Mama mwenye watoto mapacha walioungana kifua, amshukuru Rais Samia kwa kumgharamia matibabu

Mama mwenye watoto mapacha walioungana kifua, amshukuru Rais Samia kwa kumgharamia matibabu

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
AHSANTE RAIS SAMIA

Huyu ni Hadija Shaban Omar, mama mwenye watoto mapacha walioungana kifua, tumbo na nyonga wenye umri wa miaka Mitatu anapenda kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumgharamia kipindi cha miaka mwaka mmoja wallivyokuwa wanapata matibabu ambapo baadaye kuweza kusimamia safari yake ya kwenda hospital King Abdulaziz Medical City iliyopo Saudi Arabia.

Mama wa mapacha (Hassan na Hussein) amemuomba Mhe. Rais pindi watakaporejea nchini Tanzania aweze kumtembelea kuwaona watoto hao ambao hivi sasa wanatumia Mguu mmoja mmoja.

Hadija Shaban Omar hakusita kutoa shukrani kwa Hospital ya Taifa ya Muhimbili kwa kuwa naye kipindi chote cha Matibabu tangu wanatoka Tabora.


#samiaapp
#kaziiendelee
#tumejipatanamama
 
Screenshot_20241215-195235.png
 
Nilidhani kamshukuru Samia kwa kuwazaa hao mapacha, maana hii nchi kila kitu ni Samia.


Mimi kwa upande wangu namshukuru Samia kwa mvua zinazoendelea kunyesha
 
Hv samia kwa siku anashukuriwa mara ngapi?!
IMG-20241007-WA0000.jpg
 
Kwake yuko sahihi kuwashukuru hao, hizi kodi zetu kama zimemsaidia, lakini wapo wengi hizo kodi hazijawasaidia, yuko sahihi kushukuru kwa waliojitolea kumpa furaha kwenye maisha yake na wanawe.

Allah akbar!
 
Hakika, wema wa Mh. Rais ni mkubwa sana, Mungu aendelee kumbariki
 
Back
Top Bottom