Mama Samia Suluhu anajua kuongea Kiingereza?

Mama Samia Suluhu anajua kuongea Kiingereza?

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Hey peeps, let’s have some little fun....shall we?

Si vibaya kuuliza kama Mama Samia anajua Kiingereza [emoji1787].

Kwa ‘kujua’ namaanisha ana uwezo wa kuongea Kiingereza kizuri, kinachoeleweka, na kilichonyooka.

Mama Samia nishawahi kumsikia akitumia maneno mawili matatu kwa kuyachomekea katikati ya Kiswahili.

Haikuwa fursa nzuri ya kupima uwezo wake.

Mwenye kujua, mwenye video zake akitema yai, n.k., hebu tuwekeeni hapa tuone.

Na Kasimu Majaliwa naye je?
 
Kiingereza ni kiswahili cha dunia, ukiwa na madaraka halafu umepata elimu yako kwa lugha hiyo, ni aibu na fedheha kutokuijua fullstop.
Warusi, wachina, wakorea je? Ukiwa na akili za kitumwa kama zako huwezi kujikomboa. Kama wewe utaendelea kutoa mapovu humu JF kujikomboa kutoka akili za kitumwa itakuwa ni ndoto za Alinacha!!
 
Poor Nyani Ngabu! Kuna siku uliandika makala Moja kuhusu taratibu za ikulu kabla ya hapo ukagusia kwamba Elimu yako ni ya kidato cha nne. Kuna mambo mawili hapo ulidanganya na ukweli uliishia darasa la saba au kidacho cha nne ulipata ziro ambayo ni Sawa na darasa la saba tu!

Nyani Ngabu unaonaje ukiwa unasoma nyuzi tu au kuchangia kuliko kuendelea kujidhalilisha kwa kuanzisha mautumbo humu na kutujazia seva.
Kweli nilidanganya.

Mi wa darasa la 7 tu.
 
Warusi, wachina, wakorea je? Ukiwa na akili za kitumwa kama zako huwezi kujikomboa. Kama wewe utaendelea kutoa mapovu humu JF kujikomboa kutoka akili za kitumwa itakuwa ni ndoto za Alinacha!!

Nimecheka kwa nguvu ulichoongea hapa we kilaza, Warusi, wachina na wakorea wanapata elimu zao kwa kiingereza? Huyo anayejifanya anakienzi kiswahili ni kwakuwa hawezi kingereza cha kunyooka, na ukimsikiliza akiongea anachanganya kiswahili na maneno ya kiingereza mpaka inakuwa kinyaa.

Fuatilia viongozi wanaojifanya wazalendo, watoto wao wote wanasoma shule za kiingereza, na huwa wanacheka meno yote nje hao watoto wao wakiongea kiingereza, na sio wakiongea kiswahili fasaha.
 
Back
Top Bottom