Mama Samia ungefuata ushauri wangu wa tar29/03/2021" Mapema tu baada ya kuapishwa aibu hii isingekukuta

Hivi nyie mnaosemaga Kuna Rushwa ya kutisha ni pesa za Umma au ni zipi? Mbona sisi huku chini tunakofanya kazi hatuoni hayo mnayoyasema?

Nachojua Rushwa pekee kubwa watu wanayopata ni aidha Kwa Ajili ya kupendelewa kazi au tenda ambayo technically Haina athari hasi kwenye uchumi au Kwa mtu mmja mmja.

Tofauti na hiyo wengine wanakulaje pesa za Rushwa kubwa kubwa hebu tupeni mbinu maana hela za serikali ziko kwenye mifumo.

Rushwa za hivyo hazidhibitiki maana ni makubaliano ya watu ila hakuja anaechukua hela ya serikali na kuila na Mimi nikipata nakula.

Tofauti na hiyo ni Rushwa ndogo ndogo za Polisi,Mahakamani , hospital na labda Wakusanya Mapato kutopeleka hela zote Serikalini.

Sasa hayo nani amewahi yamaliza?
 
Hili la kujenga vyumba vya kupanga Nairobi waachane nalo, Kuna wale vijana waliochukuliwa kwa ajili ya kilimo siwasikii.
 
Eti wizara ya mambo ya nje inatoa pesa Tanzania inaenda kujenga majengo kenya
 
Mkuu upo serious? Sasa kama unakubali kuna kutoa rushwa tenda ipatikane, ukinipa rushwa ukapata tenda nashindwa vp kukuambia hii tenda ongeza B1 hapo juu ukilipwa nitakupa maelekezo halafu mimi nikakaa na kamati yangu?
 
Moja ya ufisadi mkubwa ni kuanzisha mradi wa majengo kenya na Kinshasa kwa mabillioni ya walipakodi
 
Nikishaona mtu anaandika bila kuweka koma, nukta ama kuzingatia matumizi sahihi ya herufi kubwa na ndogo, huwa namdharau sana.
Utachelewa sana,

Dhahabu mara zote Huwa imefichwa gizani na imechangamana na Kila aina ya uchafu.

Pembua pumba na Mchele maisha yaendelee.
 
Uwezo wake ni mdogo kung'amua mambo..
 
Government spending on luxurious goods ndio inaporomosha thamani ya Shilingi?

Halafu, japo simpendi Mwigulu, lets be fair, niulize kitu. Ikiwa gari za seikali hazitakuwa hizi Landcruizer na Prado, ambazo ziko katika muongozo wa serikali, circular, juu ya government issue vehicles, mbadala wake uwe gari gani? Tusilaumu viongozi wa serikali kutumia V8 wakati hatusemi watumie nini badala yake.

Kumbuka wakati wa Nyerere government issue vehicles zilikuwa ni Land Rovers, ambazo kwa sasa hazipo au model iliyopo huenda hata bei yake ni juu zaidi ya Land Cruiser, na haifai tena kwenye off roads.

Kwa hivyo basi, kama sio Landcruisers Wagon V8 na Box body (Dube) ambazo zinatumika sana Halmashauri za miji na majiji, serikali itumie gari gani? Maana hata Polisi sasa tumewatoa kwenye Land Rovers na kuwaingiza kwenye Land Cruisers Pick ups.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…