Basi Nenda
JF-Expert Member
- Jul 29, 2017
- 20,774
- 47,866
Itakumbukwa mnamo 1964 General Mobutu alianzisha mashambulizi huko Rusizi plain (Uvira), eneo hili lilikuwa linashikiliwa na waasi wa Simba-Mulele ,kwa usaidizi wa anga wa jeshi la Marekani mashambulizi haya dhidi ya waasi yanapata changamoto, waasi ikasemekana wanapewa dawa na bibi kizee mmoja aliyeitwa mama Onema, dawa hii inazuia Risasi yani ukiwatupia Risasi zinaletelza kama maji pale zikigusa miili yao.
Wabelgiji walimuona bibi huyu ni mchawi huku waasi wa Simba-mulele walimuona ni tabibu wa tiba za asili kama alivyo waganga wengine tu,bibi huyu aliwapa dawa pia viongozi wa kundi la waasi.
Bibi huyu alikamatwa january,25,1965 na jeshi la serikali na aliuliwa kwa amri ya Major general Mobutu,wakati huo akiwa Mkuu wa jeshi la Congo,sababu ya kutoa amri ya kifo cha huyu bibi ni kuzuia asije akaandaa mrithi wa mikoba yake ya uchawi,lakini licha ya kumuua inasemwa pia binti wa bibi huyu alikuwa mchawi.
Kifo cha huyu bibi ndio kilichangia hii leo kuwepo waasi wanajiita mai mai huko Congo kwa sababu ya uwepo wa dawa inayodaiwa kugeuza risasi kuwa maji.
CREDIT: Benjamin Babunga Watuna, Twitter