Mama nyau, nasema ukweli mtupu; sijui vitoto vyako vimeenda wapi.

Stephen Ngalya Chelu

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2017
Posts
8,252
Reaction score
18,335
Ni kweli Mama nyau hivi majuzi nilikuona uko na vitoto vyako vidogo viwili(vifaranga vya nyau) ulikuwa unavinyonyesha. Na baada ya muda ukaondoka ukaviacha pekeyake, mimi nikajua umevitelekeza hivyo nikavichukua na kuviweka ndani kwa sababu nawapenda nyau hasa tunyau tudogo kama huto tutoto twako.

Baada ya wewe kurudi ukavikosa vifaranga vyako ukaanza kulia unajigaragagaza chini na kuparamia maua yangu ukivililia. Nilikuonea huruma sana ila nikasema tu ngoja nikaze, nikakaza. Ukaondoka, juzi usiku ukaja ukalia usiku kucha sikulala unanisumbua unawataka wanao. Wanao wenyewe sijui ulikuwa unawanyanyasa! Kwa sababu pamoja na wewe mama nyau kuwalilia wenyewe walikuwa hawana hata mpango na wewe, walikuwa wanetulia tu kimya. Jana usiku ukaja tena kunisumbua nikaona isiwe tabu nikafungua mlango ukaingia sebuleni na vitoto vyako vikatoka chumbani kwangu vikakufuata na kwa macho yangu nilikuoneni mnatoka nje mkiwa mmeongozana na tunyau twako. Nikafunga mlango nikalala nikiwa najua kuwa tatizo limekwisha.

Nashangaa tena, alfajiri ya leo masaa machache tu baada ya wewe na vitoto vyako kuondoka umerudi ukiwa pekeyako unalia tena. Kwani nini tatizo, vitoto vyako si nilikupa ukaenda navyo? Kama vimekutoroka huko mlikokwenda basi ni uzembe wako na havijarudi kwangu tena. Naona unanitazama kwa jicho kali ila ukweli ndo huo mama nyau, mimi siko na wanao tena. Nimechoka na makelele yako ukiendelea kunisumbua nitakuonyesha kazi.
Cc: Mama nyau
 
Kwa hatua za awali sijaelewa kitu, pengine hajakusudiwa kusomwa na watu wa ufahamu wangu, na kama ni fasihi nafikir ni zaidi ya stori za kusadikiaka na kufikirika za shaban robert
 
Nyau wangu naishi naye SEMA kanaumwa mafua toka week iliyopita msaada nikape dawa gani wadau.nisaidieni kukatakieni na pole
 
Umenikumbusha story za bibi nyau.... Kibaraza chake kilikua hakikauki nyau si chini ya 15... Alifariki mpweke miaka ya 2000's...Mungu amrehemu ile nyumba yake barabarani pale sijui inaendeleaje... Sijapita kitambo ile njia serikali imeisahau barabara ya mtogore...

R.I.P BIBI NYAU
 
Yule ambaye alikuja kuuawa na majambazi?
 
Kwa hatua za awali sijaelewa kitu, pengine hajakusudiwa kusomwa na watu wa ufahamu wangu, na kama ni fasihi nafikir ni zaidi ya stori za kusadikiaka na kufikirika za shaban robert
Hapana mkuu, hivyo ilivyo ndivyo ilivyo. Usiku wa leo sijalala kwa raha, mama nyau anawataka wanae.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…