za "damage control" zimetoka mifuko binafsi na sio za kwetu walala hoi, Jk na Membe naomba watueleze zimetoka wapi hizo hela? kama ni damage control basi wangetoa na kumlazimisha azirudishe kama walivyomfanyia yule mbunge wa zamani alitumia pesa zetu kumpeleka mkewe matibabu nje.
 
Tatizo langu lipo kwenye maeneo mawili:

1.Je ni kiasi gani cha Fedha Serikali yetu imeahidi kulipa kutokana na mismanagement ya Dkt. Mongella?

2.Kuanguka kwa huyu mama ni KUANGUKA KWA "KIPIMO" ambacho Watanzania hususani akina mama wenye matarajio ya kufanikiwa kisiasa WALIKUWA WANAKITUMIA "KIPIMO" HICHO(yaani Dkt Mongella) kijipima walipofikia.
 
Mwalimu akifufuka leo akazisikia habari hizi.....Huyu mama alikuwa ni mmoja wa watu walooaminiwa sana na Mwalimu.
Yes.
Na hicho ndicho kilichonisukuma kuuliza swali la msingi,NINI KIMESIBU HUYU MAMA????????!!!!!!
 


Kama itakuwa ni kweli mama Mongella amefanyika haya, itakuwa ni aibu kubwa sana kwa nchi yetu ya TANZANIA (Kisiwa cha AMANI)

Ni ufisadi uliovuka mipaka kwa kweli. Jina la Tanzania linaanza kusifika kwa mambo mabaya sasa...... MIMI BINAFSI NILIKUWA NAMCHUKULIA HUYU MAMA KAMA MFANO WA KUIGWA KWA MAMA ZETU KATIKA FANI HII YA UONGOZI. Naamini atakuwa hata pia amewavunja moyo wanawake wenzake katika hili.....

Kelele za EPA ya ndani ya nchi zimedhibitiwa, na sasa ...."Hiyo ni international EPA".

MAMA MONGELA UMETUTIA AIBU KWA KWELI SISI KAMA WATANZANIA...
 
Kama kuna mfuko wa "damage control" basi akina Jeetu Patel, Chenge, Liyumba, Yona, Mramba na watuhumiwa wote nao walipiwe hasara waliyoisababishia serikali. Kwa nini ni Mongella tu ndiyo analipiwa ?? Naona serikali yetu labda ina makundi ya mafisadi wazuri na mafisadi wabaya, mafisadi wazuri wanalipiwa hasara zote walizosababisha.

Sijui ni nani anaamua huyu alipiwe na huyu asilipiwe. Pia wale wote walio jela kwa kuiba benki, kuku, nguo, magari, nao serikali iwalipie watoke jela!!!! Kaazi kweli.....
 

Mzee mzima

Bila shaka hela iliyolipwa huko PAP itakuwa ni jasho letu. JK na Membe wamlipie Mongela damage control kwa fedha za mifukoni mwao kwa kuogopa kitu gani?si wanajua tu fungu lipo la kodi za wadanganyika zitachotwa na kulipia madeni ya kishenzi kama hilo la mongela.

Na hapo ndio ujue kwamba sasahivi Tanzania uadilifu kwa viongozi ni sifuri. Wamezoea kula pesa zetu na kisha kutupigisha siasa za maji taka lakini safari hii mongela kakutana na wajanja wamemnasa.Kazi iliyobaki ni moja tu; kwa wana ukerewe wamuwajibishe huyu mama pamoja na kulitia aibu taifa lakini pia amewaaibisha sana wana ukerewe ambao ni watu waadilifu na wachapa kazi.
 
MMh kama hizo tuhuma ni kweli atakuwa ametuangusha sana,na nchi yetu kwa ujumla kweli fedha fedheha
KAMA NI KWELI

Kabla ya kufikiria kuniangusha cha kwanza naongelea kuhusu hela ambazo serikali imejicommit kuzilipa,

  • je zinatoka fungu gani la bajeti
  • na kama serikali imekubakli kubeba mzigo basi inamaana matumizi yake yalikuwa halali kama haikuwa halali kwann wakubali kulia kwamaana nyingine serikali yetu ni ya wezi
  • kama ikiwa fedha zimetumika isivyo halali basi huyu mama hatakiwi kunyamaziwa apelekwe mahakamani maramoja kujibu tuhuma maana ni kilekile alicofanya Mahalu hapa
Mwisho kabisa huyu mama ameonyesha mbegu ya ccm, kama kawaida yao hawajui maisha mengine zaidi ya wizi, amevunja heshima yake na yanchi alishindwa nn kusubiri muda mfupi uliobaki wauonguzi wake anondoke kwa sifa na mfano mzuri

WHAT A SHAME!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…