Mama Mwantumu muogope Mungu. Hata kama si kiasi hiki wajameni!

Mama Mwantumu muogope Mungu. Hata kama si kiasi hiki wajameni!

Gobole Lenye Risasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
11,519
Reaction score
23,693
Mimi asili ya kwetu tunagonga sana ugali. Tunagonga ugali kinyama hasa halafu tunapiga kazi mpaka basi.

Huyu mama Mwantumu nashangaa kaugali kake kama ngumi na simalizi. Nimefanya huu utafiti leo mara ya 4. Siku za mwanzo nlisema pengine kuna hesabu nakosea wakati wa kula. leo nimekaa na kuanza kula kwa kufuata hatua zote.

Sijamaliza. Wallah nakataa kuna namna si bure. Kaugali kadogo kama ngumi simalizi? Nikiwa home nakula ugali size ya mpira wa miguu. Tena dona imechanganywa na ngano haijasagwa. Namaliza na nyama, matembele, na maharagwe. Nashushia na mtindi.

But kwa huyu dada mama Mwantumu sielewi jamani. Sielewi kabisa inakuaje. Nikiangalie meza za wenzangu nao naona hivyo hivyo. Siku za mwanzo aliponiletea na kutenga kaugal hako.nilicheka sana na kumwambia kaniletea dagaa nile kwa ugali.

Tena nikamwambia ule ugali ni tonge tatu tu. Alikuwa ananionjesha. Alinicheck akatabasamu. Akaniambia we baba, hebu kula. Usipotosheka nitakuongeza. Nimekaa pale 👉 akaondoka akitingisha makalio yake mbinuko.

Sikuamini macho yangu. Ule ugali sikumaliza. Nikapambana, sikumaliza, nikawaza pengine ni vile sikuanza kula kwa hatua. Na sikusema Bism...h. hizi mara 3 nyingine nafuata kanuni, taratibu na hatua zote za ulaji. Ugali kama ngumi simalizi? Hapana. Si sawa. Nakataa kabisa. Si sawa. Muogope Mungu mama, muogope Mungu. Khah!
 
Mkuu huon karahisisha maisha unakula na kusaza[emoji4][emoji4]
 
Back
Top Bottom