Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
MAMA HAYA NDIYO NILIYOJIFUNZA HUKO CHUONI.
Kwa Mkono wa, Robert Heriel
"Mama nashukuru kwa kuja kwenye mahafali yangu, nimefurahishwa sana na ujio wako ingawaje nilitamani Baba pamoja na ndugu zangu nao wangekuwepo, lakini haikuwa hivyo, nafahamu sisi ni masikini tena fukara wenye hasara ya maisha"
" Mwanangu..! Sasa umekuwa mtu wa heshima, kama mama najivunia kuwa na mtoto mwerevu kama wewe, tazama joho ulilovaa, ona kofia ilivyojaa utukufu wa maarifa yasiyo na maafa, Ni dhahiri umekuwa mtu bora" Mama yangu aliongea akitabasamu, Nuru ya ufahari ilizingira uso wako, pengine niseme sikuwahi kumuona Mama akiwa na uso wa furaha kama ule.
Nilibaki nimemtazama huku nami nikimlipa hisani ya tabasamu jepesi la shukrani,
" Baada ya dhiki ni faraja, heloheloo! Dhiki ilinidhihaki kwa chuki isiyomithilika. Niliteseka mimi! Niliumia mimi jamani! Mitumba mimi....! Vikoba Mimi...! Mikopo mimi..! Kipi si kufanya ili usome! Nilikula ugali pasi na mboga ili mwanangu uvae joho siku ya leo. Nilikula tembele mchemsho ili nawe uwe bora mwanangu. Mungu hamtupi mja wake leo umehitimu, hakika machungu yote umeyafuta, bila shaka machozi nayo utayakausha"
Mama aliongea kwa uchungu mara hii machozi yakiwa yanamlenga lenga.
Hapo nikamkumbatia mama kwa upendo wote, nikasikia mapigo ya moyo wake yakidunda kwa mapenzi ya mama na mtoto. Kama ningejua lugha za moyoni ningeweza kusema moyo wa mama ulikuwa ukiniambia unanipenda, unanijali, na kunithamini. Hata hivyo mimi sio mjuzi wa lugha za moyoni ila hisi zangu tuu ndizo zinaniambia hayo.
" Nashukuru kwa yote Mama, nashukuru kwa kunilea na kunisomesha, wewe ni shujaa wangu, umekuwa mama mwema kwangu. Umejitoa kwangu kuliko hata ningejitoa mimi. Siwezi fananisha upendo wako wala kuulinganisha" Niliongea nikiwa nimemkumbatia mama, hapo nikamsikia akishikwa na kwikwi. Nikajua ameanza kulia, hisia za utamu zilimzidia na uwezo wa kuzizuia ukamponyoka.
Hii ni mara ya pili kumuona Mama yangu akilia, mara ya kwanza ilikuwa kwenye msiba wa Baba miaka mingi iliyopita. Hii ni kusema Baba alifariki tukiwa wadogo mimi na wagogo zangu.
Tofauti na kilio cha siku ile ya msiba wa Baba na siku ya leo ni kuwa, kipindi kile Mama alilia kwa uchungu na huzuni kubwa lakini leo hii alilia kilio cha utamu na furaha kubwa ya mwanaye kuvalishwa joho na kofia ya kuhitimu shahada ya juu kabisa katika chuo bora hapa nchini.
Mama akaniachia, uso kwa macho tukatazamana, nikayona machozi yakitirrika katika mashavu yake yaliyofubaa kwa taabu za maisha, kulia kwake kuliongeza macho yake kuwa mekundu. Nilijikaza nisilie kwani hisia za huzuni zilinishutumu kwa ukaidi, hata hivyo sikutaka kutoa hata tone moja la chozi kwani nilijua kama ningetoa machozi ningemfanya mama yangu kulia zaidi.
Mama akachukua mfuko ambao ndani yake akatoa boksi lililorembwa kwa manila kadi, kama mnavyojua mambo ya sherehe za mahafali. Macho yangu yakatulia kwenye lile boksi alilokuwa amelibeba Mama nikijua kuwa ndani yake ingekuwepo zawadi yangu. Shauku ya kujua ni zawadi gani ikanikaba kooni hali iliyofanya nimeze mafumba ya mate kulainisha koo langu.
Mama akatoa Msahafu ndani ya lile Boksi, ulikuwa msahafu mzuri sana. Kisha akanitazama machoni akinidadisi kuona kama nimeifurahia zawadi yake au laa. Kwa kulijua hilo nikatasamu kisha nikasujudu mpaka ardhini kwa heshima na kuupokea ile zawadi ya Msahafu aliyoniletea Mama yangu kipenzi.
Hapo nikamsikia Mama akisema;
" Mwanangu Taikon, kama kuna jambo lililokuwa likinisumbua na kunipasua kichwa ni hili la zawadi yako. Unajua fika kabisa mimi mama yako ni masikini, sina pesa! Sina zawadi ya kukufanya uchangamke moyo wako kama vile wenzako wapewavyo zawadi na wazazi wao. Usijisikie vibaya mwanangu. Huu msahafu niliununua kwa pesa za chapati nilizodunduliza kwa miezi takribani mitatu. Niliona zawadi hii ingekuwa bora kwako ambayo itakufaa wewe kuendelea kuwa bora kama hivi leo." Hapo akameza mate mimi bado nikiwa nimesujudu nikimtazama kwa juu nikiwa nimeushika ule msahafu, wote tulikuwa tumeushika, yeye akinikabidhi mimi nikiupokea.
" Humo kuna elimu ya milele, kuna maarifa ya vizazi na vizazi, zama na zama. Usichoke kuchota elimu katika kitabu hiki. Kitabu hiki kina yote uyatakayo kwa kadiri ya vile uonavyo. Usome, sawa Mwanangu?"
Nikajibu " Sawa"
Baadaye Mahafali yaliisha, tukarudi nyumbani. Huko kijijini kwetu. Watu wengi walinipongeza, wengine walihisi mwokozi wa kijiji amefika. Kijijini kwetu tulikuwa watatu tuliohitimu. Basi nilijionea fahari kabla ya hatari kujitokeza siku kadhaa za usoni.
Mama alijua kunisomesha kamaliza, kumbe kamalizwa. Alihisi ahueni mwanzoni lakini kitambo kidogo ahueni ikageuka maradhi yasiyotibika. Naam magonjwa ya akili na kuwehuka.
Sasa nikaanza kutafuta kazi ili kurejesha tumaini la mama yangu, kipenzi changu aliyesota miaka nenda bila kurudi akinisomesha.
Lakini asiye na bahati habahatishi na ng'ombe wa masikini hazai.
Kila nilipogusa nilinata, kila nilipokanya nilizama, mambo yalikuwa magumu kuliko mwanzo.
Nikaanza kugombana na Mama, mama akaniona mimi mvivu, goigoi na zoba kwani elimu yangu haikuwa na msaada wowote pale nyumbani. Ilifikia kipindi Mama akaona labda nimelogwa si unajua mambo ya jamii zetu za Kiafrika. Lakini haikuwa hivyo, na Taikon siamini mambo ya Ulozi na miti.
Siku moja Mama akaniuliza huko chuoni ulienda kusomea nini?
Swali hilo lilinifanya sukari yangu kushuka na presha kupanda. Moyo ulitafaruku, akili ikavurugika huku macho yakishindwa kuhimili ujazo wa machozi, nilijikuta natoa mililita za machozi.
Mama yangu, haya ndiyo niliyosomea huko chuoni;
1. Nilisomea kuwaheshimu wakubwa na watu wenye cheo. Huko chuoni huitwa madokta na Maprofesa. Kwa huku mtaani nafikiri wakubwa ni Wanasiasa na wenye vipato vya juu.
2. Chuoni nilifundishwa kuhesimu na kutunza muda hasa wa mtihani zaidi kuliko kujifunza. Ilikuwa rahisi kwa Mkufunzi kuchelewa ufikapo muda wa kufundisha kwenye vipindi lakini ni ngumu kwa mkufunzi kuchelewa katika muda wa mitihani. Hii ilimaanisha kuwa mitihani na majaribio katika maisha kamwe haiwezi kuchelewa inafika kwa muda mahususi kabisa.
3. Chuoni nilifundishwa kuwaona watu wa zamani ndio wanahoja kuliko mimi mwenyewe. Niliambiwa ni sharti ni rejelee wataalamu wa zamani kama walivyoandika, hali hiyo ikaua ubunifu wangu, na hapa nilipo natumia ubunifu wa watu waliokufa ambao waliacha vitabu tuu. Hii ni kusema ubunifu wangu kwa sasa ni sifuri kabisa.
4. Shuleni nilifundishwa kufanya mambo kifomula na kimpangilio kwa kufuata mfumo. Lakini nilichokutana nacho huku mtaani hakuna fomula, hii ni kusema maisha hayana fomula yapo zigzag randomly.
5. Shuleni nilifundishwa Kulipwa pesa hawakunifundisha kutafuta.
6. Shuleni nilifundishwa kujiona nina akili wakati wote wakati huku mtaani ili ufanikiwe lazima utumie akili kwenye ujinga, na kwenye akili utumie ujinga.
7. Chuoni nilifundishwa kazi zenye pesa ni mpaka uchomekee na upige tai nyekundu shingoni lakini mtaani kazi zinazodharaulika ndizo zenye pesa
8. Chuoni nilifundishwa nikifaulu sana ndio nitakuwa na maisha mazuri, huku mtaani mambo ni tofauti kumbe ukifanya kazi sana kwa bidii na ujanja ujanja ndio unakuwa na maisha mazuri.
9. Chuoni nilifundishwa adabu lakini mtaani hakuna adabu.
10. Chuoni nilifundishwa kupenda kusoma vitabu na maandishi, na nimesoma maandishi mengi. lakini ajabu ni kuwa mtaani hakuna wasoma vitabu wala maandishi na maisha yanaenda.
11. Chuoni nilifundishwa kuwa elimu ni ufunguo wa maisha, lakini mtaani Uzoefu ndio ufunguo wa maisha.
12. Mama, chuoni nilifundishwa kuwa elimu ndio kila kitu, lakini huku mtaani siasa ndio kila kitu. Wanasiasa ndio wameshikilia hatma ya watu na wala sio wenye elimu
Je mama tumepigwa?
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro Mjini
"