Uchaguzi 2020 Mama Samia: Nakubaliana na Makongoro Nyerere, CHADEMA ni jiko la mkaa huwezi kulikumbatia ama litakuunguza au litakuchafua na masizi!

Humjui mama Samia vizuri wewe, awamu ya nne alikua kinara wa kutoa mipasho kwa upinzani bungeni. Na hii ndiyo ilikua kete yake ya kuteuliwa kuwa mgombea mwenza wa Magufuli.
Hahaha mama kama mama, kwa kweli inapendeza sana kuwa na mgombea mwenza mwanamke.
 
Jiko la mkaa kazi yake ni kupika vitu ili viive na sio kukumbatiwa. CHADEMA, ni jiko la kuivisha agenda za haki, uhuru na maendeleo ya watu...
Faru John mbona anawakumbatia sana Wabunge Viti Maalum wa Chadema??
 
Humjui mama Samia vizuri wewe, awamu ya nne alikua kinara wa kutoa mipasho kwa upinzani bungeni. Na hii ndiyo ilikua kete yake ya kuteuliwa kuwa mgombea mwenza wa Magufuli.
ONGEZEA: Makamu wa mwenyekiti bunge la katiba, huyu ndiyo mama wa ile katiba pendekezwa iliyo chakachua report ya warioba.
 
Kukumbatia jiko la makaa ni sawa na kwenda kinyume na maumbile. Utakumbatiaje jiko utoke salama? Sasa CCM watu was dhuluma unataka kujichanganya na watu wa haki kweli utatoka salama!?
 
Mgombea mwenza wa CCM mama Samia Suluhu amesema anakubaliana na kauli ya Makongoro kwamba Chadema ni kama jiko la mkaa halikumbatiki...
Makongoro alipata kura 5 butiama alikozaliwa na anakoishi kura za maoni CCM.ndugu yake alipata kura 2 Hawa hawakubaliki hata ubalozi wa nyumba kumi kumi hawawezi kupata. Samia anamsikiliza na kumuamini ?
 
Kasema ukweli kwasababu vyama vingine vyote wamevikumbatia vikakumbatika. Chama cha CHADEMA serikali inajaribu kukikumbatia kwa namna zote za kuwatisha viongozi wake na wanachama lakini wamekataa kukumbatiwa kinafiki! Serikali ikijaribu kukikumbatia kwa nguvu lalima iungue na kuchafuka
 
Wamepanic mipovu inawatoka!! Kwanini hawaitaji CUF au NCCR? Mwaka huu Lissu atawanyoosha!!
 
CCM ni marehemu anaetembea kwa msaada wa dola!
Ni kweli Mkuu. Kuna kongamano la Injili lilliloandaliwa na Kituo cha Radio Safina Arusha leo tar 6/9 kwenye viwanja vya Magereza karibu na Uwanja wa Ndege wa Kisongo. Cha ajabu ccm wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Arusha pamoja na Assim Majaliwa wamekwenda kuuvamia na kuufanya ni wa Kisiasa.

Jana Kassim Majaliwa alikuwa kwenye kampeni Arusha na kampeni zao pamoja na kuwasomba watu kwa magari lkn bado haukufanikiwa kama ule wa Mh Lissu. Aibu tupu kwa ccm.
 
Yaonekana Mama amechoka na AMANI.
Aliheshimiwa kwa vile alikuwa na muonekano wa wenye uungwana
She is asking for trouble, trouble she will get.
 
Siasa ni sayansi bwashee!
 
Ni kichaa tu ndiyo atawaza swala la kukumbatia jiko la mkaa.

Jiko la mkaa linaheshimiwa mnoo na familia na kazi yake ni kupika chakula na sio kukumbatiwa
Jiko la mkaa linapika chakula,lakini unaweza kulikumbatia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…