Mama Polepole afika Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Ndogo ya Dar es salaam

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Anna Mary ambaye ni Mama Mzazi wa Mwanasiasa Humphrey Polepole amefika katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Ndogo ya Dar es salaam asubuhi hii ambako inatarajiwa kuanza kusikilizwa kwa maombi ya kesi juu ya kutekwa kwake maombi ambayo yalipelekwa na Wakili Peter Kibatala kuiomba Mahakama Kuu chini ya hati ya dharura, itoe amri ya kwamba Polepole afikishwe Mahakamani ama Mamlaka husika ziseme yupo wapi.

Kwa mujibu hati iliyosajiliwa baada ya kupokelewa kwa maombi hayo na kupewa namba 24514 ya mwaka 2025, maombi hayo yamepangwa kusikilizwa mbele ya Jaji Salma Maghimbi ambapo katika maombi hayo Kibatala ameiomba Mahakama iingilie kati mara moja akidai kuwa Polepole alitekwa nyara alfajiri ya Jumatatu, tarehe 6 Oktoba 2025 kutoka katika makazi yake yaliyoko eneo la Ununio, Wilaya ya Kinondoni, Dar es salaam na Watu waliotajwa kuwa ni Askari wa Jeshi la Polisi la Tanzania.

Katika hati hiyo ya dharura Wakili Kibatala ameieleza Mahakama kuwa Polepole hajawahi kushtakiwa kwa kosa lolote la jinai katika Mahakama yoyote, na kwamba kwa sasa inaaminika anashikiliwa katika eneo lisilojulikana na maafisa wa Jeshi la Polisi.

Maombi hayo yamewasilishwa dhidi ya wajibu maombi watano akiwemo Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP), Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Afisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalum ya Dar es Salaam (RCO) na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (RPC).

Pia Soma:

Wakili Peter Kibatala na ndugu wa Polepole Mahakamani​
 
Annamary ambaye ni Mama Mzazi wa Mwanasiasa Humphrey Polepole amefika katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Ndogo ya Dar es salaam asubuhi hii ambako inatarajiwa kuanza kusikilizwa kwa maombi ya kesi juu ya kutekwa kwake maombi ambayo yalipelekwa na Wakili Peter Kibatala kuiomba Mahakama Kuu chini ya hati ya dharura, itoe amri ya kwamba Polepole afikishwe Mahakamani ama Mamlaka husika ziseme yupo wapi.

Kwa mujibu hati iliyosajiliwa baada ya kupokelewa kwa maombi hayo na kupewa namba 24514 ya mwaka 2025, maombi hayo yamepangwa kusikilizwa mbele ya Jaji Salma Maghimbi ambapo katika maombi hayo Kibatala ameiomba Mahakama iingilie kati mara moja akidai kuwa Polepole alitekwa nyara alfajiri ya Jumatatu, tarehe 6 Oktoba 2025 kutoka katika makazi yake yaliyoko eneo la Ununio, Wilaya ya Kinondoni, Dar es salaam na Watu waliotajwa kuwa ni Askari wa Jeshi la Polisi la Tanzania.

Katika hati hiyo ya dharura Wakili Kibatala ameieleza Mahakama kuwa Polepole hajawahi kushtakiwa kwa kosa lolote la jinai katika Mahakama yoyote, na kwamba kwa sasa inaaminika anashikiliwa katika eneo lisilojulikana na maafisa wa Jeshi la Polisi.

Maombi hayo yamewasilishwa dhidi ya wajibu maombi watano akiwemo Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP), Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Afisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalum ya Dar es Salaam (RCO) na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (RPC).
 
Anna Mary ambaye ni Mama Mzazi wa Mwanasiasa Humphrey Polepole amefika katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Ndogo ya Dar es salaam asubuhi hii ambako inatarajiwa kuanza kusikilizwa kwa maombi ya kesi juu ya kutekwa kwake maombi ambayo yalipelekwa na Wakili Peter Kibatala kuiomba Mahakama Kuu chini ya hati ya dharura, itoe amri ya kwamba Polepole afikishwe Mahakamani ama Mamlaka husika ziseme yupo wapi.

Kwa mujibu hati iliyosajiliwa baada ya kupokelewa kwa maombi hayo na kupewa namba 24514 ya mwaka 2025, maombi hayo yamepangwa kusikilizwa mbele ya Jaji Salma Maghimbi ambapo katika maombi hayo Kibatala ameiomba Mahakama iingilie kati mara moja akidai kuwa Polepole alitekwa nyara alfajiri ya Jumatatu, tarehe 6 Oktoba 2025 kutoka katika makazi yake yaliyoko eneo la Ununio, Wilaya ya Kinondoni, Dar es salaam na Watu waliotajwa kuwa ni Askari wa Jeshi la Polisi la Tanzania.

Katika hati hiyo ya dharura Wakili Kibatala ameieleza Mahakama kuwa Polepole hajawahi kushtakiwa kwa kosa lolote la jinai katika Mahakama yoyote, na kwamba kwa sasa inaaminika anashikiliwa katika eneo lisilojulikana na maafisa wa Jeshi la Polisi.

Maombi hayo yamewasilishwa dhidi ya wajibu maombi watano akiwemo Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP), Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Afisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalum ya Dar es Salaam (RCO) na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (RPC).

Pia Soma:

Serikali yawekwa mtegoni .

Ikikubali inapaswa kumrejesha,kuonyesha alipo au kumfungulia shitaka .

Ikikataa kama ilivyokataa kwa wengine pia ni mtego ,maana yawezekana wanafamily wakawa na aidha na ushahidi wa Video , picture za tukio ambazo zikija kuwekwa hadharani litakuwa ni balaa jingine kwa serikali na chama cha mapinduzi hasa kipindi hiki cha campaign .

Kukataa kuwa hawajahusika ni jambo jepesi lakini nijambo lenye madhara makubwa .

Very smart move , Kibatara yuko very strategic.

Kwa waunganishaji matukio tuanzie hapa , Polepole aliwahi kueleza mkasa wa kutekwa kwa Dada yake , alionyesha wanataarifa nzima kuhusu watekaji kuanzia waliyohusika na aliyetoa oda (bila shaka wanahadi video zake na ndiyo maana hata ile siku anaongea na mwandishi wa BBC yule Mama alisema wazo kuwa hata bint yake alitekwa na hao hao , tunadhani ile kauli ilitoka kwa bahati mbaya? No, inaonyesha wanaushahidi wa tukio zima ,tujiandae kusikia moja kati ya mawili ,kama siyo siku za hivi karibuni family kuvamiwa tena kwa lengo la kwenda kuutafuta ushahidi basi kwenda kuteketeza wenye ushahidi.

Kwa upande wa Wakili wao, je! Hatapigwa mpunga ili nae atulie?

Vipi akigoma?
Je! Nae siyo wa system?

Ngoja tuone.

Inji ngumu hii.

Ngoja tuone.
 
Uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi,

The love of mother is pure,selfless and infinite,
I can feel it how his mother feeling,
 
Mke wa Mdude, wazazi wa Ben Saanane walipowasilisha kesi za kupotelewa/kutekwa kwa wapendwa wao, Mama HP hakuwahi kuwaza kwamba naye atakuja kufungua kesi ya aina hiyohiyo. Nani ajuaye kesho itakuwa zamu ya nani?
 
Ignoring the suffering or misfortune of others will eventually lead to a similar negative outcome for you,
Don't ignore when things went wrong to others,it may come your turn.
 
tujiandae kusikia moja kati ya mawili ,kama siyo siku za hivi karibuni family kuvamiwa tena kwa lengo la kwenda kuutafuta ushahidi basi kwenda kuteketeza wenye ushahidi.
Wanapaswa kupewa hii tahadhari kabla ya hatari
 
Kama haya yametokea kwa polepole, yatotokea kwa akina SSH na wengine miaka ijayo. Hakuna mwenye uhakika tanzania naona.
 
Back
Top Bottom