Aksante Afrodenzi kwa kutukumbusha siku muhimu kama ya leo kuhusu mama.
Kweli mama ni wa muhimu,mimi nilipata ajali mbaya sana nikiwa mdogo wa umri wa miezi kumi,pamoja na ushirikiano wa baba,ila mama ndiye aliyekuwa na mimi pale Mount Meru Hospital,huwa akinielezea jinsi alivyopita katika kipindi kigumu cha malezi yangu,na ambavyo ndiyo ni mtoto wake wa kwanza moyo wangu huzidi kumpenda.
hata inapotokea watu kunikejeli jinsi nilivyo,nikaugua rohoni nikienda kwake maneno yake hunipa faraja nakuendelea kumuona ni mshindi kwani kwa mateso aliyopata hakushindwa kukata tamaa,bali alizidi kuwa pamoja nami.
na kwasasa mimi ni mama,upendo kwa mama umeendelea kukua zaidi na zaidi.
Namshukuru Mungu sana kwa ajili ya mama yangu, na aendelee kuwapa ulinzi na moyo wa uvumilivu,upendo wamama woote,na wanaotarajia kuwa mama.