Mama Samia Legal Aid Campaign

Mama Samia Legal Aid Campaign

kalacha mateo

Senior Member
Joined
Sep 27, 2021
Posts
119
Reaction score
240
Katika kuunga Mkono jitihada za Rais Samia Suluhu kujenga Tanzania bora yenye ustawi, Wizara ya Katiba na Sheria imezindua kampeni ya Mama Samia ya msaada wa kisheria kwa lengo la kutoa msaada wa kisheria nchi nzima kwa miaka mitatu.

Kampeni hiyo itaelimisha haki ya kulinda mila na desturi nchini, kupingana na mila potofu kutoka nje ya nchi na utoaji msaada wa kisheria kwa kuongeza uelewa wa kisheria na haki za binadamu kwa jamii. Kampeni hiyo itajulikana kama "Mama Samia Legal Aid Campaign".

Kauli mbiu ya kampeni hiyo ni "Ungana na Mama Samia Kupinga Ukatili, Heshimu Utu wa Mwenzako; Linda Mtoto wa Mwenzako; Tujenge Nchi yenye Staha, Heshima na Amani."

Kampeni hiyo imepewa jina la Rais Samia Kutokana na jitihada zake za kuzingatia haki za binadamu, utawala wa sheria, utii wa sheria na elimu ya kikatiba na ya kisheria kwa umma.
 
..sasa kama Mama Samia na serikali wanafanya harakati nani atafanya kazi ya kuongoza?
 
Back
Top Bottom