Mama Samia Leo nimekuelewa sana

Mama Samia Leo nimekuelewa sana

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
16,295
Reaction score
33,994
Binafsi naweza kusema hii ni moja ya hotuba nzuri sana kutoka kwa Madam President.👏👏👏

1. Suala la Viongozi kujiamini na kufanya maamuzi ambayo wataweza kuyatetea, maana yake wakizingatia hili watafanya informed decision, zenye kuzingatia maslahi ya wengi, kuengage kabla ya kuamua na kutumia kiwango cha juu sanaa cha akili zao badala yakuamua tu ilimradi.

2. Taarifa vs Mawasiliano ni jambo muhimu sana kwa Viongozi kujua hilo tumeona Viongozi wamekuwa wakitoa matamuko ambayo ukienda kwenye utendaji hayafafanuliwi, kwa kuzingatia hoja hii Viongozi na watendaji hatapaswa kutoa tamko tu bila official communication.

3. Suala la kufanya kazi mpaka ukomo wa taratibu na endapo inatokea sheria imegota basi ubunifu muhimu kujua je kuna haja ya marekebisho, ikiwa kuna marekebisho angalizo yasiwe kwa maslahi binafsi maana unaweza kuta sheria inarekebishwa kwa cure jambo la msimu tu na kwa manufaa yawachache kukiwa na leeway ambayo ni uncontrolled.

4. Succession plan nakuangalia succession hiyo inatija!!! huyu mtu au watendaji wa chini wanauwezo wakukupa na kukushauri vizuri au kuweka watu ambao utapenda wakuamubudu au kutembelea kwenye viatu vya wakubwa kuliko ubunifu! hili nalo muhimu sanaa.

5. Kuheshimu watu wananchi na sekta binafsi haya mambo muhimu sana kimsingi Watendaji wakifuata haya watafanya kazi vyema sana.

Britanicca
 
Binafsi naweza kusema hii ni moja ya hotuba nzuri sana kutoka kwa Madam President.[emoji122][emoji122][emoji122]

Shida ni Watendaji au Makada wa chama chake ambao wanaenda kukagua miradi na kutoa maagizo badala ya kushauri.Hiyo semina inapaswa iwaguse na makada wake wa CCM ambao huwa wanaropoka sometimes!
 
Binafsi naweza kusema hii ni moja ya hotuba nzuri sana kutoka kwa Madam President.👏👏👏

1. Suala la Viongozi kujiamini na kufanya maamuzi ambayo wataweza kuyatetea, maana yake wakizingatia hili watafanya informed decision, zenye kuzingatia maslahi ya wengi, kuengage kabla ya kuamua na kutumia kiwango cha juu sanaa cha akili zao badala yakuamua tu ilimradi.

2. Taarifa vs Mawasiliano ni jambo muhimu sana kwa Viongozi kujua hilo tumeona Viongozi wamekuwa wakitoa matamuko ambayo ukienda kwenye utendaji hayafafanuliwi, kwa kuzingatia hoja hii Viongozi na watendaji hatapaswa kutoa tamko tu bila official communication.

3. Suala la kufanya kazi mpaka ukomo wa taratibu na endapo inatokea sheria imegota basi ubunifu muhimu kujua je kuna haja ya marekebisho, ikiwa kuna marekebisho angalizo yasiwe kwa maslahi binafsi maana unaweza kuta sheria inarekebishwa kwa cure jambo la msimu tu na kwa manufaa yawachache kukiwa na leeway ambayo ni uncontrolled.

4. Succession plan nakuangalia succession hiyo inatija!!! huyu mtu au watendaji wa chini wanauwezo wakukupa na kukushauri vizuri au kuweka watu ambao utapenda wakuamubudu au kutembelea kwenye viatu vya wakubwa kuliko ubunifu! hili nalo muhimu sanaa.

5. Kuheshimu watu wananchi na sekta binafsi haya mambo muhimu sana kimsingi Watendaji wakifuata haya watafanya kazi vyema sana.

Britanicca
Huzuni na sikitiko lq kitaifa ni pale madam anapozungumza asiyoyatenda.

Hasara ya kutumbua incompetent leader na kumuacha aendelee kutia hasara jwa sababu kumuandaa ni gharama nani analipia hizo gharama za hasara?

Kila siku anaonya, anaonya na kuonya lakini wanaoonywa wanazidi kuwa wagumu kubadilika kiutendaji.

Uteuzi wa kufutana machozi wakati msiba umeshaisha....

Aanze kuiangalia taasisi yake awatoe wote wanaomtengenezea mapichapicha kisha aisuke serikali upya.
 
Mama anapiga pasi kama Xavi Harnandez, anazungumza kwa kiada wala hana mapayo na mikwara.
 
Amewaambia Kile mnataka kusikia.. Utekelezaji haupo
Kama anatambua wakosa si awafute kazi..
Huku kupeana vyeo kama bakshishi shida inaanzia hapa…
Wanapenda kusikia maneno matamu lakini utendaji zero.
Watuonyeshe changes ktk utendaji na deliverance. Kama hakuna deliverance basi maneno matamu hayana maana.
 
Hakuna jipya haya ni maneno tu, Siasa za Kiafrica ni michosho mitupu jambo kubwa na la kujivunia kwa nchi yetu Tanzania ni Amani na Upendo tulio nao katika maisha yetu ya kila siku. Maneno ya Wanasiasa ni kama dawa ya Panadol tu inatuliza maumivu baada ya muda mfupi yanarudi tena. Mamlaka ya Rais katika uteuzi yapunguzwe.
 
Kwa kumsikiliza ‘bi tozo’ hiyo elimu ni kiwango cha A’level politics very basic inaelezea mifumo ya serikali na jinsi zinavyofanya kazi.

Sasa kama katibu mkuu anahitaji hiyo elimu au Kigogo yeyote wizarani ambae ni senior civil servant au RAS na DAS ambao hawajui serikali inavyofanya kazi kama nchi bado ina safari ndefu sana.

Makatibu wakuu ni watu ambao wanatakiwa wajue hayo na zaidi, miongozo yote ipo kichwani, uwezo wa kupanga strategy ya kufikia sera, usimamizi wa sera, nani anafanya nini kwa wakati gani na philosophy za Plato na Aristotle zipo kichwani.

Huko tulipoiga hii mifumo na kutengeneza miundo yetu ya serikali foundation yake ni hao watu, ukiuliza huko serikalini wangapi washawahi ata kusoma Plato Republic sidhani kama wanafika 10%.

Sasa wataelewa vipi malengo hasa ya kuwa na wizara ya utumishi kama hawafanyi performance appraisal (hawa wanatakiwa kuwawajibisha wengine, kama wenyewe awawezi jisimamia).

Moreover ndio maana ya mantiki ya kuhakikisha katibu mkuu wa wizara ni genius uingereza katibu mkuu wa wizara unaangaliwa ufaulu wako toka shule ya msingi, tabia zako, maadili, na succession planning sio ya kitoto hadi kufikia hiyo nafasi una ufahamu mfumo mzima wa wizara unayokabidhiwa (technically wewe unaongoza nchi na makatibu wakuu wenzako).

Tanzania tunafanya ivyo kwa kiasi, serikalini ukiwasikiliza hawa senior servants ni wakurugenzi wa wizara tu ndio wenye hizo sifa za ulaya ndio maana huwa nasema mtu kama Dorothy Gwajima nchi nyingine ndio anaweza fikiriwa kuwa katibu mkuu katika wizara yake maana umdanganyi anajua kila kitu ndani ya afya. .

Sasa semina ya kuongelea siasa za A level, what a load of nonsense and a waste of tax payers money.
 
Back
Top Bottom