MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,565
- 843
Ni mama yangu wa ubatizo,hence in my eyes she can do no WRONG.
Ni mama yangu wa ubatizo,hence in my eyes she can do no WRONG.
Folks hii habari imejulikana kitambo sana. Ambao hawafuatilii mambo ndo wanashangaa. Ukweli ni kwamba hii kashfa ya huyu mama ni ya siku nyingi..infact JK na Membe walijaribu kulimaliza kikubwa na wakubwa wenzao kwenye mkutano wa wakubwa wa Africa lakini pressure ilikuwa kubwa sana. Ndo maana TZ ilikubali kulipa gharama za upotevu wa pesa. Ilibidi huyu mama afukuzwe kwenye kikao cha AU kule Accra juzi juzi..lakini nadhani JK alitumia diplomasia kuogopa damage kwa nchi yetu.
In all, this is not new. FMES na wengine kibao humu nadhani waliweka details nyingi humu JF na tuhuma zake kuchambuliwa. na huu wizi uliripotiwa na international auditors..nadhani KPMG au Coopers kama sikosei.
Ni kama leo tukisikia Tibaijuka ameondolewa..wengine hatutashangaa maana dossier ipo siku kibao kuonyesha jinsi mama alivyovuruga..
Let her go..its a disgrace..Sema tuu wanaharibia wengine wenye moyo wa kuhangaika na kusonga mbele banking on diplomatic image of our country.
Ataadhibiwa na nani? Wote mbona watanyoosheana vidole? Ndiyo bongo yetu ya leo, nasikitika kusema. It is very sad indeed.We need to be honesty with ourselves. Tunajitia aibu nyumbani na sasa tumetia aibu nje. Kama akitokea mtu akianza ku-question ni kwanini watanzania hawapati nafasi kwenye jumuiya za kimataifa nitashangaa sana. Ajabu sana nitashangaa kama akija nyumbani hajachukuliwa hatua, kama serikali imetumia pesa kwa kulinda heshima yetu, na sijui kama kweli imelindwa, huyu mama akirudi anatakiwa aadhibiwe. She is such a disgrace. Jamani nchi yetu inanuka ufisadi, na watanzania sasa tumeanza kunuka ufisadi. Aibu tupu.
Kweli
Ukistaajabu ya Musa....................., Mwalimu Nyerere huko aliko naona anasikitika sana.
Mungu Tusaidie kwani hatujui tutendalo
Ingawa aliowapendelea ni watz, lakini ni ndugu na jamaa zakekama ni upendeleo wa ajira sijafahamu aliwapendelea wa wabongo ama vipi. Kama ni watanzania basi kudos to her.
Kama ni za kweli..ni aibu, tena si ndogo. Jamani mwenye habari za ndani za huyu mama aziaanike hapa, maana tunaweza jua ni kwanini kafanya hivyo. Au ndo kaanza tu na kudakwa..mmh lakini hizi ni za mwizi ni arobaini. JF intelligence we need more data about this beijing icon.
CCM Chama Cha Makomunisti.Unaona hilo jembe na nyundo vilivyokuwa positioned? Wameondoa sickle wakaweka jembe.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi
Mh,...halafu alikuwa anautaka urais wa nchi!
Sasa pale Ikulu sijui ndio ingekuwaje kama angeupata,i'm sure yule mtoto wake ambaye ni DC Kigoma huko labda angempa ubosi wa PCB!
Jamani,hao ndio viongozi wetu...always drooling where there's $$$
Mwenyewe Agoma Kuzungumza!
Rais wa Bunge la Afrika, Mama Getrude Mongella, anatuhumiwa kutenda makosa ya kukosa uaminifu, Wizi na utoaji ajira kinyume na taratibu za kazi yake:-
1. WIZI:- anatuhumiwa kutafuna Dola za US, 138,000 ambazo ni sawa na shillingi 180Millioni za Tanzania.
2. UAJIRI:- anatuhumiwa kuajiri ndugu zake kinyume na sheria za kazi yake, akiwemo mkwe wake, yaani mke wa mtoto wake.
Katika kikao cha AU kilichopita nchini Ghana, nchi za Afrika zilimuamuru mama huyo kurudisha hela hizo mara moja huku uchunguzi ukiwa unaendelea, kikao hicho pia kilihudhuriwa na Rais Kikwete.
Mama Mongella, anatuhumiwa kujilipa US/Dola 800, kwa siku akilifanyia kazi bunge hilo la Afrika, na huku akiwalipa US/Dola 400 kwa siku ndugu zake aliowaajiri huko AU, wakati pia akilipwa na bunge la Tanzania kwa kazi hiyo hiyo. Mkwe wake mama huyu tayari ameshaachishwa kazi na bunge hilo na wengine wako njiani kurudishwa tayari Tanzania.
Katibu wa Bunge la Tanzania, ndugu Foka, alithibitisha kupata habari hizo za tuhuma dhidi ya Mama Mongella, na amekiri kwamba ni kweli Bunge letu la Tanzania limekuwa likimlipa mama huyo fedha zote anazostahili akiwa analifanyia kazi bunge la Afrika, kwa mujibu wa makubaliano na bunge hilo la Afrika, ambalo liliwaomba mwanzoni wakati anaanza kuwa liwe linamlipa ili asilipwe na bunge hilo la AU.
Taarifa za uchunguzi tayari zimefanyika na SADC, ikishirikiana na kampuni ya KP GM ya Kenya, ambazo izmeshauri mama huyo kufukuzwa kazi na kurudisha mapesa hayo kwa AU, mara moja. Mbunge mmoja wa bunge hilo la AU, Ndugu Wanyancha,(Serengeti-CCM) amekubali kuwa kweli Mama anakabiliwa nashutuma nzito sana ambazo zitatukosesha urais huo kwa muda mrefu sana ujao, juhudi zote za kuzungumza naye kuhusu hiii sualazimakwama kutokana na kukataa kwake, mama huyo.
Source: Mwana-Halisi.