Alex Muuza Maembe
JF-Expert Member
- Dec 13, 2024
- 655
- 1,413
Mambo vp wadau??
Ninaomba radhi "in advance" kwa uandishi m-bovu. I'm not a gifted writer.
Kuna mama mmoja yeye ni kabila la Pwani/mzaramo. Ni mama mkaanga Samaki amepanga chumba na sebule huku mtaani kwetu (Kodi Jumla 30,000/= kwa mwezi). Huyu mama muwewe alifariki kama mwaka na nusu hivi umepita. Sasa kulikuwa na Binti mmoja alibeba ujauzito hapa mtaani, huyo Binti hana baba wala mama (umri kama miaka 16 au 17 hivi).
Huyu Binti ni Mnyakyusa wa Mbeya wazazi wake wote walifariki katika vipindi tofauti tofauti ila wa mwisho kufa alikuwa ni mama yake mzazi.
Sasa cha kushangaza huyu mama muuza Samaki, ambaye anaishi maisha magumu mno (faida ya Samaki labda ni 10,000 tu kwa siku) ameamua kumchukua huyu binti anakaa naye hapo alipopanga ilhali hana hata undugu naye.
Wanapika, wanakula, jioni wanaenda kuuza Samaki zao za kukaanga barabarani, huyu dada akiwa na tumbo la ujauzito.
Hii roho ya huyu mama mkaanga dagaa mpaka ninaogopa kwa maana katika hali ya kawaida watu wengi wenye vipato vidogo wanaogopa mizigo zaidi, lakini huyu mama kamchukua huyu Binti anakaa naye kama vile ndugu yake. Hivi wakuu, roho kama hizi huwa mtu anazaliwa nazo au inakuwaje?
Watu wa Pwani (Wazaramo, Wandengereko,n.k) Mwenyezi Mungu awabariki sana.
From my experience, wengi wenu hamkusoma sana na mna vipato vidogo, lakini Mwenyezi Mungu amewapa mioyo iliyojaa upendo mnoo.
NB: Mimi ni kabila la mkoa wa Mara na sio mtu wa Pwani.