Mama ongea na Mwanao Wamkana Wema Sepetu

Kumbe tuna wasanii matahira hivyo?
Wamekwama kufanya bongo movie wamekuja kutumika kwenye siasa mkuu...!

Kazi mnayo! Afu utawasikia wakisema wananchi hamsapoti kazi zao...

Kama kazi zenyewe ni drama sasa unasapoti nini...?
 
Hii nayo ni campaign au vipi , maana kama namuona captain Kombi
 
Eti wanasema wao ni makada halali wa CCM. hivi kada maana yake nini? Maana naona kila mtu anajiita kada. Ila CCM yenyewe imekaa kimya. Hawa malay* waganga njaa tu kujipendekeza CCM halafu sijui hata jina la mmoja hapo. Sijui hata bongo movie gani haw
Hata mimi sijawahi kuona kada wa chama anayelipwa apige kampeni ili chama chake kishinde uchaguzi. Labda neno 'kada' linamaana tofauti siku hizi.
 
sisiem wanawalipa wasanii kuwashika maskio wananchi.Ccm hoyeee
 
Wasanii wa filamu za Kibongo, leo wameitisha mkutano na waandishi wa habari ambapo wamekanusha kuidai CCM huku wakisema kwamba wote walilipwa.
Tazama video...
Wasanii Bongo Movies Wampinga Wema Sepetu, Wakanusha Kuidai CCM

MOVIE BADO INAENDELEA: Hivyo ndivyo tunaweza kusema baada ya wasanii wa Bongo Movie Wasanii wa Bongo Movies waliokuwa wakishiriki kwenye kampeni ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ya Mama Ongea na Mwanao ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kukanusha taarifa iliyotolewa na Wema Sepetu kuwa CCM haijawalipwa pesa za kampeni walizofanya kwenye uchaguzi huo.

Wakizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Protea, wasanii hao wakiongozwa na Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ na Ndumbangwe Misayo ‘Thea’, wamesema madai aliyoyatoa Wema Sepetu hayana ukweli wowote kwa sababu wasanii wote walilipwa na Wema alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakiwalipa wasanii hao.

Mara baada ya Thea na Yobnesh kuzungumza maneno machache, mkutano huo na waandishi wa habari ulimalizika, ukiwa umechukua dakika chache tu na kuacha kila mtu akaizungumza lake.

“Ni kweli inasemekana kwenye mitandao kuwa tulifanya kampeni na hatukulipwa, mimi kama Mwenyekiti Msaidizi wa Muda, nakanusha taarifa hizo kuwa si za kweli… wapo wanaoshawishiwa kulichafua kundi letu, kumchafua Makamu wa Rais Bi. Samia Suluhu na kuichafua CCM, mimi nakataa, sote tumelipwa na mikataba ipo.

“Zipo simu za kushwishiwa kuhama lakini hatutohama chama na Kundi la Mama Ongea na Mwanao litaendelea kuwepo chini ya Usimamizi wa Bi. Samia Suluhu.” Alisema Batuli.

Wema Sepetu alivyohamia Chadema.

Hivi karibuni msanii wa Bongo Movie, Wema Sepetu aliibuka mbele ya wanahabari wakati akihamia Chadema kwa madai ya kufanyiwa hila kwenye CCM huku akidai kuwa Kundi la Mama Ongea na Mwanao linakidai CCM pesa yao ya kampeni waliyofanya mwaka 2015.

Steve Nyerereakikanusha taarifa za kukidai CCM.

Aidha siku moja baadaye msanii wa filamu na mchekeshaji maarufu Bongo, Steve Nyerere aliyekuwa mwenyekiti wa Kundi hilo wakati wa kampeni aliibuka na kukanusha taarifa za wasanii wa Bongo Movie kukidai CCM huku akieleza kuwa wasanii wote walilipwa pesa zao kama mikataba iliyokuwa ikieleza.

Chanzo: GPL

Wote wanatafuta kitembelea nyota ya Wema
 
wakwendage uko... tuko biz na daudi wasituchanganye...
 
  • Thanks
Reactions: lcm
''Waandishi'' wa habari wa TZ ni majanga kwa kweli. Acha ile board aliyoianzisha Nape ije tu maana hakuna hamna.
 
Wakati tunaendelea na mijadala serikali mdogomdogo inaelekea dom tutashka siku tunaambiwa magu anaondoka kesho....kama kunatilewa ktk hoja za msingi vile?
 
Hakuna celebrity wa kike alikaa kwenye game miaka 11 na bado anawakimbiza. Wote hao takataka kwa Wema
 
Wema anajua kutafuta kick
sasa kawapata wapuuzi
na huyu mwezi huu ndio mwisho kwake
hii kick inabuma vibaya
 
SHIGONGO KADAI HELA ZAKO WENZIO WOTE WAMELIPWA WEWE KILA SIKU UNAPEWA MAJI YA KUNYWA YA MIA TANO.
 
Back
Top Bottom