Mama Mongella - Aghushi na Kutafuna Mamillioni Ya Pesa!

Mama Mongella - Aghushi na Kutafuna Mamillioni Ya Pesa!

Mwalimu akifufuka leo akazisikia habari hizi.....Huyu mama alikuwa ni mmoja wa watu walooaminiwa sana na Mwalimu.

Mwalimu angekuwa hai , mama huyu ndio lilikuwa chaguo lake kuwa Rais kipindi cha pili cha BWM [2000-20005]!!! Sijui angetuletea aibu gani Yarabi!! It seems Mwalimu was cheated many times by personal appearances!
 
Loh! ni aibu kweli kweli kwa Kiongozi aliyetegemewa kuongoza ukombozi wa mwanamke Afrika na Dunia nzima. Kashfa ya wizi haiwezi kutetewa na mtu yeyote, ni vyema apelekwe mahakamani.Aibu aliyoitia nchi yetu ni sawa na kinyesi kwenye uso wa mtu muungwana.
Mama Mongella umetia aibu na umelitia aibu Taifa.
Zile tetesi za miaka mingi za kuwa alirudi na condom kwenye mkoba akitoka Beijing zinaweza kujirudia.Kuna msemo usemao kuwa mwanamke apendaye pesa kupindukia lazima anakatabia kasikopendeza kanakoendana na tamaa hiyo.
 
Last edited:
Wanaoshangaa ngoja washangae - Ufisadi na CCM ni pete na kidole. Ufisadi ndio mtaji pekee wa CCM na yeyote anayekataa hilo ujue ni fisadi vile vile. Narudia kama nisemavyo siku zote - huwezi kuishi kwenye tope usiwe mchafu, huwezi kuishi kwenye uvundo usinuke na huwezi kupanda maharage ukavuna machungwa - it is that simple. CCM walishaonja nyama ya Watanzania, kamwe hawataacha.

Mnaouliza hizo hela zimetoka wapi na kwenye fungu gani nawaambia zimetoka hazina na ni kodi zetu. Mnaouliza wamepata wapi ruhusa ya kufanya hivyo nawajibu kuwa tumewapa sisi na si ajabu mwaka 2010 tukawapa tena. Yanikumbusha ile mizimu inayonyonya watu damu, unakuta mtu anajipeleka mwenyewe kunyonywa damu yake. Ndipo hivyo tulivyo Watanzania na ukweli ndio huo.
Tutanyonywa hadi tuzimie
Labda tuombee the Obama effect mwakani - naona hata Iran imetua.
 
Ila ni aibu kubwa sana kwa Tanzania jamani kama hayo yaliyosemwa ni ukweli.

Hakuna cha aibu kwa Tanzania bali ni aibu yake mwenyewe. Besides huyu kaiba huko siyo nchini na kama ni upendeleo wa ajira sijafahamu aliwapendelea wa wabongo ama vipi. Kama ni watanzania basi kudos to her. Hili la aibu siliamini maana kama ni aibu ingekuwa kwa Ghana kwa yale aliyofanya mtoto wa Kofi Annan tena UN nini AU lakini wapi Ghana wanapeta tu.
 
Hakuna cha aibu kwa Tanzania bali ni aibu yake mwenyewe. Besides huyu kaiba huko siyo nchini na kama ni upendeleo wa ajira sijafahamu aliwapendelea wa wabongo ama vipi. Kama ni watanzania basi kudos to her. Hili la aibu siliamini maana kama ni aibu ingekuwa kwa Ghana kwa yale aliyofanya mtoto wa Kofi Annan tena UN nini AU lakini wapi Ghana wanapeta tu.

Ndugu yangu heshima kitu cha bure, na hakigharimu kitu kuheshimika .Lakini kukosa heshima kwa tuhuma za wizi, hasa kwa mwanasiasa wa caliber ya huyu mama Mongella ni aibu, AIBU TUPU.

Kwa Tanzania ni aibu zaidi kwa vile ndio iliyokuwa referee wake katika hicho kinyag'anyiro cha Urais wa AU.
Pamoja na matatizo yetu mangi Tanzania tumajijengea heshima ambayo mataifa mengi hayana.Pbgine siku hizi lakini hatukuwemo kwenye caliber ya kina Moubutu,Nguema,Haile Mariam au hata Bokassa.

I now shiver to think that mtu kama mama Mongella angependekezwa na Mwalimu kwa Uaris wa Tanzania
 
Hatuna kabisa umakini wa kutathmini sifa za viongozi. Anaeshangaa kuanguka kwa Mongella, hebu nitajie ulivyokuwa unamjua wewe Mongella, alikuwa na sifa gani zamani? Aliwahi kufanya nini Mama Mongella?
 
Tamaa aliumbiwa binadamu wala si fisi! Awe wa kike au wa kiume tamaa iko pale pale!
 
Hatuna kabisa umakini wa kutathmini sifa za viongozi. Anaeshangaa kuanguka kwa Mongella, hebu nitajie ulivyokuwa unamjua wewe Mongella, alikuwa na sifa gani zamani? Aliwahi kufanya nini Mama Mongella?

Mkuu hapo umenena! ndo hayo hayo tulivo ingia kichwa kichwa hata kwa mkuu wa kaya.. kiongozi ni rekodi!

huyu mama pamoja na vyeo vyote hajafanya lolote hata huko jimboni kwake anazidiwa na hasimu wake Msekwa walau alijenga shule watoto wanasoma!
 
Duu!! ufisadi wa kitanzania umevuka mipaka ya nchi?!! Angalau wabunge wa Bunge la Afrika wamesema enough is enough. No to Mongella. Let it be our motto - NO TO ALL FISADIS

Du story yote mbona ilitolewa live huku some weeks ago na mama mmoja mbunge ngangari toka Uganda alimg'ang'ania mwakilishi wetu Mama Mongella ingawa Cheyo alijaribu kusevu ngoma and it was really an embarassing situation during the session here in Midrand SA! Matatizo yetu yale ya baadhi ya viongozi wetu/ulaji na kukataa kuwajibika!
 
Huyu mama katutia aibu wote kwani nina uakika nchi yetu ili lobby wakati anagombea hiyo nafasi, and ni aibu kwa yeye ku embazzle hizo fedha na mengineyo.

Naomba hilo bunge limepeleke mahakamani kama inawezekana...na ajue haitakuwa kama Kisutu, atanyea debe, shame on her
 
Duu ametuchafua kabisa wa tz aisee kumbe ndio maana JKN alikuwa hataki tena wanawake kwenye maamuzi mazito baada ya GM kutoa siri za Kamati kuu......kazi ipo..
 
Nafikiri mama Mongella alijisahau akadhani bado yuko kwenye siasa za Bongo siasa za kubebana.
 
Taabu ya Tz..Impunity!! kiongozi anaharibu na bado tu..hachuliwi hatua..yaani uswahiba tu na urafiki!!

Lini kioongozi akiharibu..atawajibishwa????
 
Lakini huyu mama anaendelea kupeta kama mbunge wa kawaida bunge la Afrika. Alitaka kutumia weakness ya ukosefu wa clear documentation kujiongezea muda wa uongozi.
 
President Abraham Lincoln once said, "Nearly all men can stand adversity, but if you want to test a man's character, give him power."
 
Back
Top Bottom