Mama Samia Suluhu: Rais anawasalimia, anasema tuchape kazi tulete tija kwa Taifa letu

Mama Samia Suluhu: Rais anawasalimia, anasema tuchape kazi tulete tija kwa Taifa letu

Ukitaka kujua kuwa ww si wa muhimu ktk chama na serikali ni kipindi hiki ambacho hata ww hujui Rais yuko wapi na ni mwanaccm kindakindaki au hata kiongozi mkubwa tuu kwenye serikali.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mambo mengine ni ya kitoto sana. Yaani salamu mpaka amtume Samia? Anatusalimia kutokea wapi akiwa katika hali gani?
Hawa watu ni wajinga hakuna mfano. Ngoja tupenyezewe kapicha ka full na oxygen kisha waseme ni photoshop.
Alimlaza TL Nairobi na Belgium 2 years kwa maumivu makali sasa naye atalala muda huohuo
 
Leo Mama Samia ameanza ziara mkoani Tanga na akiwa kwenye kiwanda kimojawapo alichozindua kinachoshughulika na matunda wilayani Korogwe, alipata nafasi ya kusalimu wananchi baada ya kuombwa na mkuu wa mkoa wa Tanga ambapo alianza na salam kutoka kwa Rais Magufuli

"Kabla ya kuwapongeza niwasalimie salam za Rais anawasalimia, anasema tuendelee tuchape kazi, kipindi hiki tushikane tujenge mshikamano, tujenge upendo, tuchape kazi tulete tija kwa Taifa letu"

Baada ya salam hizo Mama Samia amewapongeza kwa kuwa na kiwanda kwani ni mkombozi.

Pia soma > Mama Samia: Katika wakati muhimu Watanzania kushikamana ni wakati huu, Si wakati wa kusikiliza maneno yanayotoka nje yakatuparaganya vichwa
Bwana Magu anawasalimia watanzania,
Hihihihihihihiiii,hahahahahaha,huhuhuhuhuhuhuuuu....acha nicheke kwa sauti ya kimzimu
 
Nilimsikia na kumuona runingani Waziri Mkuu wangu Majaliwa (akiwa kule Njombe) kuwa Rais Magufuli anawasalimia na kuwataka kuchapa kazi. Hapa Tanga nilipo pia, mubashara kabisa nikamsikia Makamu wa Rais Mama Samia akiwaambia wana-Tanga na watanzania kwa ujumla kuwa Mhe. Rais Magufuli anawasalimu na kuwataka kuchapa kazi kwa maendeleo ya taifa letu pendwa.

Bado sijasikia viongozi wangu wa CCM wakizifikisha salamu za Mwenyekiti wetu kwa wanaCCM na watanzania kwa ujumla. Dr. John Pombe Magufuli ni Rais wetu. Ni mkuu wetu wa nchi. Ni Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa na Amiri Jeshi wetu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama. Hajawahi 'kutuma salamu zake' kwa namna hii. Kwasasa anatuma salamu hizo akiwa wapi na akiwa kwenye hali gani?

Alivyozoeleka miongoni mwetu ni kuwa zinapofikishwa salamu zake, yeye binafsi hupiga simu kwa mfikishasalamu husika na kuzungumza na wananchi mubashara na kutoa maagizo na maelekezo. Imewahi kutokea kwa Makonda wa Dar na Chalamila wa Mbeya. Kwanini Majaliwa na Mama Samia hawajapigiwa na Rais na Rais kuongea na wananchi wake waliomchagua na wanaompenda katika kuchagiza salamu zake?

Rais Magufuli ana utaratibu wake. Si mkaa-kimya kwenye kuongea na wananchi wake. Si mkaa-kimya katika kufikisha ujumbe wake. Si mkaa-kimya katika kujibu hoja. Kwasasa yu wapi na yu katika hali gani? Mama Samia, WM Majaliwa na Balozi Kipilimba tusaidieni kujua hayo kumhusu Rais wetu.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa safarini mkoani Tanga)
 
Inawezekana mama Samia mwenyewe hajui Magufuli alipo[emoji16][emoji16]
 
Mbinu za kisiasa hubadilika kulingana na wakati!
Bwashee! Sisi watumishi wa umma pia tunatambulika kama Public Servants!! Huwa tunafanya kazi zetu katika mazingira ya uwazi!

Ni wakati sasa wa kutuambia, mtumishi mwenzetu wa umma yuko wapi?
 
Huenda amezungukwa na mitungi ya oksijen, na labda hajitambui. lakini kwasababu Raisi wetu mpendwa anatupenda sana sana ametuma huo Ujumbe labda kwa kupitia nyenzo ambazo sisi Raia hatuzijui.

Labda ni zilezile za madaha ya Gambosh
 
Back
Top Bottom