A
Anonymous
Guest
Hii si hadithi, ni maisha halisi ndani ya Jiji la Dar es Salaam, ni kuhusu mwanafunzi wa kike anayesoma Kidato cha Nne katika Shule ya Kimbiji Secondary School.
Msichana huyo jina nalihifadhi amekuwa katika mgogoro wa muda mrefu na mama yake mzazi, ambapo mama anashinikiza mwanaye aondolewe shuleni, wakati huohuo yeye mwenyewe amemfukuza nyumbani.
Kibaya zaidi Mwanafunzi yupo katika mwaka wa mwisho shuleni hapo ambapo anatarajiwa kuwa mmoja wa watakaofanya mtihani wa taifa wa kuhitimu.
Kutokana na “sumu” ya mama mtu imefikia hatua hata Mwalimu Mkuu naye anataka kumtenga, kwa ufupi saikolojia ya mtoto imeharibika na amekuwa akipitia changamoto nyingi ikiwemo za masuala ya afya.
Inawezekana kweli mtoto ana makosa lakini kwa historia ya mama huyo, sisi ambaye tumeishi naye hapa mtaani tumeona hii si mara yake ya kwanza, alishawahi kumfanyia hivyo mtoto wake mkubwa, ambapo alifikia hatua ya kumwambia amekua, aondoke akajitafutie wakati akiwa bado anasoma sekondari.
Elewa neno “akajitafutie”, ikabidi kweli binti akajitafutie kwa Wanaume mbalimbali.
Mama huyo ambaye alikuwa akifanya kazi hospitalini kama mfanyakazi wa usafi, alisimamishwa kazi mapema mwaka 2026, tangu wakati huo ugomvi ndani ya nyumba ulikuwa wa kila siku kati yake na binti yake huyu wa sasa anayesoma kidato cha nne.
Binti huyu amekuwa na changamoto kubwa za kiafya; anasumbuliwa na vidonda vya tumbo pamoja na maumivu makali ya tumbo la uzazi, kiasi kwamba kila wiki amekuwa akihitaji matibabu.
Licha ya yote hayo bado anaonesha uwezo darasani, mwezi wa sita 2026 alipata alama za juu.
Natoa wito kwa Serikali ikiwemo mamlaka za elimu kufanya uchunguzi kuhusu kinachoendelea kwa binti huyo na mzazi wake, tunapoelekea inaweza kuwa mbaya zaidi kwake.
Waangalie namna ya kumrekebisha kwa kuwa bado ni mtoto, kuendelea kumkandamiza ni kuzidi kuharibu afya yake ya akili, pia wito kwa mamlaka zinazohusika zimuangalie mama yake mzazi kwani kitendo cha kuwa anawaambia mabinti zake kuwa wakajiongeze kutafuta hela wakiwa na umri mdogo ni kutengeneza mazingira ya kuwaharibu Watoto wake na wengine wote wanaowazunguka.